Utabiri wa Hemed Kivuyo kwa Manara watimia. Alitoa onyo hawakusikia

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Lile kanjanja lialia shabiki la kutupwa la utopwinyo fc lililokuwa ITV Hemed kivuyo last year lilitoa onyo kuhusu ALHAJI ALBINO na alichosisitiza kwamba popote hyo jamaa alipo basi matatizo yake binafsi huyasukumia yawe ya taasisi, naaam yameonekana kwenye suala la Karia kuna wengine walidai eti Karia aliibeza yanga utajiuliza umbali wa kutoka alipokuwepo TAKADINI NA KARIA hapo kati hakukuwepo na kina GHALIB, SENZO, MWANASHERIA, INJINIA?

Hawakusikia Karia? Waliogopa? Hawana uchungu na yanga kama SOPE? Haya tujikumbushe onyo hili la mwaka jana.
***************************************************************

Anaandika Hemed Kivuyo.

Wananchi leo ni Siku yetu, tusherehekee tufurahi lakini tuwe Macho na Haji!
Haji atatufurahisha kwa mbwembwe zake na Kejeli zake kwa Mabosi wa Simba, tumsikilze, tumshangilie ila tusimtillie maanani , Haji anawasema Viongozi lakini anaikwepa kuisema Simba Direct.

Wananchi tunapaswa kufahamu ya kuwa Manara anawachukia Baadhi ya Watu Pale Simba lakini Haichukii Simba !Wiki nzima iliyopita Haji Ametawala kwenye Vichwa vya Vyombo vyote vya Habari kabla ya Kufunikwa na tukio la Hamza mwishoni Mwa wiki.

Hakuna Mwanasimba anayeamini kuwa ni Haji yule yule Bingwa wa Misemo na Mchambaji wao Maarufu ndiyo huyu huyu anayewaponda sasa Viongozi wao leo, ni Viongozi wale wale wa Simba aliowasifia kwa Mbwembwe nyingi huko nyuma anaowasema leo, hili linapaswa Kutupa Tahadhari kubwa!

Ukweli halisi ni kuwa Haji hawezi kuwa na Mapenzi na Yanga hata kidogo, Haji ni aina ile ya Watu wasiotaka kushindwa, kupenda Kushindana na wanaoupenda Umaarufu bila Kujali unapatikanaje, kutokana na Sifa hizo ilikuwa ni Vigumu sana kwa Haji kukaa kimya, hivyo ilimlazimu kutafuta jukwaa la kurushia Vijembe na kutoa nyongo zake, haji hakutaka kabisa akae nje apoteze Umaarufu wake.

Hapa tukachemka Klab kubwa na yenye Historia tumekubali igeuzwe kuwa Jukwaa lake la kurusha makombora kwa watesi na mabwana zake, Hizi mmesahau Clip zake zilizovuja akiwaambia kuwa yeye Ni Simba kulikoni Barbra na Viongozi wengine??

Mnakumbuka alisema watatoka watamuacha, inawezekana kaamua kutumia njia hii ya kuegemea ili awatoe watu pale kwenye Klabu aliyojinasibu ya Babu yake.

Hatujui na hatujaelezwa vizuri lkn waoanga mikakati wameonelea Jukwaa lililo Sahihi imekuwa ni Yanga kwa sasa ila Ambacho Sijui ni kama Yanga kweli ilikuwa ni Chaguo la Awali baada ya Kutemwa Simba?

Dalili za Awali zilijionyesha anataka kwenda Azam mpaka akapiga Picha na Bakhresa akiwa Dubai, huenda huko Aligonga Mwamba au Azam hawakutaka Vita na Simba ili kulinda brand yao maana huu ugomvi Ni wa MTU kudai au kuoambania maslahi yake Binafsi lakin anakuja kuzitumia Taasisi.

Tuwe nae makini mno au laa tumlishe Yamini maana siku akiondoka kwetu haya ya Simba hatakuwa maradufu kwetu.
Siamini Kama amehama kimoyoni, Ni ghadhabu tu na pia anatafuta ulinzi kwetu, Sasa Angalia Nugazi na BUMBULI wamekosa Raha.
Kwanini Haji ni Bomu linalosubiri kutupasukia?

Wazaramo wa mbele huko wana Msemo wao Maarufu unaosema “Dont Make Decision when ur angry” Yaani usifanye Maamuzi pale unapokuwa na hasira, ni Dhahiri Haji amefanya Maamuzi yake akiwa na hasira, na ili kudhibitisha Hilo ni kwamba pamoja na Simba , Mo na Babra kuamua kutomjibu Haji lakini yeye Amekomaa na Ishu hiyo kila Anapozungumza, Anapotweet ishu ni ya hao tu, hii ni dhahiri Hasira bado hazijamtoka bwana huyu, na kitendo cha kufukuzwa Simba kimemuumiza sana lkn pia hakuwa kutegemea, aliamini mashabiki wa Simba wangemtetea lkn kiukweli nao walikuwa wamemchoka kwa tabia zake za ubinafsi na lugha mbaya wa Waandishi na makundi mengine, umimi uliopitiliza, ujanja ujanja wa Kariakoo ktk kuitibu njaa.

Sasa Ikitokea siku Atakapomaliza hasira zake kwa Simba ndipo siku za kutuhujumu sisi itakapoanza, Kwa Historia ya Haji na Kila Alikopita katika Maisha yake iwe ni Kisiasa, kijamii na sasa Kimichezo hajatoka Salama, Maisha ya Binadamu yamepambwa na Matukio ya Kihistoria kama Alivyosema Mzee wetu Mwinyi Senior ya Kuwa Maisha ya Binadamu ni Hadithi basi kuwa Hadithi nzuri itakayosimuliwa, kwa Ndugu yetu Haji Hadithi yake Mpaka Sasa Imejaa Matukio ya Kuhuzunisha kama sio Kuliza Kabisa.

Pita Ndani ya Chama Cha CUF toka alipokuwa huko kisha Mfuate CCM halafu pitia hapo Msimbazi kwa Mikia utajua Haji Manara ni Nani. Hili nalo ni la kuzingatia sana.

Katika kitu Haji Amebarikiwa ni kujua kucheza na mind set za watu ila kitu. Alichoshindwa kujizuia nacho ni Tamaa na kupenda Ukubwa kote huko Tamaa ndio imeharibu na kujiona Mkubwa. Hata kwetu Tatizo linaweza kuwa lile lile.

Hivi sasa Tunashuhudia Haji akitumia Nguvu kubwa kujibrand Binafsi kuliko Timu yetu hii maana yake nini? Maana yake ni kutaka kuaminiwa na Wananchi halafu atumie fursa hiyo kukidhi haja zake, lakini Pia huko mbele ikitokea kutokuelewana na waliomleta basi apate kusema yeye ndiye aliyeibeba Yanga, Ifahamike kote Haji ameingia Yanga Ameikuta Yanga imejipanga kwenye Maeneo mengi ili kufanya Vizuri, ameikuta Yanga Imeshafanya Usajili wake, Imeshaanda siku ya Mwananchi kwa Asilimia 100, Imeshazalisha Jezi Mpya na Mengi mengineyo.

Ndugu zangu wananchi wekeni Kumbu kumbu hii Yanga ikifanikiwa Kubeba Ubingwa Mwaka huu, Haji atajinasibu kuwa ni Mchango wake Yeye, Yanga imekuwa inajaza Uwanja kwenye Siku ya Mwananchi na Mechi za Simba na Yanga hili pia Haji atajinasibu ni Yeye huko Mbele.

Haji anapenda sana kuwa karibu wa kupitiliza na Wachezaji Mastaa wa Timu kwa Malengo yake binafsi kama ilivyokuwa Simba hili nalo Viongozi wawe nalo Macho, mikia Kuna safari walijua wanamuacha kimkakati sio kuwa walikuwa wanamuonea, Uhujumu wa Timu huanzia hapa endapo ataona Malengo yake hayatimii. Maana pia yeye hupenda saaana kuishi Maisha ya gharama na ya juu mnadhani kwa Mshahara upi ataenda likizo huko Dubai, Hispania na kwingineko??

Wale Simba majasusi na bado hajagombana nao wotee, watamnunua ambao Wana Mahusiano nae mazuri.. Viongozi muwe nae makini saana huyu Mtu.

Mimi Binafsi namfahamu huyu tangu akiwa Uhuru, na sijaanza leo kumpa live, nilimpa makavu akiwa Mkiani kule na nitaendelea kumpa, maana Sina Imani nae kabisa.

Wananchi Wenzangu tuombe Mungu atupe Maisha Marefu ili tushuhudie Siku Haji akija Kujinasibu kwa Haya na mengine mengi ya Uongo ya kutuharibia Timu yetu, inaweza kuchukua Miaka kadhaa ila Naamini ipo siku tu bomu hili litapasuka.

Kumbukeni mamia ya wananchi wanaoipenda Yanga na kujua miiko yake hawajafurahishwa na hili, hivi vilabu vina Mila na miiko yake.

Wahenga waliwahi kupata Kusema kuwa Siyo kila mgeni anapaswa kuingia Chumbani, wengine Mwisho Ni sebuleni tu.

Tujiulizeni Sasa sisi HAJI SUNDAY MANARA ambaye hata Mwanachama wetu Sunday Manara alisema huyu Ni Simba, tumemkaribisha mpaka wapi? Liwe swali la Tafakari tunapoenda kuwaona mashujaa wetu.
 
Ngoja niroll rizla 2 tatu ndio nije baadae kusoma hili gazeti

Hakika msokoto unahitajika hapa. Juzi alisema Haji MANARA amejaa hekima leo kaja na stori nyingine.
IMG_0665.jpg

 
Ngoja niroll rizla 2 tatu ndio nije baadae kusoma hili gazeti
Usilisome mkaanza kumtukana Kivuyo, he saw this coming last year August kilichobaki ni Alhaji Takadini Muyabebe matatizo yake binafsi yawe ya taasisi yenu ya utopolo
 
Mimi najua kukaa na mtu bila kukwazana ni ngumu Utopolo wote wanajua Manara amefata Yanga vitu viwili cha kwanza pesa na pili ugomvi wake na Babra.

Utopolo kaeni vizuri tu ila siku mkikorofisha akirudi Simba mtalia kwakuwa atakuwa anajua siri zenu zote
Mimi navyomjua Haji kwa hali inayopitia Simba kwa mwaka huu ingekuwa Yanga angetania mpaka kero ila nachompenda pamoja na kuwa Yanga lkn hatutanii sana that's why hatumii kinachouma ni kufungwa na hawa utopolo na kukosa ubingwa.

Laiti tukipata ubingwa mwaka huu hata haji mwenyewe hatakuwa na nguvu ya kuiponda sana Simba tunajua wazi huyo ni mwenzetu mwaache atafute hela ila ipo siku atarudi Simba na akirudi atakuwa ana siri zenu zote mtaliaa kima nyie utopolo
 
umeandika nini kwanza, hebu nifupishie
Hujui kusoma bwasheeee?? Ni utabiri wa mwaka jana na unaanza kutimia kipande kwa kipande,takadini watu wanamjua vizuri tangu miaka hiyo akiwa CUF, NNCR akidhaminiwa na mzee tozi kugombea udiwani walionya tu lakini mnashaupaza shingo na kujitoa fahamu.
 
Na kweli jamaa kaanza kujisifu sana kwamba mafanikio ya Yanga yameletwa na ujio wake, Hemed Kivuyo anamfahamu vema sana mtu huyu bila shaka.
 
Hujui kusoma bwasheeee?? Ni utabiri wa mwaka jana na unaanza kutimia kipande kwa kipande,takadini watu wanamjua vizuri tangu miaka hiyo akiwa CUF, NNCR akidhaminiwa na mzee tozi kugombea udiwani walionya tu lakini mnashaupaza shingo na kujitoa fahamu.
okay
 
Back
Top Bottom