Sheria za kibinaadam hutungwa kwa nyakati zake, zamani darsa la kwanza watu wanaanza tayari washa balehe, imeshuka mpaka sasa hata miaka 5 wanaanza std 1.
Zamani ilikuwa inaaminika kila unavyokuwa ndio unakuwa na uwezo zaidi, siku hizi watafiti na wasomi wanaamini kuwa "productivity tends to fall with age" soma hapa:
Age and productivity: Over 30 and over the hill | The Economist
Nadhani ni wakati muafaka wakati tunaelekea kwenye kutunga katiba mpya umri wa kugombea Urais nao upunguzwe ili tuwe na highly productive president. Wewe unaonaje.
Sina nia ya kuwachafua chadema, kwani Zitto ni yeye mwenye aliyetangaza nia ya kugombea Urais na mimi namkubali na ikiwa chama chake kitamptisha na niko hai basi nnamuahidi kura yangu.
Lakini chadema "msimjaribu, mtaumia".
Mimi naamini uwepo wa upinzani wowote wenye nguvu (chadema kwa sasa) ndiyo chachu ya maendeleo na usimamizi mzuri wa mali za Watanzania.