Msimjaribu Zitto, mtaumia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zomba, Jun 4, 2012.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna kila njama zinazofanywa kwa makusudi kabisa, kupunguzia kasi Zitto Kabwe katika jukwaa la kisiasa. Njama hizo zinatokea kwa vigogo fulani wa CHADEMA, wanaomuona kuwa Zitto ni mwiba mkali.

  Historia ya karibuni ilionesha kuwa Zitto alisakamwa sana alipotaka kugombea uenyekiti na baada ya kuzipangua hoja zote za kumuumiza kisiasa ndani ya CHADEMA akaambulia kupoozwa kwa kusukumiwa cheo cha unaibu Katibu Mkuu, cheo ambacho hakina manufaa yoyote kwa CHADEMA wala kwa Zitto. Ili kuponesha maumivu na kutibu majeraha ya kisiasa, Zitto akakikubali cheo hicho, lakini ukweli ni kwamba hakifanyii kazi yoyote.

  Uthibitisho mwingine wa kumshusha kisiasa Zitto ni pale ambapo hajahudhuria vikao vya CHADEMA na Kikwete huko Ikulu, kuna mambo ya msingi ambayo Zitto amekuwa akitofautiana na viongozi wengine wa CHADEMA na hayo ndio yanamfanya ajaribiwe kushushwa hadi na kutokuwekwa kwenye maamuzi mengi ya chama na yeye hustukia tu maamuzi yameshafanywa. Na anapotoa misimamo yake huwa ina tofauti na ya chama chake, mifano ipo mingi.

  Tunawaasa vigogo wa CHADEMA kuwa hata ndugu zetu wa Kigoma walipopiga kura za Ubunge zilikuwa ni kura za Zitto na si za CHADEMA, hilo walielewe. Kama ilivyo kwa kura za Shibuda, zilikuwa ni za Shibuda lakini si za CHADEMA hilo linajidhihiri kwa kuwa kura za Urais za Kigoma 90% zilikuwa za Kikwete hata kwenye jimbo la Zitto.

  Aliposhindwa Mbowe uchaguzi mkuu wa 2005, 2010 akawekwa Slaa, tunataka Zitto agombee 2015 tumpe kura zetu, kumbuka, hatuwapi kura CHADEMA tutampa Zitto Kabwe, bila yeye sahauni kura za wengi.

  Kati ya vitu asivyopendezwa navyo Zitto ni namna ya chaguzi za wabunge wa upendeleo zinavyoendeshwa kimabavu ndani ya CHADEMA.

  Tunawatahadharisha CHADEMA wasimjaribu Zitto, wataumia kisiasa.
   
 2. L

  Laurano Senior Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu hujitengenezea historia mwenyewe
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mods naomba mrekebishe kichwa cha habari ni typo tu, kisomeke "Msimjaribu Zitto, mtaumia".
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wewe ni msemaji wa Zitto Kabwe? mbona mwenywe hajasema haya!
   
 5. k

  kipuyo JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 1,149
  Likes Received: 522
  Trophy Points: 280
  Wana wa Uamsho kazini.Itakuwaje ikiwa ccm watamsimamisha Bassaleh na chadema wakamsimamisha Zitto,je utamchagua nani?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na ndivyo ilivyo kwa Zitto.
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Source Pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz tutaaminije maneno yako? Weka Picha tuone ha ha haaaaaaaaaaa Magamba yanaruka na kukanyagana
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani yote yanayosemwa humu wanayasema wenyewe? Haya ni yangu mimi, si ya mwengine. Nna kila sababu za kuchambuwa wana siasa kadri ya uwezo wangu.
   
 9. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  zomba,
  Did you count me in your generalized statement? Mine is "NO" guaranteed if Zitto stands for Presidential Candidate under CDM.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Source ni mimi mwenyewe.
   
 11. S

  SUWI JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  \

  Kumbe tatizo lako kwa CDM ni wachaga!!!
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Picha Pliiiiiz
   
 13. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Magamba hamchoki kutaka kuleta chokochoko CDM? Mbona hamfanikiwi lakini???
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Weka Picha
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Though I am neither a member nor a fan of CHADEMA but I am suddenly a fan of Zitto Kabwe, if he runs for president and I am still alive, count my vote for him, if he continues the way he is now.
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika vazi la asili la kabila la Waha wakati wa sherehe za uzinduzi wa barabara ya Mwandiga- Manyovu. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto. (Picha na John Lukuwi).
   
 17. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli premises and conclusion are differ... kajipange urudi tena.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inaonesha hujui maana ya siasa.
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jakaya anasafisha Nyota kwa Zitto ha ha haaaaa. Magamba mnapenda kumfatilia sana huyu dogo. Juzi alikuwa Marekani akawananga mkakimbilia kumjibu Kitooooooooooooto
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Premises na conclusion weka wewe. Message delivered!

  Hapo nilipokuwekea nyekundu ilikuwa usiweke "are" kama umeweka "are" basi ungeandika "different".
   
Loading...