Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Mkuu Kilembwe, kumbe humjui Zoba! hapa anataka kuwagombanisha wana CHADEMA kwa fitina zake za udini. Hapo anataka kutumia uislam wa mh. Zito kwa manufaa yake. Zoba ni mtu wa kuogopwa sana. Tangu lini gamba kama yeye akajifanya msemaji wa mh.Zito?

Nakupa pole sana, au hujamsikia Zitto akisema atagombea Urais 2015? au mnae mliokwisha amua tayari?
 
Kuna kila njama zinazofanywa kwa makusudi kabisa, kupunguzia kasi Zitto Kabwe katika jukwaa la kisiasa. Njama hizo zinatokea kwa vigogo fulani wa CHADEMA, wanaomuona kuwa Zitto ni mwiba mkali.

Historia ya karibuni ilionesha kuwa Zitto alisakamwa sana alipotaka kugombea uenyekiti na baada ya kuzipangua hoja zote za kumuumiza kisiasa ndani ya CHADEMA akaambulia kupoozwa kwa kusukumiwa cheo cha unaibu Katibu Mkuu, cheo ambacho hakina manufaa yoyote kwa CHADEMA wala kwa Zitto. Ili kuponesha maumivu na kutibu majeraha ya kisiasa, Zitto akakikubali cheo hicho, lakini ukweli ni kwamba hakifanyii kazi yoyote.

Uthibitisho mwingine wa kumshusha kisiasa Zitto ni pale ambapo hajahudhuria vikao vya CHADEMA na Kikwete huko Ikulu, kuna mambo ya msingi ambayo Zitto amekuwa akitofautiana na viongozi wengine wa CHADEMA na hayo ndio yanamfanya ajaribiwe kushushwa hadi na kutokuwekwa kwenye maamuzi mengi ya chama na yeye hustukia tu maamuzi yameshafanywa. Na anapotoa misimamo yake huwa ina tofauti na ya chama chake, mifano ipo mingi.

Tunawaasa vigogo wa CHADEMA kuwa hata ndugu zetu wa Kigoma walipopiga kura za Ubunge zilikuwa ni kura za Zitto na si za CHADEMA, hilo walielewe. Kama ilivyo kwa kura za Shibuda, zilikuwa ni za Shibuda lakini si za CHADEMA hilo linajidhihiri kwa kuwa kura za Urais za Kigoma 90% zilikuwa za Kikwete hata kwenye jimbo la Zitto.

Aliposhindwa Mbowe uchaguzi mkuu wa 2005, 2010 akawekwa Slaa, tunataka Zitto agombee 2015 tumpe kura zetu, kumbuka, hatuwapi kura CHADEMA tutampa Zitto Kabwe, bila yeye sahauni kura za wengi.

Kati ya vitu asivyopendezwa navyo Zitto ni namna ya chaguzi za wabunge wa upendeleo zinavyoendeshwa kimabavu ndani ya CHADEMA.

Tunawatahadharisha CHADEMA wasimjaribu Zitto, wataumia kisiasa.

Umbea mtupu!
 
Fuata yako ndugu

Asiyefata siasa huyo labda haishi dunia hii, kwani siasa ndio zinaamua bei ya mkate wa kila siku.

Haya ni yangu na yananihusu kila upande, hujui kuwa Zitto ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? ndio watungaji wa sheria zetu na kwa uwezo wake aliouonesha naona anafaaa kabisa awe Rais Jamhuri ya Muungano Watanzania.
 
CHADEMA bila Zitto Kabwe inawezekana. kwani Zitto nini CDM, hivi ni wangapi ktk CDM ni bora kuliko Zitto hata ujumbe hawana, Na Zitto ni binadamu CDM ni Taasisi itakayokuwepo hata bila Mh.Mbowe,Dr Slaa, John Mnyika, Heche Na wengine. Ni kwavipi mnataka tuamini watu badala ya Sera na Uwezo wa kutafsiri na kufanyia kazi kwa vitendo. Zitto Anamapungufu Mengi may be kuliko hao unaowaita wanamshusha na Angelikuwa anafikiri vizuri Zitto angekemea tabia za washabiki wake kushabikia tabia za ki ccm za kuwepo makundi ktk chama, amekua akifurahia ujinga huu bila hata kuukemea na anajua ulivo na athali ktk chama. Mi naamini Zitto amekosa busara ya kawaida ya kuweka ligi hata mambo yasiyo na tija ktk CDM. Mi Naamini AKIKUA ATAACHA na ndo utakua muda muafaka kwa yeye kuaminiwa na kupewa Madaraka yenye maamuzi ktk CDM na Nchi kwa ujumla. But kwa sasa Zitto ni Nothing ktk CDM HAAMINIKI na yeye mwenyewe HAPENDI AAMINIKE KWA MATENDO YAKE ya kukubali kutumika hata na MAFISADI kama kushabikia kununua Magenereta USED ya DOWNS
 
Nimeshangaa sana kwamba hadi thread imefika page ya tano Waberoya bado hajacoment, tena kwa thread kama hii! Anyway labda atakuwa amelala. Tusubiri azinduke tuone!

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Duh..nimeamini CDM wapo makini...hizi kelele zinaonyesha CDM lazima chaguzi zao viwe na mchujo mkali.Na kila anayepewa jukumu lazima aaminike sana.Otherwise hizi kelele ziaonyesha failure za hawa wacheza kamikaze.

Mtei anajua business...kuwa Chama kinapooanza ni km business ukiachia nyani utavuna mabua.Ila biashara ikukuwa na kukomaa kimtaji then public offering ya share inaweza kuwa salama.

Cha kushangaza hawa wapuuzi kwanini wanaota kuuwa CDM kwa faida ya CCM iliyokufa?Huyu Zitto haoni kuwa Huo urais ungekuwa wazi na mtamu km angefunga mdomo kwa 100yrs.
 
Zomba

Nimepitia taratibu Na Kwa makini bandiko lako.. Na Kwa bidii nikawa napitia kila hoja ya raia unavyoijibu.. Na baadae nikavutiwa kujua Kama wewe ni mwanachama Wa CDM, baadae ukanisaidia sana kwamba sio CDM.

ungekuwa mwanachama wa CDM, Basi nadhani rasmi Chama kingekuwa kimevamiwa Na kirusi cha Kutisha mno.

Na hili ndilo tatizo la CCM Chama chetu hiki. Kwa miaka mingi kimejitahidi kupindua ila sasa kinajipindua chenyewe.. Sijui ni Laana gani hii. Ona Zomba, umejenga Hoja yako, sasa ulivyoanza kujibizana mabandiko ya raia, ukajisahau , akili yako ikawa haina akili tena, ukajikanyagakanyaga Na kujibizana Kwa lugha za kimwambao Na zenye tafsiri ngumu.

Kuna tatizo kubwa sana Ccm, kuna utitiri wa wabunge, madiwani, ma DC, mawaziri Na hata Rais.. Ila wote wemelazwa.. Kila mmoja Yuko bize na mishemishe za kivyake.. wamemwachia Nape ambaye maskini ya Mungu Hajui nini aseme wapi, Mara atoe amri as if ni waziri, Mara atoe maelekezo Kama Rais vile ,, ila anazunguka tu peke yake Ccm imelazwa fofofo.. Kazi kupiga majungu tu Na propaganda za kipumbavu ambazo zinakididimiza Chama ..

Pambaneni uwanjani.. Hoja Kwa Hoja .. Mambo ya ZITO yanakuhusu nini Kama si mwachama Wa Chama alichoko Leo ..
 
Zomba

Nimepitia taratibu Na Kwa makini bandiko lako.. Na Kwa bidii nikawa napitia kila hoja ya raia unavyoijibu.. Na baadae nikavutiwa kujua huyu ni Kama wewe ni mwanachama Wa CDM, baadae ukanisaidia sana kufundua kwamba sio CDM.

ungekuwa mwana CDM, Basi nadhani rasmi Chama kingekuwa kimevamiwa Na kirusi cha Kutisha mno.

Na hili ndilo tatizo la CCM Chama chetu hiki. Kwa miaka mingi kimejitahidi kupindua ila sasa kinajipindua chenyewe.. Sijui ni Laana gani hii. Ona Zomba, umejenga Hoja ya yako, sasa ulivyoanza kujibizana mabandiko ya raia, ukajisahau , akili yako ikawa haina akili tena, ukajikanyagakanyaga Na kujibizana Kwa lugha za kimwambao Na zenye tafsiri ngumu.

Kuna tatizo kubwa sana Ccm, kuna utitiri wa wabunge, madiwani, ma DC, mawaziri Na hata Rais.. Ila wote wemelazwa.. Kila mmtu Yuko bize kivyake.. wamemwachia Nape ambaye maskini ya Mungu Hajui nini aseme wapi, Mara atoe amri as if ni waziri, Mara atoe maelekezo Kama Rais vile ,, ila anazunguka tu peke yake Ccm imelazwa fofofo.. Kazi kupiga majungu tu Na propaganda za kipumbavu ambazo zinakididimiza Chama ..

Pambaneni uwanjani.. Hoja Kwa Hoja .. Mambo ya CDM yanakuhusu nini..
Aheri umemwambia kwa kumuelimisha, sisi tunamtazama tu anavyoweweseka hapa jf kutwa kucha! Kila thread hapa jf lazima Zomba aichangie kinyume, na kila siku lazima aanzishe thread zaid ya 20 na kuzisimamia ipasavyo hata kwa ujinga tu basi atabishana kutwa kucha!
 
Kuna kila njama zinazofanywa kwa makusudi kabisa, kupunguzia kasi Zitto Kabwe katika jukwaa la kisiasa. Njama hizo zinatokea kwa vigogo fulani wa CHADEMA, wanaomuona kuwa Zitto ni mwiba mkali.

Historia ya karibuni ilionesha kuwa Zitto alisakamwa sana alipotaka kugombea uenyekiti na baada ya kuzipangua hoja zote za kumuumiza kisiasa ndani ya CHADEMA akaambulia kupoozwa kwa kusukumiwa cheo cha unaibu Katibu Mkuu, cheo ambacho hakina manufaa yoyote kwa CHADEMA wala kwa Zitto. Ili kuponesha maumivu na kutibu majeraha ya kisiasa, Zitto akakikubali cheo hicho, lakini ukweli ni kwamba hakifanyii kazi yoyote.

Uthibitisho mwingine wa kumshusha kisiasa Zitto ni pale ambapo hajahudhuria vikao vya CHADEMA na Kikwete huko Ikulu, kuna mambo ya msingi ambayo Zitto amekuwa akitofautiana na viongozi wengine wa CHADEMA na hayo ndio yanamfanya ajaribiwe kushushwa hadi na kutokuwekwa kwenye maamuzi mengi ya chama na yeye hustukia tu maamuzi yameshafanywa. Na anapotoa misimamo yake huwa ina tofauti na ya chama chake, mifano ipo mingi.

Tunawaasa vigogo wa CHADEMA kuwa hata ndugu zetu wa Kigoma walipopiga kura za Ubunge zilikuwa ni kura za Zitto na si za CHADEMA, hilo walielewe. Kama ilivyo kwa kura za Shibuda, zilikuwa ni za Shibuda lakini si za CHADEMA hilo linajidhihiri kwa kuwa kura za Urais za Kigoma 90% zilikuwa za Kikwete hata kwenye jimbo la Zitto.

Aliposhindwa Mbowe uchaguzi mkuu wa 2005, 2010 akawekwa Slaa, tunataka Zitto agombee 2015 tumpe kura zetu, kumbuka, hatuwapi kura CHADEMA tutampa Zitto Kabwe, bila yeye sahauni kura za wengi.

Kati ya vitu asivyopendezwa navyo Zitto ni namna ya chaguzi za wabunge wa upendeleo zinavyoendeshwa kimabavu ndani ya CHADEMA.

Tunawatahadharisha CHADEMA wasimjaribu Zitto, wataumia kisiasa.
Aaaah Zomba mwana CCM hata wewe umeingia ktk kukatiwa pochi mkuu wangu? vibaya hivyo. Zitto wetu sisi na tunampenda sisi haya mtayasema sana mwaka huu na 2015 inapiga hodi tik tak tik tak..Zitto yupo sana Chadema na anafurahia sana mnapogongana kwa ashiki zenu wenyewe hamuishi kumtaja taja. CCM hatokuja na wala msitegemee kutuvuruga maana ndio nia yenu watu wafikirie kwamba hii ni kambi ya Zitto..maanake tunawajua mlofanya kwa ghiriba zenu kwa yule Kabourou - leo chanuu!. Mtawachukua tu kina Maalim Sief, Mbatia wenye mukhu wa kuitwa waheshimiwa lakini sii hapo mkuu wangu.
Tuacheni tuijenge nchi.
 
Zomba

Nimepitia taratibu Na Kwa makini bandiko lako.. Na Kwa bidii nikawa napitia kila hoja ya raia unavyoijibu.. Na baadae nikavutiwa kujua Kama wewe ni mwanachama Wa CDM, baadae ukanisaidia sana kwamba sio CDM.

ungekuwa mwanachama wa CDM, Basi nadhani rasmi Chama kingekuwa kimevamiwa Na kirusi cha Kutisha mno.

Na hili ndilo tatizo la CCM Chama chetu hiki. Kwa miaka mingi kimejitahidi kupindua ila sasa kinajipindua chenyewe.. Sijui ni Laana gani hii. Ona Zomba, umejenga Hoja yako, sasa ulivyoanza kujibizana mabandiko ya raia, ukajisahau , akili yako ikawa haina akili tena, ukajikanyagakanyaga Na kujibizana Kwa lugha za kimwambao Na zenye tafsiri ngumu.

Kuna tatizo kubwa sana Ccm, kuna utitiri wa wabunge, madiwani, ma DC, mawaziri Na hata Rais.. Ila wote wemelazwa.. Kila mmoja Yuko bize na mishemishe za kivyake.. wamemwachia Nape ambaye maskini ya Mungu Hajui nini aseme wapi, Mara atoe amri as if ni waziri, Mara atoe maelekezo Kama Rais vile ,, ila anazunguka tu peke yake Ccm imelazwa fofofo.. Kazi kupiga majungu tu Na propaganda za kipumbavu ambazo zinakididimiza Chama ..

Pambaneni uwanjani.. Hoja Kwa Hoja .. Mambo ya ZITO yanakuhusu nini Kama si mwachama Wa Chama alichoko Leo ..

Naona bado unashindwa kuelewa hoja ya kuwa huko tunakoelekea hakuna Rais ataeshinda kwa kura za chama chake tu na pengine itafikia hivyo hata kwa wabunge.

Tazama nchi zilizoendelea kidemokrasia, kila mtu anapigania apate kura za wapinzani ili apate ushindi, na Tanzania niionavyo, huko ndiko inakoelekea.

Kumbuka kuwa haya majukwaa ya mtandaoni ya kijamii yanabadili vijiwe na barza za mitaani, kwa hiyo tukiwa humu, tupo wengi na kila mmoja ana namna yake ya kuongea na inabidi tujibizane kama ilivyo, mradi tu tusitukanane.
 
Aheri umemwambia kwa kumuelimisha, sisi tunamtazama tu anavyoweweseka hapa jf kutwa kucha! Kila thread hapa jf lazima Zomba aichangie kinyume, na kila siku lazima aanzishe thread zaid ya 20 na kuzisimamia ipasavyo hata kwa ujinga tu basi atabishana kutwa kucha!

Na wewe si tupo pamoja ndio maana ukaziona zote hizo. Au? Humu tutabanana sote, labda mtuambie CCM marufuku, mdanganyane wenyewe kwa wenyewe.
 
Aaaah Zomba mwana CCM hata wewe umeingia ktk kukatiwa pochi mkuu wangu? vibaya hivyo. Zitto wetu sisi na tunampenda sisi haya mtayasema sana mwaka huu na 2015 inapiga hodi tik tak tik tak..Zitto yupo sana Chadema na anafurahia sana mnapogongana kwa ashiki zenu wenyewe hamuishi kumtaja taja. CCM hatokuja na wala msitegemee kutuvuruga maana ndio nia yenu watu wafikirie kwamba hii ni kambi ya Zitto..maanake tunawajua mlofanya kwa ghiriba zenu kwa yule Kabourou - leo chanuu!. Mtawachukua tu kina Maalim Sief, Mbatia wenye mukhu wa kuitwa waheshimiwa lakini sii hapo mkuu wangu.
Tuacheni tuijenge nchi.

Hapana sijakatiwa pochi na mtu wala sitegemei kama kuna siku itakuwa hivyo.

Zitto ni kijana ambae hakuna ataepinga kuwa ameipaisha sana chadema, lakini kwa masikitiko makubwa naona chadema wanamtenga, sijui kwanini.

Namfatilia sana siasa zake, ingawa na yeye ni kama binaadam mwengine yeyote kwani sote sisi hakuna aliyekamilika, juu ya mapungufu yake lakini ni kijana anaejituma, mchapa kazi na anakwenda na wakati kisiasa. hayumbishwi hovyo na huwa ana misimamo katika hoja zake. Namsikitikia sana kuwepo CHADEMA kwani mwisho wa siku watampiga teke kama vile hajawafanyia kitu. Nyota njema huonekana Alafajiri.

Zitto hata akiwa chadema na akigombea basi kura yangu anayo.
 
Ulitaka awe CUF na NCCR?
 
Ulitaka awe CUF na NCCR?

Kuwa chama chochote hakumuondelei mtu umahiri wake wa kazi. Isipokuwa wale ambao hawakufanya lolote la maana kutoka katika vyama walivyokuwepo zamani, mfano Slaa alitemwa CCM katika kura za maoni kwa kuwa walishamuona kuwa hafai uongozi, wakati huohuo chadema licha ya kumpa shutuma nyingi sana Zitto wameshindwa kumpiga chini kwa kuwa ni kijana hodari na amezisoma mbinu na anapambana nazo akiwa humohumo ndani. Slaa yalimshinda hayo ya kupambana akiwa ndani ya CCM, inaonesha kabisa ni mtu aliyekuwa ana uchu wa madaraka na si uongozi.
 
Back
Top Bottom