Msiomkubali mwalimu Nyerere angalia hapa.

Msiomkubali mwalimu Nyerere angalia hapa.

ni ngumu sana kumkubali mtu mwingine kama wewe mwenyewe hujikubali

Ni nani almkataa Mzee Nyerere kuwaa ndiye alikuwa Rais wa kwanza? ni nani ambae anapingana na maneno ya Nyerere ambayo mwenyewe alisema kuwa ana makosa aliyofanya na tuyaache makosa yake tufanye mazuri yake. Sasa wewe onesha mazuri yake na mimi naonesha makosa yake. Kuna tatizo lipi hapo la kumkubali au kutokumbali? yupo?
 
Rais wa kwanza wa Tanzania Mzee Nyerere katuwekea historia ambayo tuliokuwepo wakati wake hatuisahau daima:

Tulikosa hata dawa za meno wakati wake, tukaletewa dawa za kichina ukipigia mswaki, haupati testi ya chumvi wala sukari.

Umeshawahi uziona hizi?

Maxam%20120g.jpg

Na leo tumejiletea nini? Wizi,uongo na ufisadi wa mali ya umma!
 
Ni msomi wa zamani na Rais wa kwanza wa Tanzania, hakuna anaepinga hilo, nawe usipinge kuwa yeye ndiye aliifanya hii nchi kuwa maskini wa mwisho duniani, alikuwa dikteta, na ndiye chanzo cha udini Tanzania kwa kulitumikia Kanisa Katoliki zaidi ya wananchi wake ambao wengi wao si wakatoliki na ndio sababu mpaka alipostaafu Mwitongo akihudumiwa na ma sista wa kanisani kama ma hausigeli wake na ndio katuzwa uwenye heri akingojea muujiza wa kumfanya mtakatifu.

UMELAANIWA! Hata Mh. JK unayejikombakomba kwake hawezi kukusifia na utamsikitisha sana.
 
Kipi bora,kumkosoa marehemu au kuyaendeleza yale mazuri Yatakayotusaidia?
 
Mkuu najua kinachokusukuma kumsema Mwalimu..ni imani yako wala si kingine....maana watu wa imani yako ndio wanaongoza kwa kumsonga Mwalimu...
Lkn wenye akili tunajua hizo ndizo tabia zenu za asilikabisa katka imani yenu kugeuza geuza mambo..tunaowajua hamtusumbui...naweza weza hata kukupa andiko kutoka katika imani yako inayosapoti tabia zenu hizi za kufundishana hata kupigana bila kufikiri!!
Any way ..Nyerere kitu gani bwana, watu wanampinga Yesu kristo walimpinga akiwa hai dai leo wana mpinga na kupotosha mafundisho yake!! Watu wanampinga Mtume Mohamed SAW... walimpinga alipokuwa hai hadi leo wanampinga....!
Lakini mwisho wa siku kweli itasimama na itauweka huru, nuru itashinda giza!!

Amen...
 
Kipi bora,kumkosoa marehemu au kuyaendeleza yale mazuri Yatakayotusaidia?

Kwa nini vyote visiwezekane pamoja?

Its not like there is an inherent mutual exclusivity.

Kwa nini tusitafute ukweli zaidi?
 
Hivi umemsikia Edwin Mtei anavyomuongelea Mwalimu? au unakumbuka mwalimu mwenyewe alivyosifia sera nzuri chama cha Mtei CDM! Unakremu ee?

Ungejua yaliyosababisha Mtei kutoka kwenye Cabinet ya Nyerere 1980 usingeandika ulichoandika.
 
Mwl. J.K.Nyerere ni muungwana kwa vitendo kwani hajakataa kuwa wakati wa uongozi wake hakufanya mambo mabaya. Alitushangaa baadhi yetu kuacha mambo mazuri yaliyofanywa na uongozi wa awamu ya kwanza na kuchukua mambo ya kijinga.
 
KINA LUMUMBA WETU: HUZUNI NA MAJONZI YA KUWAPOTEZA HANGA, SHARIFF, SADALLAH NA ABDULAZIZ K. TWALA.

"Karume hakuwapenda Wasomi, na hakuwa akiwaamini kabisa, hata ukiangalia wengi wa Viongozi wa ASP waliofungwa na Karume walikuwa ni wale Wasomi, Kama Othman Shariff.

Othman Shariff na Karume walikuwa ni Mahasimu ndani ya siasa za ndani za ASP hata kabla ya Uhuru wa Zanzibar, baada ya Mapinduzi Shariff aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu kisha mara tu baada ya Muungano na Tanganyika akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Marekani.

Inasemwa kuwa wakati flani Shariff aliporudi nyumbani Tanzania kwa mapumziko aliwahi kuonekana akipiga picha katika maeneo ya Ikulu, hilo tu la kuonekana akipiga picha Ikulu lilitosha kulifanya 'Baraza la Mapinduzi' kumtuhumu Balozi Shariff kuwa ni 'shushushu' wa CIA aliyekuwa akipeleleza kwa ajili ya Manufaa ya Serikali ya Marekani.

Mamlaka za Usalama zilimkamata kwa tuhuma za 'Ushushushu na Ukibaraka' lakini zilimuachia mara baada ya Rais Nyerere kuingilia hilo. Alishushwa Madaraka yake kutoka Balozi mpaka kuwa Afisa wa Mifugo katika Mkoa wa Iringa, Tanzania Bara.

Baadaye Usalama wa Taifa wa Zanzibar kwa amri Maalum ya Baraza la Mapinduzi ulitumwa kwenda kumkamata Balozi Othman Shariff Mussa huko Iringa na kumrejesha Zanzibar, Mwalimu Nyerere alijaribu tena kuingilia kwenye hilo baada ya kuombwa kufanya hivyo na Wazee wa Iringa.

Baadaye Nyerere alikubali kumkabidhi Shariff kwa Mamlaka za Usalama wa Taifa wa Zanzibar baada ya kushawishiwa na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, mara baada ya kufikishwa Zanzibar huo ndio ulikuwa mwisho wa Shariff.

Abdallah Kassim Hanga alikuwa Msomi kutoka Urusi na mtu Mashuhuri sana Miongoni mwa Wanachama Vijana wa Chama cha Afro-Shiraz (ASP). Mara baada ya Mapinduzi alitangazwa kuwa Makamo wa Rais wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar chini ya Karume kabla ya kuhamishiwa Jijini Dar es salaam kwenye Serikali ya Muungano mara baada ya Muungano.

Punde tu Hanga alimtumbukia nyongo Nyerere kwa sababu ya Ukaribu wake na Kambona, aliyekuwa Waziri wa Nyerere wa Mambo ya Nje na Ulinzi. Wakati wa Uasi wa Jeshi la Tanganyika (King's African Riffles) mwaka 1964, alikuwa ni Kambona aliyekwenda kuzungumza na Wanajeshi wale akijaribu kuwatuliza wakati Nyerere akiwa Mafichoni.

Mara baada ya Kambona kukosana na Nyerere na kwenda Uhamishoni, Hanga naye alitazamwa kwa Jicho baya kwa kuwa alikuwa karibu mno na Kambona. Punde aliondolewa kwenye Baraza la Mawaziri na akaamua kuhamia Conakry, Nchini Guinea kwa kuwa alikuwa ameoa Mwanamke wa Kiguinea.

Baada ya muda, Rais Nyerere alipeleka Ujumbe kwa Rais Ahmed Sekou Toure wa Guinea, ambaye ndiye aliyekuwa amempa hifadhi Hanga Nchini mwake, akimuomba akubali kumrudisha Hanga Nchini Tanzania na akimuahidi kuwa Hanga asingedhuriwa na angebaki salama.

Kwa bahati mbaya, Mara baada ya Hanga kurejea Tanzania alikamatwa na akadhalilishwa hadharani wananchi wote wakishuhudia. Katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Nyerere alimleta Hanga Uwanjani hapo akiwa na Pingu mikononi.

Katika Hotuba yake aliyoitoa viwanjani hapo, Rais Nyerere alimdhalilisha na kumsema vibaya Hanga na kama haitoshi akakubali kumrudisha Zanzibar ambako aliteswa na kisha kuuawa kinyume kabisa na ahadi aliyoitoa kwa Rais Sekou Toure".

Source:
http://kidojembe.blogspot.com/2013/01/unamfahamu-mwafrika-aliedhulumiwa-kwa.html

President Julius Nyerere is pictured on January 16th when he addressed an open air rally where the detained former Tanzania Minister and Vice-President of Zanzibar was brought to face the people. Mr. Kassim Hanga (seated between two police officers) is under detention with a number of other top Tanzanians after allegedly boasting that he had been called from voluntary exile in Guinea to lead an army coup on Zanzibar.

n33dxl.jpg

IMAGE:© Bettmann/CORBISDATE PHOTOGRAPHED January 16, 1968
LOCATION Dar-Es-Salaam, Tanzanian

Nukuu:
Hanga ni huyo alie chini ya ulinzi wa polisi wawili.


source: Mzalendo.net

Na hapa JF: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/63054-nyerere-alishiriki-mauaji-ya-kassim-hanga-9.html

Ndugu usihangaike na hawa WADANGANYIKA, washazoea kudanganywa kila siku, na wao wenyewe wanajiita wadanganyika bado tu unataka kuwaonesha ukweli? Waache wadanganyike, maana angekua kiongozi mahiri uchumi wetu wa nchi ungekuwa mzuri katika kipindi chake lakini shilingi ilishuka thamani wakati wake ama ndio ni process ya kuleta maendeleo? Na jinsi wadanganyika walivokuwa wapuuz.i wanataka legacy ya nyerere iendelee badala ya kiongozi kuapply idea na akili zake katika kuleta maendeleo ndio maana tupo hapa tulipo yote ni nyerere!
 
Shujaa kwako!mtu aliyetawala kwa miaka 25,akashindwa kvambua mahitaji MUHIMU ya raia wake,kwa kipindi chote hicho hakuweza KUJENGA JAPO CHUMBA KIMOJA TU CHA DARASA! HATA KM MOJA TU YA BARABARA YA TOPE ACHILIA MBALI LAMI.ALIYETAKA TULINGANE NA WANYAMA KWA KUTEMBEA UCHI.SINTA MSAHAU!
.
Mwalimu alishawahi kusema naomba ninukuu,"Upumbavu siyo tusi ni sifa kama tu kumwona mtu mwingine akiwa mrefu,mfupi,mnene na vinginevyo na vivyo hivyo kwa wengi tu ndani ya jf na mmojawapo si mwingine zaidi yako.huwezi toa maelezo finyu kama hayo ukafikri unaelewa sana ,no ur totally wrong, nani asiyejua ubora wa elimu na mazingira ya kusoma enzi za mwalimu, madaftari bure, madawati ya kumwaga na walimu wakutosha, labda kama unataka tu kujifurahisha na wapumbavu kama tu watakuunga mkono.Hebu angalia nyumba nyingi za waswahili wa magomeni zote zilijengwa chini ya mpango wa mwalimu na wazee wanajua walivyoweza kumiliki nyumba bora zilizo pimwa na mitaa ikiwekewa lami hata pasipokuwa na uwezo wa kujenga.Jamani someni vitabu mjue historia ya nchi hii siyo kufuata mihadhari ya walafi wa pilau na ubwabwa.
 
zomba, tuache kucheza na wakati...tutaishia kuwa wahanga wa mashimo tunayochimba wenyewe. Unless sisi tuko safi kabisa, unafiki na longo longo zina muda tena mfupi sana kabla mambo hayajabadilika kwa milele yote. Adhaniyaye amesimama aangalie asianguke!
 
Last edited by a moderator:
Mwl Nyerere ni miongoni mwa watanzania waliowahi kuwa wazalendo wa kweli! Mengi ya aliyokuwa akifanya alikuwa akifanya kwa manufaa ya taifa. Alikuwa na akili na vission. Kuna misingi mingi katika nchi hii ambayo ameiweka na leo hii tunagundua baada ya kuanza kuiharibu. Kwa sehemu kubwa ya hayo mabaya aliyoyafanya, ukiangalia vizuri utakuta alikuwa na dhamira nzuri kwa ajili ya taifa, ila tu ikatokea labda sio njia sahihi. Hakuna binadamu anayeweza kuiona future 100% ila ni kwa kukisia. Aliweka plan nyingi ambazo alitarajia zilisaidie taifa hili, lakini zingine kwa bahati mbaya zikashindikana kutekelezeka. Siamini kama kuna kitu alibuni kwa ajili ya kumfurahisha yeye au mtu mwingine binafsi, bali aliweka taifa mbele. Anayejua maisha aliyokuwa akiishi nyumbani kwake Msasani na Butiama naamini atakubali.
 
Ni msomi wa zamani na Rais wa kwanza wa Tanzania, hakuna anaepinga hilo, nawe usipinge kuwa yeye ndiye aliifanya hii nchi kuwa maskini wa mwisho duniani, alikuwa dikteta, na ndiye chanzo cha udini Tanzania kwa kulitumikia Kanisa Katoliki zaidi ya wananchi wake ambao wengi wao si wakatoliki na ndio sababu mpaka alipostaafu Mwitongo akihudumiwa na ma sista wa kanisani kama ma hausigeli wake na ndio katuzwa uwenye heri akingojea muujiza wa kumfanya mtakatifu.

zomba hizo story zimechosha njoo na kitu kingine kipya maana kila ukija hapa ni story za ukatoliki na Mwalimu Nyerere
Njoo na nyingine mpya na utuonyeshe udikteta wake sio kusema tuu na kuishia maana hata hazina tija maana kama unataka huduma ya masista hata wewe unaweza kuipata haijalishi ni mkatolic au mlutheri
Na hatuoni ni wapi Nyerere alihudumia wakatoliki zaidi ya wananchi wengine hebu toa ushahidi wako mkuu maana kama ni elimu hata wewe uliipata na kama ni huduma za afya au mawasiliano hata wewe ulipata hata kama hukuwa mkatoliki
 
Last edited by a moderator:
Ni msomi wa zamani na Rais wa kwanza wa Tanzania, hakuna anaepinga hilo, nawe usipinge kuwa yeye ndiye aliifanya hii nchi kuwa maskini wa mwisho duniani, alikuwa dikteta, na ndiye chanzo cha udini Tanzania kwa kulitumikia Kanisa Katoliki zaidi ya wananchi wake ambao wengi wao si wakatoliki na ndio sababu mpaka alipostaafu Mwitongo akihudumiwa na ma sista wa kanisani kama ma hausigeli wake na ndio katuzwa uwenye heri akingojea muujiza wa kumfanya mtakatifu.

aina ya watu kama wewe huwa pia wanashida ya kufikiri na kuchanganua mambo kwa kina.
 
hakuna mtu dunia ambaye ni mkamilifu, binadamu lazima awe na pande mbili. hao wanaomkataa walinganishe na viongozi waliomrithi. hao wanaouma na kupuliza.
 
Jela, mahakama, sheria nakubaliana nazo kwa kila mkosa, lakini hili la kuanikwa na kusutwa mtu ni sheria ya wapi? bila kufikishwa mahakamani? tulikuwa vitani? ilhali nchi yetu imekabidhiwa madaraka bila kumwaga damu zaidi ya mbuzi ya damu aliyofanyiwa makafara Nyerere na wazee wa bagamoyo.

Kwa hayo tutamkumbuka sana Rais wetu wa kwanza Mzee Nyerere.

Wewe unachuki binafsi na Nyerere, lakini nilkusahauri jambo.Usipoteze nguvu sana kupingana au kudhihaki heshima ya mtu kwa kusikiza propaganda za mitaani. Bob Marley alipata kusema "Who Jah (GOD) bless no man can curse". Nyerere alifanya kazi yake ya urais kwa uaminifu wa hali ya juu, kuna alipokosea kama binadamu wengine lakini katika hali ya kujaribu kufanya vema, tofauti na watu wanao kaa kikao cha kuuza rasilimali zetu kwa maslahi yao binafsi.
Tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom