Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Kama una leseni na muda nunua TVS bajaj used ya 4m zipo nyingi tu ukomae nayo mwenyewe kufunga ef30 kawaida sana wanapiga mpaka 50,60 kwa siku.Utatumia kama laki 2,3 kufanya service ndogo inayobaki 800k acha kwenye acc kwa ajili ya dharula.

NOTE:Brand ni Tvs tu si nyingine
Wapi hiyo mkuu wanapoingiza 50-60 per day
 
Nimerudi

Wewe uko wapi kwa sasa? Na biashara ya kufanya mfano kutoa bidhaa nchi jirani na kuleta huku utaweza kuimudu?.

Uganda kuna kadeti na mashuka na pia unaweza kutoka huku na mchele kutoka kahama na ukapeleka uganda si lazima uchukue mwingi ila unachukua kiasi kwa ajili ya kukuza mtaji, mfano unachukua mchele wa 3 milioni halafu utakavyouza huko pesa hiyo hiyo unafanya kununua hayo mahitaji uliyoyafata.

Biashara ya kadeti ni kwa huku Dar ndio naona itafaa au kama kuna fursa kwa dodoma pia sio mbaya
 
Kaka samah nahitaj muongozo vizur hyo biashara ya mchele
 
Kuna viwanda sasa hivi vinakamua mafuta toka kwenye tairi chakavu huo mchakato unaitwa pyrolysis.

Na mafuta yanayokamuliwa yanaitwa IDO(Industrial Diesel Oli) haya yana soko kubwa sana kwenye viwanda vyote vinavyotumia mfumo wa BOILERS kama chanzo cha NISHATI

Tairi moja chakavu unainunua kati ya 1000 na 2000 nawe unaenda kuuza tani moja (approximately tairi 16 kwa laki moja.. Ukitoa mtaji na usafiri hukosi 50,000 faida kwa kila tani

Tairi kwa wingi zinapatikana kwenye mayard makubwa yenye kampuni za usafri
Viwanda vyenye kuhitaji hiyo malighafi hivi hapa
Mvuti Chanika
Kibada Kigamboni
Madafu Kibaha
Bagamoyo
Tegeta Dar

Naamini nimetoa maelezo ya kutosha sana
TATIANA
aliyetegwa
kwa mtaji wa milioni kumi mtu hawezi fanya hii kitu kwani kwanza upatikanaji wake wa hiyo bidhaa mpaka aaanze kuitafuta then mpaka apate tani aisee but ni wazo zuri excacly kwa mtaji wa 1m to 2 m
 
Dili ya direct tairi chakavu kwa mtaji wa nusu ya hiyo hela. Masoko yapo machaka ya kupata mzigo yapo
Dili nyingine ya moja kwa moja oil chafu. Faida yake haina hasara hata siku moja.
Elezea hizo biashara kwa mapana mzee.
 
Wakuu kama kichwa cha habari hapo juu. Najua hapa kuna wajuzi wa aina mbalimbali. Nimeona nililete kwenu kwa msaada zaidi.

Kuna dogo anataka kupiga mishe. Biashara gani inaweza kumuingizia milioni 1.5 hadi 2 kwa wiki kwa mtaji wa milioni 10?.

Karibuni
 
1.5M mpaka 2M kwa wiki, maana yake ni 6M mpaka 8M kwa mwezi. Hiyo ni 60% mpaka 80% ya mtaji wake (10M).

Uanze biashara leo, ndani ya mwezi upate 60% mpaka 80% ya mtaji wako wote. Hizi papara ndio zinatukwamisha vijana wengi. We want overnight success!

Ngoja waje wajuvi, nisije onekana mnoko!

Back
Top Bottom