Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Mwanzisha mada umekurupuka kwani hata katiba haimruhusu zito kugombea urais kutokana na umri wake, iweje ukurupuke na kudai atapata kura yeye kama yeye na siyo cdm wakati qualification zake hazimruhusu?
 
Sisi tunatanguliza nchi yetu mbele sio mtu au chama mana vyote hivyo vinapita...cdm sio Zitto ni Taasisi ipo na itakuepo bila Zitto wala wengine wengi...kwani hata sasaiv kazi inafanyika huko kusini Zitto yupo huko?!! wewe vipi bana tafta chakula ule..njaa itakuua...
 
Kigoma nimeweka mfano hai tu, kuwa kura zilikuwa za Zitto na si za CHADEMA kwani kwenye kura za Urais chadema waliambulia kidogo sana kuliko alizopata Zitto kwenye jimbo lake.

Mimi si wa Kigoma lakini Zitto namkubali na kuna wengi nnao-wafahamu wanamkubali Zitto.

Na Kikwete aliisha hint, anatamani Rais ajae awe "kijana". Nani zaidi ya Zitto kwa sasa, katika vijana kutokea chama chochote kile?

Kikwete atabaki anatamani tu hawezi kutuchagulia Rais. Tunahitaji rais mwenye vision na demonstrated committment ya kuifanya Tanzania kucompete na nchi kama South Africa, Botswana, n.k na sio umri wa mtu.

Mifano halisi tunayo, serikali ya CCM ina vijana kwa wazee lakini hakuna mwenye uzalendo wala committment ya kututoa kwenye umasikini huu wa kutisha.
 
HUYU JAMAA ANAHOJA ZA KIPUMBA FU KWELI. Kama hawakipigii kura za uraisi CHADEMA Bali wanampigia Zito amshauri Zito agombee kupitia ata CCM AU NCCR.

Nafuu tuweke Mbwa CHADEMA KULIKO MROHO WA MADARAKA ZITTO
 
Huwezi ku conclude kuwa zito anakubalika nchi nzima kwa reference ya uchaguzi wa kigoma! Ulishaweka mlinganyo wa slaa na zito jinsi wanavyokubalika countrywide? Zito ni jembe la ukweli chadema lakini chadema sio zito! Chadema ni wananchi! Ni wangapi wamehama vyama vyao kuja chadema kwa sababu ya zitto? Mapenzi yako kwa zito yasiwe conclusion ya hisia na mitazamo ya watu! Nenda kwa takwimu!
 
Haya mambo hayo, vitisho vya kitoto na mbio za uraisi 2015. Mbona hujasema CHADEMA wataumiaje?
 
Simba wanasirikiana katika mawindo,wanafanya coordination katika mawindo. Inakuwaje Chadema wagombane when the enemy is strong?
 
Aheri umemwambia kwa kumuelimisha, sisi tunamtazama tu anavyoweweseka hapa jf kutwa kucha! Kila thread hapa jf lazima Zomba aichangie kinyume, na kila siku lazima aanzishe thread zaid ya 20 na kuzisimamia ipasavyo hata kwa ujinga tu basi atabishana kutwa kucha!

Mkuu zomba ndio zitto kabwe mwenyewe, fuatilia utajua
 
though i am neither a member nor a fan of chadema but i am suddenly a fan of zitto kabwe, if he runs for president and i am still alive, count my vote for him, if he continues the way he is now.


so do i !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
.. wewe na nani mnamtaka Zitto? Au ndo yale yale ya "wakeup sleeping giant!" Cheap!
 
Wewe ni zitto nini!!! Nadhani unajihami mapema baada ya kugundua kuwa jitihada zako za kuutafuta urais zinaweza kugonga mwamba mbele ya wapiganaji wengine ndani ya cdm. Kama wewe ndiwe kabwe basi usijidanganye na ndoto zako za kuwa RAIS wa nchi labda kama ni kuwa RAHISI. Inawezekana huto tusafari twako twa kukutana na viongozi maarufu duniani ni mbinu mojawapo utakayoitumia wakati wa kuchukua fomu lakini mbele ya cdm hilo si lolote si chochote. Utaangukia pua tu.

Hapana, mimi si Zitto, mimi ni mnazi wa Zitto ingawa mimi si magwanda ya kijivu, mimi ni gwanda orijino la kijani.
 
Lowassa ni mwamba wa kaskazini hamuwezi nyinyi mlikuwa mnafikiri ni wa bagamoyo sio atawalipua

Huyo wa Bwagamoyo ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Lowassa ameshawahi kuwa Waziri Mkuu wake, au umesahau? wale ni chanda na pete hawakujuana "barabarani".
 
Zombi=zomba upo wapi? Naona huko ccm mnamtamani sana zito kiongozi wetu shupavu CDM. Viongozi wenu ni lowassa mwamba kaskazini jaribuni kumgusa muone moto Pambaf

Sasa ndugu yangu, kama unaona id yangu ni Zomba wewe kunipachika Zombi, huoni kuwa huo ni uchokozi wa wazi wazi? Kama mjadala wa kiungwana unakushida, nakushauri kunywa maji kidogo, upumuwe kisha urudi tena. Tusianze kuitana majina "name calling" ni kinyume na kanuni za JF. Natumai moderators wanakusoma na watakufahamisha zaidi.

Naomba tuongee mada husika tusianze kushambuliana binafsi. Si vyema, au unasemaje kijana?
 
Zombi=zomba umeingia mitini lowassa Mzee wa makanisa Hana mpinzani ndani ya ccm lazima wote mfyate Mkia mpaka Rais wenu

Ni Zomba na si Zombi kama unavyonikejeli. Naomba tuendelee na mjadala wa kuheshimiana. Sijaingia mitini, nipo, kunywa maji halafu urudi, utapunguza Munkar na kejeli zisizo na tija kwako wala kwangu.
 
Kuna kila njama zinazofanywa kwa makusudi kabisa, kupunguzia kasi Zitto Kabwe katika jukwaa la kisiasa. Njama hizo zinatokea kwa vigogo fulani wa CHADEMA, wanaomuona kuwa Zitto ni mwiba mkali.

Historia ya karibuni ilionesha kuwa Zitto alisakamwa sana alipotaka kugombea uenyekiti na baada ya kuzipangua hoja zote za kumuumiza kisiasa ndani ya CHADEMA akaambulia kupoozwa kwa kusukumiwa cheo cha unaibu Katibu Mkuu, cheo ambacho hakina manufaa yoyote kwa CHADEMA wala kwa Zitto. Ili kuponesha maumivu na kutibu majeraha ya kisiasa, Zitto akakikubali cheo hicho, lakini ukweli ni kwamba hakifanyii kazi yoyote.

Uthibitisho mwingine wa kumshusha kisiasa Zitto ni pale ambapo hajahudhuria vikao vya CHADEMA na Kikwete huko Ikulu, kuna mambo ya msingi ambayo Zitto amekuwa akitofautiana na viongozi wengine wa CHADEMA na hayo ndio yanamfanya ajaribiwe kushushwa hadi na kutokuwekwa kwenye maamuzi mengi ya chama na yeye hustukia tu maamuzi yameshafanywa. Na anapotoa misimamo yake huwa ina tofauti na ya chama chake, mifano ipo mingi.

Tunawaasa vigogo wa CHADEMA kuwa hata ndugu zetu wa Kigoma walipopiga kura za Ubunge zilikuwa ni kura za Zitto na si za CHADEMA, hilo walielewe. Kama ilivyo kwa kura za Shibuda, zilikuwa ni za Shibuda lakini si za CHADEMA hilo linajidhihiri kwa kuwa kura za Urais za Kigoma 90% zilikuwa za Kikwete hata kwenye jimbo la Zitto.

Aliposhindwa Mbowe uchaguzi mkuu wa 2005, 2010 akawekwa Slaa, tunataka Zitto agombee 2015 tumpe kura zetu, kumbuka, hatuwapi kura CHADEMA tutampa Zitto Kabwe, bila yeye sahauni kura za wengi.

Kati ya vitu asivyopendezwa navyo Zitto ni namna ya chaguzi za wabunge wa upendeleo zinavyoendeshwa kimabavu ndani ya CHADEMA.

Tunawatahadharisha CHADEMA wasimjaribu Zitto, wataumia kisiasa.

Hapo kwenye red, wewe na nani? Sasa naona umetumwa, kuna chama kipya kimeanzishwa kinaitwa ADC mshauri zito aende huko mkampee kura zenu. Ama kama hilo litakuwa gumu mshauri asimame kama mgombea binafsi kama katiba itakuwa imepitishwa. Huku CDM asahau kusimama kama mgombea wa urais, hatutakubali hilo litokee, tunahitaji kamanda mpambanaji zaidi bishoo. Pamoja na mtu sisi tunachagua Chadema. Zitto ni mbinafsi na mpenda sifa, ni mroho wa madaraka. Baba wa taifa alitushauri kuwa ukiona mtu anakimbilia Ikilu huyo ni wa kuogopwa kama ukoma. Angekuwa na busara walau kidogo angeacha watu wampeleke kuliko yeye kukimbilia. Angengojea kama Dr Slaa mwaka 2010, sio kujikimbiza kimbiza.

Hapana Zitto anafaa kuendelea kuwa mbunge tu labda huko baadaye akikuwa. Mara natakuwa mwenyekiti wa chama, mara nataka kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, mara nataka kuwa rais; who are you? kusema hivyo si kwamba napuuzia mchango wake katika siasa za mageuzi nchini mwetu, lakini ana kiherehere mno.

Ushauri wa bure.
 
Back
Top Bottom