Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Kuna wakati lazima viongozi wetu wawe na uwezo wa kuona mbali kwamba wanapaswa kutokweka misimamo ambayo athari zake zitakuwa mbaya huko mbeleni.
In fact, kuwa na msimamo tofauti na matakwa ya wengi na ushauri wa watu wenye hekima ni kuwa na kiburi
Hili suala la kubadili kanuni za uchaguzi hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atasema kanuni zetu hazina tatizo, hata walio ndani ya CCM wanajua kwamba ni kweli zina tatizo na zimelenga kuwanufaisha wao. CCM wanachosema hadharani ni kauli za mdomoni tu, lakini wanajua kwamba madai ya Lisu na Chadema yake yana msingi.
Kila Mtanzania mwenye akili anapaswa kujiuliza; ubaya wa ushauri wa kubadili kanuni za uchaguzi ni nini?
Sasa Raisi Samia anapotoa kauli pinzani ili aonekane ana mismamo kama kiongozi, hasa baada ya kauli za viongozi wa dini kipindi hiki cha pasaka zilizoonyesha kwamba serikali inapaswa kusikiliza malalamiko kuhusu kanuni za uchaguzi na kuzifanyia kazi, matamko yeyote dhidi ya ushauri huo wa viogozi wa kidini ni kuleta mgawanyiko wa kidini nchini. Siku zote waumini wanatarajia viongozi wao wa kidini waheshimiwe katika wanayosema.
Raisi Samia anapaswa kuelewa kwamba anavyoshughulika na suala hili, kama asipotumia busara, nchi hii itaanza kupiga kura katika misingi ya udini. Serikali ya Samia inapoanza kuwabeza viongozi wa dini waliotoa matamko kuhusu kurekebishwa kwa kanuni za uchaguzi, watakuwa wanafanya kosa linaloweza kuigharimu nchi hii kwa kiwango cha juu sana.
Kuna makundi mawili nchini ambayo raisi mwenye busara anapaswa kuwa makini sana wanapotoa malalamiko - waalimu na viongozi wa dini. Haya makundi yako kwenye nafasi ya kuamua nani awe raisi wa nchi kwa sababu wana mfikio (access) kwa wapiga kura wengi sana nchini. Sahau hili kwa gharama yako mwenyewe.