Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari wa Kenya atengeneza Wakili wa kisasa mwenye ujuzi wa Sheria zote za Kenya

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Wakati Naftal Obwoni alipokuwa shuleni, baba yake aliachishwa kazi bila taarifa, jambo lililosababisha kesi iliyochukua muda mrefu dhidi ya mwajiri wake. Obwoni alishuhudia kwa macho yake mapambano ya baba yake kupata haki, na hii ilikuwa kwa sababu baba yake hakuwa na uelewa wa mfumo wa kisheria na mifumo ya mahakama ya nchi.

Kutokana na changamoto hiyo, alianza kutafuta suluhisho kwa Wakenya wa kawaida ili waweze kupata habari kuhusu masuala ya kisheria na mifumo ya mahakama ya Kenya.

Obwoni alisomea IT na akaendelea kutoa ufumbuzi kwenye mambo kadhaa, akitumia vema fursa ya teknolojia mpya zinazotoka.

Moja ya uvumbuzi wake ni Wakili, Mwanasheria wa kisasa anaeendeshwa na akili bandia mwenye ujuzi wa sheria zote za Kenya na mifumo ya mahakama.

Unachohitaji kufanya ni kupata Wakili kwenye simu au kompyuta, andika swali lako kwa Kiswahili, Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, au Kiitaliano, na majibu yatakufikia.

Obwoni anasema Wakili ameandaliwa kutoa majibu kwa Kiingereza, Kiswahili, Kihispania, Kiitaliano, Kifaransa, na Kichina.

Ikiwa una swala lolote linalohitaji ufafanuzi wa kisheria wanatakiwa kuandika hapo kwa Kiswahili au Kiingereza, Mwanasheria huyo wa kisasa anayeelewa sheria zote katika nchi hii ataweza kukushauri, kutoa maelezo ya kisheria, na kukuambia vipande vya katiba vinavyokupa njia ya kuchukua," anaelezea jinsi Wakili anavyofanya kazi.

Wakili imeandaliwa kwa lengo la kuwahudumia wote wanaovutiwa na masuala ya kisheria, kuanzia kwa Mwananchi wa kawaida hadi wataalamu wa sheria na hata taasisi zinazotaka kutunga nyaraka za kisheria.

Citizen TV
 
Ila usije mchukua huyo wakili ukasonga naye mahakamani, utafungwa 😄!.
 
Back
Top Bottom