Wakubwa nina mtaji wa shilingi milioni mbili na nataka nifanye biashara.
Je, biashara gani ninaweza kufanya kulingana na pesa hiyo?
Nimetafakari sana ila nakosa kujua kwa usahihi biashara gani inanifaa.
===========
SIMILAR CASES:
===========
May 18, 2012:
Oktoba 09, 2014:
Oktoba 22, 2014:
Aprili 13, 2015:
-----------
12 Aprili 2016
Je, biashara gani ninaweza kufanya kulingana na pesa hiyo?
Nimetafakari sana ila nakosa kujua kwa usahihi biashara gani inanifaa.
===========
SIMILAR CASES:
===========
May 18, 2012:
May 10, 2014:Msaada jamani nataka kufanya biashara nina 1m. Sijui nifanye biashara gani?
May 16, 2014:Ushauri wa kibiashara! nina mtaji wa milioni nne mkononi...
Nafikiri nianzishe biashara! ushauri wenu tafadhali ni biashara gani itakayoweza kunilipa kirahisi! m
Mhauri mmoja kaniambia nifungue mpesa-airtel money na pia niuze vifaa vya simu! Mwingine kanishauri niuze yebo yebo niwe naagiza kutoka kiwandani na kuuza huku kwa jumla jumla!
Bado sijafikia maamuzi nipeni ushauri kati ya hizo mbili au biashara nyingine!
Ahsanteniwajasiria mali wenzangu
Habari zenu wadau na wakuu wa jamiiforums,
Mimi ni kijana wa elimu ya chuo kikuu, nimejizatiti hasa baada ya miezi miwili hivi kupita, nisaifiri kwenda Kaskazini kwa ajili ya kuanza biashara ndogo ndogo ya ununuaji wa madini aina ya dhahabu kutoka kwa wauzaji wadogo wadogo.
Wakuu, nimekuja hapa mbele yenu kuomba mwongozo juu ya ufanikishaji bora wa biashara hii, isitoshe mimi ndiyo mara yangu ya kwanza naingia katika soko.
Kwa kiasi fulani nilishaona dhahabu ikiwa inauzwa katika vipimo tofauti tofauti vyenye madaraja tofauti tofauti ya bei kama kuanzia shs elfu 30 na kuendelea.
Naombeni mwongozo kwa mnaoifahamu vizuri biashara hii,changamoto zake ni zipi?
NB; Pia kama kuna wazo lingine la biashara linaloendana na hili, tafadhali usisite kuninong'oneza!
Oktoba 09, 2014:
Wadau nimekuja kwenu nina vijicent kidogo tu mil 2. million mbili.
Nahitaji kuanza biashara mi nipo Dar; nahitaji biashara ambao ntaendelea kuikuza kadri iwezekanavyo.
Naomba mnisaidie kwa huo uwezo wangu naweza fanya nini. Naamini kuwa wajasiriamali wengi ambao wanaweza kunishauri nini cha kufanya.
Oktoba 22, 2014:
Novemba 10, 2014:Wakuu mimi ni kijana wa Umri wa Miaka kama 30 hivi, Najua nimechelewa kutoka, Ila ni kutokana na kutokea kwenye familia ya kawaida sana. Sasa wakuu nimejichanga changa nimesave kama ka-milioni na taka kufanya jambo niongeze kipato.
Mnanishauri nifanye nini?
Feb 18, 2015:Nisaidieni jamani wapendwa nifanye biashara gani ili niweze kijipatia kipato angalau niweze kujikimu kimaisha.
Nina mtaji wa sh 1,500,000.00/= [milioni moja na nusu]
TUSAIDIANE JAMANI. MWENYE MSAADA ANI PM BASI.
Habari wakuu,
Hivi wanabodi ukiwa na mtaji wa Tsh 5 million unaweza fanya mradi gani ukatoka?
Naombeni mawazo yenu wakuu
Aprili 13, 2015:
Ndg,
Bila shaka muwazima, mungu azidi kuwatia pumzi pamoja na upeo wa kufikiri.
Mimi nina milioni 1(1,000,000/=) Tsh.kama kianzia. Ninapenda nami siku niitwe tajili ktk kundi la watu ! Naomba msaada wa mawazo nifanye nn ili niweze kufanikiwa? Hii Pesa nimeipata kwa kufanya kazi za watu hivyo nimechoka kuajiliwa nami napenda nijiajili.
Nitafurahi sana kama mtakao npe ushauri mtanitajia na namna ya kukabiliana na changamoto nitakazo kutatana nazo katika kuendesha hiyo shughuli nitakayo ianzisha.Nipo tiari kuishi sehemu yeyote si mjini wala kijijini tu!
Nitashukuru sana kama nitasaidiwa
-----------
Biashara
Mtaji wako waweza kuwa mdogo au ni mkubwa, hii inategemea na aina ya biashara utakayo taka kuwekeza, ningependa kukupa angalizo kidogo, bila shaka litakupa mwangaza kidogo kabla ya kuwekeza ktk biashara yoyote.
- Kwanza tafuta biashara ambayo itakujenga kiakili, ambayo haitakufanya kuwa mtumwa wayo, ambayo itakupa fursa ya kuwekeza kichwa pia, OJT au OBT (ON JOB/BUSINESS TRAINING), Hii inamaana wafanya biashara huku ukijifunza kuwa mweredi zaidi. Wekeza kichwani kwanza. Benjamin Frankilin aliwahi kusema:- "if a man empties his purse into his head, no man can take it away from him. An investment in knowledge always pays the best interest."
- Biashara nzuri ni ile inayogusa jamii, kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, hii yahitaji muda kidogo kufanya kautafiti, yaani ni kutafuta pengo na kulijaza ama kuwa suluhisho la changamoto.
- Biashara nzuri ni ile ambayo itakupa passive income au Residual Income, itakayo kupa Inner Freedom, Location Freedom, Time Freedom na zaidi baada ya miaka mitatu au mitano yaweza kukupa financial freedom pia, tena ambayo yeyote aki – copy na ku-paste (kwani ni kawaida) biashara hiyo bado kwako itakuwa faida, yaani ambayo hautakuwa na choyo kumwelekeza mingine jinsi ya kufanya.
- Tafuta Biashara ama fursa itakayokupa changamoto na kukupa ubunifu wa kupambana na changamoto hizo, kumbuka tunakua kutokana na changamoto tunazo kutana nazo kila siku, kubweteka ama kufanya kwa mazoea hakuletelezi kukua.
- Pia ambayo itaenenda na mtaji wako, kwa kuwekeza kwanza kidogo, labda kama laki 4 kwanza na elimu (kwa gharama ndogo au bure) la namna ya kufanikiwa katika biashara hiyo la namna ya kuweka malengo na kufanikiwa. Tumia muda wa kutosha kujifunza kabla ya kutumbukiza pesa, jiridhishe kuwa hii biashara itakutoa. Abraham Lincolin alisemaga zamani – "Give me six hours to chop a tree and I will spend the first four sharpening the axe."
- Katika karne hii ya sayansi na teknologia, fursa za biashara ziko za aina nyingi sana, ni juu yako kutafuta biashara sahihi na kuwekeza, usiangalie iliyorahisi sana au mazoea, au ambazo kila mtu anakimbilia, tafuta iliyohalali hata kama watu watakwambia ni ngumu, kumbuka wengi wanaosema biashara Fulani ni ngumu, asilimia kubwa hawajawai kuifanya, ama walisikia kuna mtu kajaribu kashindwa pasipo kujua kashindwaje, wao wanabeba bango kuwa ni ngumu, wanakuwa wanachagizwa na woga zaidi kuliko uhalisia.
- Kila la kheri, ni PM ukiwa na swali lolote.
12 Aprili 2016
Habari ya muda huu wadau wenzangu. Nilikuwa na wazo la kufanya biashara kwa kuanza na mtaji wa milioni mbili, sasa bado sijajua uhakika kamili kwamba ni biashara gani naweza kuanzisha na ikanipa faida nzuri kwa kiasi hicho cha mtaji. Ahsanteni...