Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,028
- 59,657
magamba yanajua kimeshanuka hapo 2015
Sio wananchi wote tuna vyama
magamba yanajua kimeshanuka hapo 2015
Ningependa sana kuamini lakini kwa maneno ya hapo juu kila nikisoma naona Pochi kubwa tu.. Maana siku hizi CCM wanakata sii mchezo ahaaahahaha!Hapana sijakatiwa pochi na mtu wala sitegemei kama kuna siku itakuwa hivyo.
Zitto ni kijana ambae hakuna ataepinga kuwa ameipaisha sana chadema, lakini kwa masikitiko makubwa naona chadema wanamtenga, sijui kwanini.
Namfatilia sana siasa zake, ingawa na yeye ni kama binaadam mwengine yeyote kwani sote sisi hakuna aliyekamilika, juu ya mapungufu yake lakini ni kijana anaejituma, mchapa kazi na anakwenda na wakati kisiasa. hayumbishwi hovyo na huwa ana misimamo katika hoja zake. Namsikitikia sana kuwepo CHADEMA kwani mwisho wa siku watampiga teke kama vile hajawafanyia kitu. Nyota njema huonekana Alafajiri.
Zitto hata akiwa chadema na akigombea basi kura yangu anayo.
Kuwa chama chochote hakumuondelei mtu umahiri wake wa kazi. Isipokuwa wale ambao hawakufanya lolote la maana kutoka katika vyama walivyokuwepo zamani, mfano Slaa alitemwa CCM katika kura za maoni kwa kuwa walishamuona kuwa hafai uongozi, wakati huohuo chadema licha ya kumpa shutuma nyingi sana Zitto wameshindwa kumpiga chini kwa kuwa ni kijana hodari na amezisoma mbinu na anapambana nazo akiwa humohumo ndani. Slaa yalimshinda hayo ya kupambana akiwa ndani ya CCM, inaonesha kabisa ni mtu aliyekuwa ana uchu wa madaraka na si uongozi.
Leo nimemsikia kiboko yenu kwenye ITV akikumbusha operation Sangara mwaka 2008, mlikuwa mkisema hayo hayo lakini kufika wakati wa kura mkaambulia wabunge 23 kati ya zaidi 200. Safari mkijitahidi sana mnaweza kuongeza viti vingine 23 vikawa 46. Tunawatakia kila la heri. Lakini Urais muusahau kabisa labda agombee Zitto kama bado atakuwepo chadema, hapo kidogo ntashawishika kwa sababu kura yangu atakuwa nayo (kama kuna uhai na majaaliwa) na ntampigia debe kwa wengine.
Ulimaanisha nini uliposema unamsikitikia kuwa CDM?
Zombi kanunua modem juzi Hana kazi ya kuifanyia zaidi ya kufungua thread na kuisimamia ili malipo kwa nape yawe makubwaNa wewe si tupo pamoja ndio maana ukaziona zote hizo. Au? Humu tutabanana sote, labda mtuambie CCM marufuku, mdanganyane wenyewe kwa wenyewe.
inshallah Mungu atatupa uhai..mimi kiukweli simpingi Zitto na wanaompinga zitto hapa wanapinga tu kwa vile wewe mwana ccm ndio umeileta hii mada hapa wakijua kuwa umelipwa,
la zitto akichaguliwa na chama basi tutakuwa nyuma yake,
kwa hiyo anza kukusanya watu kabisa huko piga kampeni za chini chini wainge madarakani kwani wakiingia hapo 2015,
hata kama Zito hatakuwa rais ila atakuwa kwenye cheo kikubwa na chenye maamuzi.
Mbona nyie hamumuenzi lowassa mmeiba Mihela kibao kawabebea mizigo yenu mpaka ya Rais wenuNamsikitikia kwa kuwa chadema hawamuenzi na kumkubali ipasavyo, hata ukisoma maoni tu ya wanachadema wa humu JF kuhusu Zitto utaona kuwa na uchapa kazi wake wote lakini chadema hawamthamini kwa sana, wanamuona kama yupo yupo tu.
Katika mitambo ya Dowans mkuu wangu sikuwa naye Zitto maadam sababu za chama chake zilikuwa wazi kabisa. Na binafsi yangu siamni kukunua mali ya dhulma, wizi, ama mali ambayo ingekuwa ushahidi mzuri wa kesi nzima ya Richmond dhidi ya EL maana ilikuwa chakavu, utapeli na wakabadilisha sheria ili tuinunue. Wewe kama mpinzani huwezi kukubali sheria ibadilishwe kwa ajili ya kitu kimoja tena chenyeb utata wa mkataba wakati nyuma chama chako kimepigana kwa nguvu zote kuondoa ununuzi wa vifaa chakavu baada ya kujifunza toka ATC, magari na vifaa ktk serikali na mashirika mengine ya Umma.Mkandara,
Nimekusoma na nimekuelewa. Mimi na Zitto labda afanye madudu yasiyo-sameheka. Namkubali sana tena sana.
Mfano mzuri ni pale alipopigania mitambo ya Dowans inunuliwe, wengi wakampinga hususan kupitia humu JF, mwishowe, umeme tukakosa kwa muda mrefu, mitambo tutailipia kwani mahakama zimeshaamuwa, na mitambo bado ipo na ndiyo inatumika kwa sasa na watu wote kimya. Jee, wangemsikiliza Zitto? Hasara tuliyoipata isingekuwepo au ingekuwa ni haba sana. Hilo wapingaji wakubwa walikuwa chadema wakiongozwa na mzee mwanakijiji humu JF. Nashangaa sana kuwa hata yeye kakaa kimya na mitambo inadunda.
Kwa mfano huo, namuona Zitto kuwa anaona mbali zaidi ya wanasiasa wengi na maslahi yake ni nchi kwanza.
Ulikuwa unatumia ya kuanzimaTazama tarehe yangu ya kujiunga.
Jaribuni kwa lowassa muone moto mtaishia kusema gamba mvueni asipo taja wezi wote mnamgwayaHayo yako wewe, mimi simo. Lowassa ni kiongozi mzuri sana.
Katika mitambo ya Dowans mkuu wangu sikuwa naye maadam sababu za chama chake zilikuwa wazi kabisa. Na binafsi yangu siamni kukunua mali ya wizi, mali ambayo ingekuwa ushahidi mzuri wa kesi nzima ya EL maana ilikuwa chakavu na wakabadilisha sheria ili tuinunue. Wewe kama mpinzani huwezi kukubali sheria ibadilishwe kwa ajili ya kitu kimoja wakati nyuma chama chako kimepigana kwa nguvu zote kuondoa ununuzi wa vifaa chakavu baada ya kujifunza ATC na mashirika mwngine ya Umma.
Pale kulikuwa na mchezop wa kumsafisha EL mapema na kupoteza ushahidi halafu unamlipa mtu yuleyule mbaya wenu kisheria. Hata kama mitambo hiyo imenunuliwa na shirika la Marekani na tumepachikwa kiraka ktk nguo yetu bado haina maana tunakubaliana na hatua iliyochukuliwa. Na kikubwa zaidi matatizo yetu ya Umeme ni zaidi ya uwezo wa Dowans wala hizo megawatts 100 hazikuwa sababu kabisa ya sisi kukosa umeme kwa sababu kama JK angetaka kununua mtambo mpya angeweza na kwa order ya siku moja. Kama unakumbuka toka mgogoro wa Dowans wakisema kuagiza mtambo itachukua miezi tisa ilipitwa miezi 16 kabnla ya mitambo hiyo kuanza kazi kwa hiyo CCM na uongozi walilazimisha kitu ambacho hakikutakiwa. Tumeozeshwa mke tusompenda.
Namsikitikia kwa kuwa chadema hawamuenzi na kumkubali ipasavyo, hata ukisoma maoni tu ya wanachadema wa humu JF kuhusu Zitto utaona kuwa na uchapa kazi wake wote lakini chadema hawamthamini kwa sana, wanamuona kama yupo yupo tu.
Inaonekana magamba wanatafuta kujua Zitto amepewa kazi kubwa katika kuhakikisha CDM kinaisambaratisha CCM. Maana kila siku watauliza mbona Zitto haonekani Jangwani? wakijibiwa watauliza katika M4C nako? wakijibiwa atashiriki saa ngapi katika kamati za bunge? Ulishawahi kujiuliza kwanini wafuga kuku wa kisasa kila cycle wanarudi kununua vifaranga na kwa nini wasizalishe wenyewe?