Masanjaone
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 844
- 596
Mboe achia ngazi! Umetosha kupiga luzuku zetu.
Mkuu hapa umepotosha. Objectives za DA uchaguzi wa mwaka jana ilikuwa kuretain Western Cape na Kuishusha ANC chini ya 50% Gauteng na hilo walifanikiwa so si kweli Maimane alishindwa. Pia Kwa mara ya kwanza DA ilipata kura za watu weusi wengi kuliko wakati wowote ule kwenye historia ssa unaposema alifeli kuwavutia una maana gani? Kwa takwimu zipi?? Mkuu una credibility sana humu JF at least uwe unakuja na facts sio ushabiki.Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.
Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.
MM. Mwanakijiji
Kuna nyakati nyingine watu wawe na angalau aibu, wajisitiri ili wasionekane kwa misimamo yao kuwa wanawaona wenzao wanaosoma wanayoyawasilisha hawana akili kichwani.Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.
"Credibility"? You must be kidding.Mkuu una credibility sana humu JF at least uwe unakuja na facts sio ushabiki.
Rubish, I head is too small for this.Na. M. M. Mwanakijiji
Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.
Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.
Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.
India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.
Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.
Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.
Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!
Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.
Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.
Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.
Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!
Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.
Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.
Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.
Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.
Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.
MM. Mwanakijiji
Mkuu hapa umepotosha. Objectives za DA uchaguzi wa mwaka jana ilikuwa kuretain Western Cape na Kuishusha ANC chini ya 50% Gauteng na hilo walifanikiwa so si kweli Maimane alishindwa. Pia Kwa mara ya kwanza DA ilipata kura za watu weusi wengi kuliko wakati wowote ule kwenye historia ssa unaposema alifeli kuwavutia una maana gani? Kwa takwimu zipi?? Mkuu una credibility sana humu JF at least uwe unakuja na facts sio ushabiki.
Kuhusu Mbowe niseme tu ndio mwenyekiti pekee hapa TZ ambaye kila uchaguzi chama chake kinaongeza wingi wa wawakilishi ngazi zote na kura za urais kwahiyo hajafeli kama ulivyotaka kupotosha. CCM wao ndio wanaporomoka kila chaguzi from 88% to 62 to 56 sasa hapo nani failure??
Btw chaguzi za hao uliotaja ni huru na haki ndio maana mtu akishindwa anakubali matokeo ssa huku kwetu mnaharibu chaguzi kma Jecha ssa utasema kweli Maalim au Mbowe wameshindwa kwenye chaguzi?? Case study zako haziendani kabisa
Kiufupi mwanakijiji you are overrated!!
Mkuu kabla ya kupitia hoja zako, nianze na ya Mzee Mwanakijiji. Sikubaliani na hoja ya Mbowe kujiuzulu kwa sababu zifuatazo"JokaKuu, post: 34429132, member: 221"]
Kukukua kwa CDM kuna sababu..kwasababu kuna wengine wanaamini tangu Mbowe amekuwa mwenyekiti chama kimekuwa kikikua kwa kuongeza idadi ya mashabiki, wanachama, na wabunge.
Ubora wake unahitaji muda kuupima...pia ubora na udhaifu wa Mbowe
unaupima vipi?
Haiwezekani kumlinganisha nao, udhaifu wa hao ndio unakuza upinzani. Kwa wenyewe wanasema ''blessing in disguise''Unamlinganisha na wenyeviti waliopita wa CCM?
Hapana, udhaifu wa viongozi wengine ndiyo ilikuwa fursa kwake kuitumiaAu unamlinganisha na wenyeviti wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini?
Katiba mpya ni fyongo kubwa sana. Wakati wa JK CDM ilikuwa na nguvu ya umma haswa.Au unajaribu kuona ni wapi angeweza kufika, lakini hakufika, kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa na resouces at the disposal of his party?
Hii Chadema acheni kuhangaika nayo zaidi utaambulia matusi. Nafikiri maonyo yametosha, tubakie wapenzi watazamaji hadi tutakapokuja kupata watu serious.
Sent using Jamii Forums mobile app
You talk of them because you fear them!Duh... sasa unafikiria kiko wapi; peponi?
Mbowe ameonekana kuwa tishio kwao,so wamejaribu kila namna wameshindwa kumdhoofisha!Sasa wamekuja na hii,wanajaribu kuwahamasisha wanaCDM wamuone Mbowe hafai tena!Uzuri mbinu hii ishajulikana na nafurahi majibu wanayoyapata!Kwa mazingira ya siasa za Tz zilivyosasa ukianza kulaumu mbowe kwamba ndio anadhoofisha upinzani utakua una shida sio ya kufikiri tu bali njaa. Njaa ni mbaya sana. Anaetakiwa aondoke anajulikana ila kwasababu hatuwezi kukwambia basi muda utasema.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo nalo neno. Nadhani cdm inatakiwa iwaandalie vijana wa kuchukua hatamu za juu za uongozi e.g. Katibu mkuu wa sasa aliyelewa na cdm ni mfano mzuri wa hayo malezi.Tatizo cdm hawaandai viongozi, na inakuwaje ukubwa wote huu wa chama hakuna viongozi walio andaliwa kushika hatamu?
Mzee unateseka sana. Ulimponda Lowasa akiwa CHADEMA< karudi CCM Kimya. Hivyo hivyo kwa Sumaye & Co. Kwa nini unajifanya una uchungu sana na CHADEMA, wamekuomba uwahurumie?? Na kile kijarida chako cha CHECHE vipi cheche zimeisha??Watu wanafikiria kuwapoteza watu kama Kitila, Mwigamba, ni jambo dogo... wengine tuna maslahi zaidi na CHADEMA kuliko watu wanavyofikiria. Tungeshindwa uchaguzi fair and square 2015 leo tungekuwa kwingine kabisa...
Mzee Mwanakijiji nadhani unakuza fikra zako juu ya Aina ya siasa za Tanzania na kuona kuwa ni vizuri Mbowe akajiuzulu..... Kwanza hebu jaribu kuangalia haraka ni nani anayeweza kubeba na kusimama imara katika upinzani kama Mbowe. Lakini pia kwa mizania kutokuwa sawa dhidi ya viongozi wa vyama mbadala na wafuasi wao na pia kwa Aina ya siasa kwasasa na kwa faida ya taifa hili Mbowe ndiye anafaa kuwa kiongozi wa CHADEMA na upinzani kwa ujumla hapa Tanzania.Na. M. M. Mwanakijiji
Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.
Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.
Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.
India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.
Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.
Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.
Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!
Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.
Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.
Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.
Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!
Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.
Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.
Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.
Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.
Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.
MM. Mwanakijiji
Na. M. M. Mwanakijiji