Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Fanya kautafiti cha Bei ya mazao ya nafaka Sokoni - DSM.

Kisha Kodisha Lori, nenda Mbeya kanunue mzigo mkubwa kisha uje uwauzie kwa Bei ya jumla.
 
Habari kuna sehemu nilikuwa nimeajiriwa sasa nimejikusanya na kupata milioni 5 baada ya mkataba wangu kuisha nifanye biashara gani ya kuingiza faida ya isiyopungua 30,000 kwa siku, ushauri wenu ni muhimu sana, asanteni sana.
 
Habari kuna sehemu nilikuwa nimeajiriwa sasa nimejikusanya na kupata milioni 5 baada ya mkataba wangu kuisha nifanye biashara gani ya kuingiza faida ya isiyopungua 30000 kwa siku ushauri wenu ni mhimu sana asanteni sana.
Mkuu unafahamu kuendesha boda? Kama unafahamu ungechukuwa 2M ukanunua pikipiki ukapiga kazi.

Kama haufahamu au hauna interests basi tafuta mtu unayeweza kuingia nae mkataba umpe aendeshe yeye. Hautapata 30K kwa siku ukimpa mtu ila angalau unaweza kufikisha nusu yake.

Kuhusu changamoto za bodaboda mkuu usijali sana maana kila kazi ina changamoto zake. najua kuna watu watakwambia boda achana nayo waendeshaji ni pasua kichwa.

Sasa wewe badala ya kusikiliza changamoto, fanya analysis ya hizo changamoto zote kisha utafute njia za kuzitatua moja baada ya nyingine. Ukisimamia vizuri bodaboda, baada ya muda unaongeza ya pili. Mwishwe unanunua bajaji, kisha IST, na badae inakuwa coaster.

Baaada ya miaka mkuu unamiliki basi. Mie siyo motivation speaker ila nakupa tu some insights maana we unaweza ukawa hauna hili wazo. Mkuu ukitajirika usinisahau na mie. Utanikumbuka mkuu.
 
Mkuu unafahamu kuendesha boda? Kama unafahamu ungechukuwa 2M ukanunua pikipiki ukapiga kazi.

Kama haufahamu au hauna interests basi tafuta mtu unayeweza kuingia nae mkataba umpe aendeshe yeye. Hautapata 30K kwa siku ukimpa mtu ila angalau unaweza kufikisha nusu yake...

Ushauri wako ni mzuri, ila kwa tahadhari ajitahidi kupata mtu mwaminifu.

Kuna mtu alichukua mkopo akanunua pikipiki ya biashara, aliyefanya nae biashara hakuwa mwaminifu. Alihisi kuvurugikiwa akili.

Labda kama anaweza kusimamia kwa ukaribu zaidi.

Ama sivyo, afanye biashara ya nafaka kama vile mahindi, mpunga nk. Kwa baadhi ya mikoa mwaka huu kumekuwa na ukame, kwahiyo akibahatisha kununua gunia kadhaa kwa bei nzuri, anaweza kupata faida kwasababu bei ya nafaka inazidi kupanda
 
Back
Top Bottom