Serikali inashindwa nini kutunga sheria ya mamlaka ya kuendeleza tafiti na bunifu za Teknolojia

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Siyo siri,
hatuwezi kuendelea kwa kutegemea ujimba tunaoukumbatia. Tunajua kwamba serikali inajenga hofu kubwa sana kwenye suala la mawasiliano kwa sababu mpaka leo inajiweka mbali kwenye maendeleo ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano.

Dunia inakimbia kwa kasi mno, na sasa akili bandia imeshatamalaki na hata hapa nchini wanufaika wa matumizi ya akili bandia wamezidi kuongezeka. Tunaishi kwenye ulimwengu wa mtindikio wa teknolojia isiyo na ukomo. yaani kila siku kuna jambo jipya linaingizwa kwenye mawanda ya sayansi na teknolojia.

Mtaalam wa sayansi bwana Elon Musk ameweza kugusa nyanja karibia zote za teknolojia akiwa ni mbobezi wa teknolojia ya mawasiliano. Ameweza kuunda Neuralink inayodeal na sayansitiba (Gaia) na anaendesha tafiti kubwa za kuendelea afya ya binadamu, Ameunda Space X inayodeal na sayansi ya anga za juu na makapuni kedekede kuanzia mawasiliano, magari na kadhalika.... Hayo yote yamewezekana kwa sababu nchi aliyopo ine sheria nzuri inayolinda, kuendeleza na kukusa sayansi bunifu.

Sisi hapa Tanzania, ukiangalia sheria zinazohusu TEHAMA sehemu kubwa imejikita kwenye udhibiti na kuminya uwezekano wa kwenda miles za ubunifu na sayansi mawasiliano. tunayo NIMRI ambayo inasimamia na kuratibu tafiti za sayansitiba ambapo ukiangalia sheria yake imejikita kwenye kutoa ithibati kwa wanaofanya tafiti za tiba mbalimbali. Lakini haina maabara za kuruhusu waTanzania kufanya tafiti kwenye maabara hizo. Vivyo hivyo tuna COSTECH ambayo inashirikiana na UNESCO nchini kuendelea bunifu za kisayansi, zaidi ya kuwatambua wabunifu haina uwanja wa kuwapatia watafiti wa bunifu za kisayansi kufanya yao. Tunayo TCRA ambayo ni mamlaka ya mawasiliano yenye kazi kubwa ya HACKING na Regulating matumizi na watumiaji wa sayansi mawasiliano...


Ni wakati sasa, Serikali ikaliomba Bunge kutunga sheria ya kuunda chombo cha kuendeleza tafiti za kisayansi hususani tafiti bunifu. kiandae maabara na karakana nchi nzima kuruhusu wabunifu wanaochipukia kujitokeza na kufanya majaribio ya bunifu zao. Inaweza kufanyakazi kwa ufanisi ikishirikiana na maabara au karakana za VETA na SIDO zilizosambaa nchi nzima. Pia sheria ya kuunda JWTZ ifanyiwe marekebisho kuongeza kipengele cha kuendesha, kusimamia na kukuza bunifu mbalimbali zenye tija kwa nchi.

Natoa hoja
 
natamani siku moja Tanzania tuwe na satellite angani kwaajili ya ulinzi,utafiti,mawasiliano n,k lakini kwa jinsi vile mambo yalivyo kwenye nchi yangu ni ngumu zaidi ya ngumu hili jambo kutokea.
 
natamani siku moja Tanzania tuwe na satellite angani kwaajili ya ulinzi,utafiti,mawasiliano n,k lakini kwa jinsi vile mambo yalivyo kwenye nchi yangu ni ngumu zaidi ya ngumu hili jambo kutokea.
Serikali ipo bize kununua mitambo ya kuingilia mawasilianno ya raia wake.

Katiba mpya itatupatia serikali inayowajibika kwa nchi na siyo ujinga wa wanasiasa
 
Back
Top Bottom