Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Na tutawavua sana Magamba! Tuko Kusini tunamalizia taratibu za Maziko ya CCM, Baada ya Mwili wa Marehemu CCM kupewa heshima za Mwisho huku kusini Tutaenda Kuuzika kwa Heshima Zote Tanga tukiongozwa na Kamanda Zitto Zuberi Kabwe

Tusaidieni kazi tuliyoianzisha, hapo tumewapiga kwa mtindo wa Kung Fu ujulikanao kama "Aap Ki Do", tunawapiga kwa kutumia nguvu zenu wenyewe, tunayavua magamba bila kutumia nguvu zetu.
 
ZOMBI lipo kazini linatafuta angalau ugali wa watoto kupitia thread Leo Nape hajaenda Bank utakula kisavu
 
Ila Zitto ananifurahisha sana kuwapuuza hawa Magamba ila akipata nafasi anawanyoa. Aliwanyoa Kirumba, akawanyoa Songea na akawanyoa Kiwira
 
sasa kama hampigii kura chadema bali zitto kwanni usianzishe chama chenu mumweke humo mumpe mavyeo yote?? shenzzigwa we

Unafikiri kura zote za Kikwete zilikuwa za wana CCM peke yake? ukingoja kura za chama chako tu, huukwai Urais hata ufanye nini. Kumbuka hilo darsa.
 
zomba, pole sana kiongozi, hizi hadithi mbona ni za kale sana? ilikuwa 1995, 2000, na 2005, tangu 2010 mambo ya propaganda za kuua upinzani haiwezekani kabisa, nakushauri mtafute mtu anayejiita wa 16 atakwambia, pia kaongeze elimu ili uweze kucheza na akili za watu, bado haujaweza kuutambua muktadha na emotion za watu na wakati.
 
Tusaidieni kazi tuliyoianzisha, hapo tumewapiga kwa mtindo wa Kung Fu ujulikanao kama "Aap Ki Do", tunawapiga kwa kutumia nguvu zenu wenyewe, tunayavua magamba bila kutumia nguvu zetu.

Ha ha ha Gamba Limenata Kiunoni na sasa Linajitwalia Nafasi nyeti. Ama kweli CCM ni kama Popo, si ndege si Mnyama
 
Wana wa Uamsho kazini.Itakuwaje ikiwa ccm watamsimamisha Bassaleh na chadema wakamsimamisha Zitto,je utamchagua nani?

Jenga hoja kama hoja ilovyotolewa, Shekhe Baswaleh ni mtu ambaye anaheshimika kwa watu wake hivyo kuleta mzani hambao haujui unapima nini sio vizuri na una kipunguzia credit chama kwamba kina harufu kidogo ya udini, kwanini usingetumia mfano mzuri wenye maana.
 
Ila Zitto ananifurahisha sana kuwapuuza hawa Magamba ila akipata nafasi anawanyoa. Aliwanyoa Kirumba, akawanyoa Songea na akawanyoa Kiwira

Huyo ndio mwana siasa na penye ukweli huwa anasema vilevile haogopi gwanda wala gamba. Ndio maana binafsi namkubali.
 
Wewe endeleza Propaganda hapa JF sisi tunavua Magamba Mtwara na Lindi
 
Huyo ndio mwana siasa na penye ukweli huwa anasema vilevile haogopi gwanda wala gamba. Ndio maana binafsi namkubali.

Mnamkubali au Mnamwogopa ha ha ha! Zitto hana Urafiki na CCM na Ataendelea kuwanyoa sana tu
 
Kusema arudi darasani maana yake aliwahi kuwepo huko, jambo ambalo sio sahihi. Mwambie arudi MADRASSA

Madrasa kwa Muislaam haiishi na haina kurudi, ni kila siku mpaka umauti unapotukuta, au hujui kuhusu darsa wewe?
 
Halafu watu wengine bana! Hivi Nafasi za U-DC ziko ngapi jamani mpaka inawafanya watu kukesha hapa JF kulamba miguuu ya CCM. U-DC utawafanya muanze kurogana vijana wa CCM
 
M4C: Kama ni Nyoka tunapiga Kichwani tu, Ngo Ngo Ngo With No Apology
 
Ukiona CCM wanakuja huku na kuanza Kulalama eti kwa Nini Zitto hayuko na Makamanda Kusini ujue kabisa M4C imekamata mahala pake. Sasa hapo tumetuma akina Heche mnalamika je akiingia Zitto mtaanza kusema mbona shibuda hayumo. Sisi tunatwanga tu
 
Kuna kila njama zinazofanywa kwa makusudi kabisa, kupunguzia kasi Zitto Kabwe katika jukwaa la kisiasa. Njama hizo zinatokea kwa vigogo fulani wa CHADEMA, wanaomuona kuwa Zitto ni mwiba mkali.

Historia ya karibuni ilionesha kuwa Zitto alisakamwa sana alipotaka kugombea uenyekiti na baada ya kuzipangua hoja zote za kumuumiza kisiasa ndani ya CHADEMA akaambulia kupoozwa kwa kusukumiwa cheo cha unaibu Katibu Mkuu, cheo ambacho hakina manufaa yoyote kwa CHADEMA wala kwa Zitto. Ili kuponesha maumivu na kutibu majeraha ya kisiasa, Zitto akakikubali cheo hicho, lakini ukweli ni kwamba hakifanyii kazi yoyote.

Uthibitisho mwingine wa kumshusha kisiasa Zitto ni pale ambapo hajahudhuria vikao vya CHADEMA na Kikwete huko Ikulu, kuna mambo ya msingi ambayo Zitto amekuwa akitofautiana na viongozi wengine wa CHADEMA na hayo ndio yanamfanya ajaribiwe kushushwa hadi na kutokuwekwa kwenye maamuzi mengi ya chama na yeye hustukia tu maamuzi yameshafanywa. Na anapotoa misimamo yake huwa ina tofauti na ya chama chake, mifano ipo mingi.

Tunawaasa vigogo wa CHADEMA kuwa hata ndugu zetu wa Kigoma walipopiga kura za Ubunge zilikuwa ni kura za Zitto na si za CHADEMA, hilo walielewe. Kama ilivyo kwa kura za Shibuda, zilikuwa ni za Shibuda lakini si za CHADEMA hilo linajidhihiri kwa kuwa kura za Urais za Kigoma 90% zilikuwa za Kikwete hata kwenye jimbo la Zitto.

Aliposhindwa Mbowe uchaguzi mkuu wa 2005, 2010 akawekwa Slaa, tunataka Zitto agombee 2015 tumpe kura zetu, kumbuka, hatuwapi kura CHADEMA tutampa Zitto Kabwe, bila yeye sahauni kura za wengi.

Kati ya vitu asivyopendezwa navyo Zitto ni namna ya chaguzi za wabunge wa upendeleo zinavyoendeshwa kimabavu ndani ya CHADEMA.

Tunawatahadharisha CHADEMA wasimjaribu Zitto, wataumia kisiasa.

Huko Kigoma kuna kura ngapi? mimi nadhani Zitto bado anahitaji muda kujijenga zaidi kisiasa na kujiaminisha kwa watanzani kuwa amekomaa kisiasa. Aidha anaweza kuwahudumia zaidi wananchi kwa kuwa Mbunge kuliko kuwa kiongozi.
 
Huko Kigoma kuna kura ngapi? mimi nadhani Zitto bado anahitaji muda kujijenga zaidi kisiasa na kujiaminisha kwa watanzani kuwa amekomaa kisiasa. Aidha anaweza kuwahudumia zaidi wananchi kwa kuwa Mbunge kuliko kuwa kiongozi.

Kigoma nimeweka mfano hai tu, kuwa kura zilikuwa za Zitto na si za CHADEMA kwani kwenye kura za Urais chadema waliambulia kidogo sana kuliko alizopata Zitto kwenye jimbo lake.

Mimi si wa Kigoma lakini Zitto namkubali na kuna wengi nnao-wafahamu wanamkubali Zitto.

Na Kikwete aliisha hint, anatamani Rais ajae awe "kijana". Nani zaidi ya Zitto kwa sasa, katika vijana kutokea chama chochote kile?
 
Ukiona CCM wanakuja huku na kuanza Kulalama eti kwa Nini Zitto hayuko na Makamanda Kusini ujue kabisa M4C imekamata mahala pake. Sasa hapo tumetuma akina Heche mnalamika je akiingia Zitto mtaanza kusema mbona shibuda hayumo. Sisi tunatwanga tu

Rudia post yangu uone kama kuna hayo unayoyasema. Nyie ndio wale wakuchakachuwa!
 
Halafu watu wengine bana! Hivi Nafasi za U-DC ziko ngapi jamani mpaka inawafanya watu kukesha hapa JF kulamba miguuu ya CCM. U-DC utawafanya muanze kurogana vijana wa CCM

Umri wangu ukiniita kijana ni sifa kubwa sana, saa hizi mie wakuamulia vijukuu mnapokosana, si wa u dc wala u cd.
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa​
ATAMBA, MAADUI ZAKE HAWATAMNYIMA USINGIZI
Moses Mashalla, Arusha, Raymond Kamnyoge, Dar
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amewapiga vijembe aliowaita maadui zake kisiasa wanaomchafua katika majukwaa mbalimbali akisema kuwa, hawamuwezi na hawamnyimi usingizi.

Lowassa akitambia maadui zake, kambi yake nayo imezidi kujizatiti baada ya mshirika wake kisiasa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amefanikiwa kukalia kiti cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi hivyo kuzidi kuongeza nguvu kwenye bungeni.

Jana, akiwa mkoani Arusha katika harambee ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Elaira, Lowassa alitumia sehemu ya muda wake kuwapiga vijembe maadui zake pasipo kuwataja majina akisema kamwe hawamnyimi usingizi.Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alitoa kauli hiyo, baada ya Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer kumtaka aendelee kufanya kazi ya Mungu licha ya baadhi ya watu kumkatisha tamaa.

Akizungumzia kauli ya Askofu Laizer, Lowasa alisema mahasimu wake kisiasa wamekuwa wakimsema kupitia vyombo mbalimbali vya habari, lakini akatamba kwamba juhudi hizo hazitaweza kufua dafu kwake kwani kelele zao hazimnyimi usingizi.

“Wanaonisema kwenye magazeti wala hawanisumbui, nasema hawaninyimi usingizi kwa kuwa mimi namtegemea yule anitiaye nguvu daima,” alisema Lowasa, kitendo kilichosababisha kushangiliwa na waumini waliohudhuria kanisani hapo.

Aliongeza kuwa yeye daima humtegemea Mungu amtiaye nguvu na kamwe hawezi kushindwa kulala usingizi kwa kusikiliza kelele zao za mara kwa mara.

“Nakushukuru Baba Askofu kwa kunijibia, wale wote wanaonisemasema kwenye magazeti wala hawanisumbui na wala hawaninyimi usingizi,” alisema Lowasa.

Alisema kwamba yeye ataendelea kumtumikia Mwenyezi Mungu ambaye amtiaye nguvu siku zote bila kujali maneno ya mahasimu wake wa kisiasa.

Kabla ya kuendesha harambee hiyo, Lowasa aliwaongoza waumini wa kanisa hilo kwa nyimbo zilizopo kwenye Kitabu cha Tenzi za Rohoni na kuibua shangwe kanisani hapo.

Kambi yake yajizatiti
Chenge ambaye ni mshirika mkubwa wa Lowassa kisiasa amechaguliwa katika kamati nyeti ya Bunge ya Fedha na Uchumi, akizidi kuongeza nguvu kwenye mhimili wa kambi hiyo.

Lowassa mwenyewe anaongoza Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama huku mshirika wake mwingine, Peter Serukamba akiongoza Kamati ya Miundombinu.

Katika uchaguzi wa juzi wa kamati hiyo uliotawaliwa na malalamiko ya vitendo vya rushwa bila kuelezwa ilikuwa ikitolewa na kambi ipi, aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti ni Dunstan Kitandula ambaye ni mbunge wa Mkinga.

Uchaguzi huo ulikuwa wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk Abdallah Kigoda aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda hivi karibuni.

Akizungumzia uchaguzi huo jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema, Chenge alipata nafasi hiyo baada ya kumshinda Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa.


“Mwambalaswa alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi kabla ya uchaguzi, hivyo aliamua kujiuzulu ili kugombea nafasi ya uenyekiti na Chenge, lakini akashindwa," alifafanua Dk Kashillilah.

Alipotakiwa kuzungumzia mizengwe na rushwa iliyotawala kwenye uchaguzi huo, Dk Kashililah alisema hawezi kuzungumzia hilo kwa sababu hakuwepo kwenye mchakato wa upigaji kura.

“Wanaoweza kuzungumzia hilo ni wale waliopiga kura ndiyo wanaweza kuelewa kama kulikuwa na mazingira ya rushwa lakini mimi sikuwapo,” alisema.

Tayari kambi ya Lowassa pia inaonekana kuwa na nguvu katika baadhi ya kamati kutokana na kuwa na washirika wenye msimamo wa wastani akiwemo Agustine Mrema wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) inayoongozwa na John Cheyo, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe na hata Kamati ya Bunge ya Katiba ya Sheria na Utawala inayoongozwa na Pindi Chana
 
Back
Top Bottom