Msimjaribu Zitto, mtaumia!

Msimjaribu Zitto, mtaumia!

zomba mshauri Zitto achukue fomu kama anataka kugombea na sababu zote ulizozitoa siyo sifaya kuwa mgombea Uraisi kwa sababu wengi wanazo........................we are looking for someone uniquely wise and free of official graft and Zitto's habds are full of filthy gunk.............................sijui nikumbushie barrick alikata ngapi pale..............sijui Tanesco kwenye Dowans alikatiwa ngapi...............the list is endless.................hakuna atakayempa bwana mdogo ugali na ikifikia huko bora wanamagamba waendelee tu kutesa........theyr are the devils we know............at least...........

Mimi si wa kumshauri Zitto achukuwe form, hiyo ni juu ya chadema na yeye mwenyewe.

Hivi kama kweli ana madudu yote hayo usemayo, bado mnamwacha tu? siamini mpaka uniwekee ushahidi wa kutosha na si kauli za humu kijiweni. Au ndio nikubali kuwa magamba ya ufisadi yanayojivuwa CCM yanadondokea chadema? Kwetu kuna operation vua gamba, kwenu kuna operation vua gamba vaa gwanda, sasa nimeelewa maana yake.
 
Hatumgusi kwa kuwa tunaogopa kulisahau jina la CCM tulimwambia ang'atuke tu. Zitto for President 2015!
Yaani magamba watu wa ajabu sana. Mnataka mtuchagulie candidate wetu 2015 huku ninyi mkiwa magamba. Amazing.
Chadema ni chama makini. Kitachagua mgombea makini wakati utakapofika 2015.
 
Wewe zomba wewe unataka kumwaga damu! Urais ndani ya CDM kwa sasa ni taboo kuusema. CDM wana kauli yao kuwa hata ukiweka jiwe dhidi ya CCM basi CDM itashinda! Hivyo kila mtu anadhani akiwekwa na CDM kwenye kugombea urais atashinda. Kila mtu anautolea macho urais huko CDM.

Kama ni taboo si mimi niliyovunja miiko, ni Zitto mwenyewe mwana chadema wa kutegemewa: soma zaidi:

SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015, kauli hiyo ...
 
Mwanzisha mada umekurupuka kwani hata katiba haimruhusu zito kugombea urais kutokana na umri wake, iweje ukurupuke na kudai atapata kura yeye kama yeye na siyo cdm wakati qualification zake hazimruhusu?

Hujui kuwa katiba ipo katika mchakato wa kuandikwa upya? isitoshe, katiba si msahafu kuwa haiwezi kurekebishwa. Na yeye ameshatangaza nia au hajui kuhusu katiba? Soma hapa.
 
Sisi tunatanguliza nchi yetu mbele sio mtu au chama mana vyote hivyo vinapita...cdm sio Zitto ni Taasisi ipo na itakuepo bila Zitto wala wengine wengi...kwani hata sasaiv kazi inafanyika huko kusini Zitto yupo huko?!! wewe vipi bana tafta chakula ule..njaa itakuua...

CCJ kilikuwa chama vilevile, kiko wapi? hata TANU na Afro Shirazi Party vilikuwa vyama, viko wapi? taasisi huanzishwa na watu, ikiwa watu wanaovianzisha wanakufa itakuwa vyama? fikiri!
 
Haya mambo hayo, vitisho vya kitoto na mbio za uraisi 2015. Mbona hujasema CHADEMA wataumiaje?

Katika wengi waliochangia, wewe umekuja na swali linalohusika na mada, nakupongeza kwa hilo. Wengi wanakuja na jazba.

Chadema wataumia kwa kuwa Zitto ana wafuasi wengi sana, kumbuka Zitto aliwafunguwa macho vijana na wakasema, kumbe inawezekana. Mtapoteza kiti chake cha ubunge. Mtapoteza na wafuasi wake wengi ndani ya chadema. Isitoshe, ana siri nyingi za chadema azijuazo, mko tayari zianikwe?
 
Kuna taratibu za kupata mgombea wa CDM 2015 hayo tuwaachie CDM ingawa ushauri wako kama wameuona utazingatiwa.
Ila I can see Dr Slaa as the president and Zitto as the Minister for Finance
 
2015 wana UAMUSHO hamna pakutokea. CCM watamsimamisha mbuzi katoliki na
Chadema watamsimamisha mbuzi katoliki. CUF hata kama watamsimamisha mwana
mfalme wa SAUDI ARABIA hawapati kitu. So kazi mnayo mwaka huo.
 
A lot of confused people in Africa...kuanzia madereva daladala, wa vibajaj na hatimaye wale wazee wa kazi muhimu nao wameanza kuchanganyikiwa....2015 bado mbali sana. Tuyamalize haya tuliyonayo ili 2015 iwe na smooth ride
 
Huwezi ku conclude kuwa zito anakubalika nchi nzima kwa reference ya uchaguzi wa kigoma! Ulishaweka mlinganyo wa slaa na zito jinsi wanavyokubalika countrywide? Zito ni jembe la ukweli chadema lakini chadema sio zito! Chadema ni wananchi! Ni wangapi wamehama vyama vyao kuja chadema kwa sababu ya zitto? Mapenzi yako kwa zito yasiwe conclusion ya hisia na mitazamo ya watu! Nenda kwa takwimu!

Unachosema nimekisoma na nimekuelewa, mimi binafsi namkubali Zitto, simkubali Slaa wala siikubali chadema.

Zitto katangaza nia ya kugombea Urais nami namuunga mkono na akigombea, mimi kura yangu anayo. Kila mtu na mawazo yake kuhusu siasa, sitazami anapendwa na nani ili nimkubali natazama yale ambayo nayaona mimi kuwa anayasimamia vyema kuliko mwingine kwa muono wangu.
 
Hapo kwenye red, wewe na nani? Sasa naona umetumwa, kuna chama kipya kimeanzishwa kinaitwa ADC mshauri zito aende huko mkampee kura zenu. Ama kama hilo litakuwa gumu mshauri asimame kama mgombea binafsi kama katiba itakuwa imepitishwa. Huku CDM asahau kusimama kama mgombea wa urais, hatutakubali hilo litokee, tunahitaji kamanda mpambanaji zaidi bishoo. Pamoja na mtu sisi tunachagua Chadema. Zitto ni mbinafsi na mpenda sifa, ni mroho wa madaraka. Baba wa taifa alitushauri kuwa ukiona mtu anakimbilia Ikilu huyo ni wa kuogopwa kama ukoma. Angekuwa na busara walau kidogo angeacha watu wampeleke kuliko yeye kukimbilia. Angengojea kama Dr Slaa mwaka 2010, sio kujikimbiza kimbiza.

Hapana Zitto anafaa kuendelea kuwa mbunge tu labda huko baadaye akikuwa. Mara natakuwa mwenyekiti wa chama, mara nataka kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, mara nataka kuwa rais; who are you? kusema hivyo si kwamba napuuzia mchango wake katika siasa za mageuzi nchini mwetu, lakini ana kiherehere mno.

Ushauri wa bure.

Tupo wengi tu, soma post #211. Bado sijapata cheo hicho cha utumwa, mie najituma.

Si mimi wa kumshauri Zitto awe chama kipi. Si mimi niliyetangaza nia ya kugombea Urais ni Zitto mwenyewe, nami namuunga mkono na akigombea kura yangu anayo nikiwa hai na debe ntampigia, ikiwa hatafanya madudu kwani siasa ni mchezo mbaya na 2015 ni mbali, tumuombee uzima, afya njema na uchapa kazi wa ziada. Zitto for President 2015.
 
Yaani magamba watu wa ajabu sana. Mnataka mtuchagulie candidate wetu 2015 huku ninyi mkiwa magamba. Amazing.
Chadema ni chama makini. Kitachagua mgombea makini wakati utakapofika 2015.

Hapana, hatuwachagulii "candidate" wenu, mimi nafata kauli ya Zitto ya kuwa ametangaza nia ya kugombea Urais 2015 au hujui hilo? kama hujui jikumbushe kwa kusoma hapa.
 
Kuna taratibu za kupata mgombea wa CDM 2015 hayo tuwaachie CDM ingawa ushauri wako kama wameuona utazingatiwa.
Ila I can see Dr Slaa as the president and Zitto as the Minister for Finance

Mimi siujui utaratibu wenu wala sina haja ya kuujuwa, mimi nafata kauli ya Zitto ya kutangaza nia ya kugombea Urais 2015 nadhani na yeye pia anaujuwa utaratibu ndio maana akaamuwa kutangaza nia, kama umesahau jikumbushe hapa.
 
2015 wana UAMUSHO hamna pakutokea. CCM watamsimamisha mbuzi katoliki na
Chadema watamsimamisha mbuzi katoliki. CUF hata kama watamsimamisha mwana
mfalme wa SAUDI ARABIA hawapati kitu. So kazi mnayo mwaka huo.

Too low.
 
Mkuu Zomba, nimekufuatilia tangu mwanzo.

Nakupongeza kwa kuwa mjasiri katika kujenga hoja bila jazba na kuzisimamia bila kutumia lugha ya kejeli.

Wengi wanaokujibu hawajatambua kuwa hapa umeweka kipima joto, na mpaka sasa kuna mafanikio makubwa ya kusoma hali ilivyo kwa suala unalozungumzia.
 
Mkuu Zomba, nimekufuatilia tangu mwanzo.

Nakupongeza kwa kuwa mjasiri katika kujenga hoja bila jazba na kuzisimamia bila kutumia lugha ya kejeli.

Wengi wanaokujibu hawajatambua kuwa hapa umeweka kipima joto, na mpaka sasa kuna mafanikio makubwa ya kusoma hali ilivyo kwa suala unalozungumzia.

Magamba yana tabia ya kujiona kuwa yanaelewa kuliko wengine wote Tanzania

Huu ni mfano tu
 
Back
Top Bottom