Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Kwa hali inayo endelea hivi sasa ya kupoteza wanachama kila kona ya nchi wakati tunaelekea ktk maandalizi ya Uchaguzi mkuu ni busara Mbowe akijiuzulu haraka ili kulinda heshima ya chadema, vinginevyo chama kitamwifia na aibu itakuwa kubwa sana kwake.

Uhamaji wa wanachama unasababishwa Na uongozi mbovu wa mwenyekiti. Ni ushauri tu
 
Chama kipo mkononi mwa wanachama na sio mbowe ama wengine wanaofanana na mbowe....
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Alianza kuhama Lowasa. Wakafuatia Sumaye, Mwambe, na Mashinji. Wengine wako njiani.
Tafuteni angle nyingine ya kuifuta CDM.
 
Poa, tutamwomba akae pembeni.

Ila nafasi yake ataichukua Tundu Lissu kisha Umakamu tutampatia John Heche naona ahapo hoja zenu zitakwisha mtaanza kuleta maada za maana kama Kwa nini Taifa halisongi mbele kwa maelewano.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

MM. Mwanakijiji

Incredible! The sound of war drums at last. In the US’s foreign policy strategy, they say “all options are on the table”. And grasped by the eagle’s claws are an olive branch on one leg and a bunch of arrows on the other.

Seems Mr. Mbowe is still missing the point. After decades of consistent provocation and gross repression of the opposition by the State Party, reaching climax in this regime, he is EXPECTED to engage the only remaining option: combat/violence. Since he has demonstrated lack of guts for the fight, he is being asked to give way for a more warrior type of leader OR capitulate/acquiesce to the powers that be! It’s a daring taunt to Mbowe and CHADEMA.

This is the clear message being stated here. (I can even imagine the sneering grin). Only I’m wondering about the exact objective of the proponents.
 
Ndugu zangu,

Kuna msemo unasema ''ukiona kenge anatoa damu kwenye masikio ujue anakufa''. Siasa za Tanzania zina mtindo wa kujirudia rudia usipokuwa makini na kukaza shingo, lazima itakatika.

Nakumbuka jinsi Mrema alivyokimbiwa na akina Prof.Baregu, Marando na wengine lukuki alijipa moyo na zaidi aliwadhihaki akawaambia waende wanakotaka, aliamini chama chake kilikuwa kinajisafisha.Ikumbukwe Mrema ni mmoja wa wanasiasa waliwahi kutikisa medani za siasa za nchi hii ambaye vijana wa wakati huo wakiongozwa na Lissu na Mbatia walisukuma gari lake mara kadhaa mitaa ya Jangwani, Magomeni, Manzese hadi Ubungo.

Ilipothibitika kuwa umaarufu na nguvu ya Mrema kisiasa imeshuka mara kadhaa hata bungeni alikemea kambi rasmi ya upinzani na kuwatambia kuwa yeye alikuwa ''mpinzani'' mwenye nguvu kuliko wao. Muda unaenda kasi sana, leo na miaka ijayo ndugu yangu Mbowe na CHADEMA wanapitia njia hiyohiyo.

ACT Wazalendo kwa turufu ya Zanzibar wanaweza kutengeneza kambi rasmi ya upinzani bungeni. Zitto ni fahari asiyekubaliana na Mbowe na kundi lake kiasi walitamati awe ameshafilisika kisiasa. Siku Zitto akitangazwa kuwa KUB hapa Mbowe na CHADEMA hawatamuunga mkono, wataweka nongwa na ghubu hapa ndipo CHADEMA itaonesha ''UCCM B'' bila chenga na hatimaye kutetereka kufikia ilipo TLP (NCCR-Mageuzi).

Siasa ni sayansi, wenye uwezo mdogo kufikiri watatukana, watakejeli wakiamini kuwa wanatetea chama badala ya kutulia wakijenga hoja na kufanyia kazi ushauri.

Baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 CHADEMA walikuwa na msemo ''Acha woga, tukutane 2020'' kauli ambayo sasa hivi imefutika kwenye vinywa vyao na kuhamia kwenye kauli isiyohakisi imani yao ya ''No hate no fear'' ambayo imeasisiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Dr.Mashinji.

Tujenge hoja bila vurugu.

''Ajizi nyumba ya njaa''
 
Wakudadavuwa,

Wakudadavua sijui una kichaa

Ni mwaka wa 28 huu mnaongea hivyo hivyo

Usimfananishe Mbowe na vitu vya ajabu kama Mrema

Mbowe ni mwenyekiti mwaka wa 20 kasoro,na mnaongea upuuzi huo huo,Mrema alikua mwenyekiti NCCR kwa miaka 5 akaharibu kila kitu

Kaingia TLP ambacho si chama ni mavi ya chama dont even mention that here!

Uwe serious aisee!
 
Kwanza nikitarajia uoneshe kujirudia kwa siasa za Tanzania hususan ukilinganisha siasa za wakati huo na sasa ili tuweze kuona kwenye mizani.

Pili, umeonesha nguvu na umaarufu wa Mrema ilivyosaidia kuinua Chama chake na ukakiri nguvu yake ilivyoisha na habari ikaishia hapo.

Je, Chadema hii tunayoiona ni kwasababu ya nguvu au umaarufu wa Mbowe? Au umaarufu wa nani? Je, Mbowe na Mrema wanafanana?

Chadema na TLP au NCCR ya kipindi hicho vinafanana? Kimuundo, ukuaji na nk? Ukiweza kutuwekea uchambuzi wa haya utakuwa umetusaidia.

Nakubaliana na wewe siasa ni sayansi na sio ujambazi.
 
Wakudadavuwa,
Pole sana,
Ndugu yangu yaonekana inapofikia yanayomhusu Mh Mbowe na CDM huwa unaongozwa na chuki binafsi kuliko hoja, lakini wataka ujibiwe kwa hoja.
\
Hiyo yakufanya ueleweke WAZI kuwa wewe si mtetezi wa haki wala huna upendo kwa wanyonge wa nchi hii kama ambavyo huwa mnajaribu kujinasibu. Wala sina hakika kama una kifahamu unachokitafuta kwa nchi hii, lakini kwa vyovyote vile SIO AMANI wala maendeleo ya kweli kwa ajili ya watz.

Ila nina hakika kuwa SAFARI hii mtashindwa hata kwa yale mliyofanikiwa kwa Mh Mrema. Kama mafarisayo waliyofurahia na kushangilia sana njama na kusulubishwa kwa Yesu, itabidi uje kutunga uongo mwingi kupotosha ukweli kuwa yu hai.
 
Hii ndiyo kibri yenu ilipo
tapatalk_1582299881767.jpeg
FB_IMG_1582080397242.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu msemo CDM inakufa umeanza kutumika miaka mingi sana iliyopita!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alianza yule mzee wa Kwa Esther Bulaya kwamba Chadema inakufa, Esther Bulaya akamgaragaraza akafa kifo cha mende, akaja Komba akasema Chadema inakufa badala yake akafa yeye, Dr Kaborou akaondoka wakasema Chadema inakufa, Dr. Slaa wakasema Chadema inakufa, wengi wameondoka akina Tumbiri, Machange, Waitara, bado Chadema inawalimisha kwa meno, wakaja kutumia nguvu za usalama wa taifa na polisi bado Chadema inawalimisha kwa meno.

Chadema hiyo kila siku haishi midomoni mwao lakini kila wakijaribu kuizuia ndivyo inazidi kukua na kupanuka. Ukitaka kuujua ukweli ebu waipe mwezi mmoja tu wafanye mikutano uru waone cha moto, au ukitaka kujua woga wa yule wanamuita ni mfu wambie tume uru uone wanavyojikojolea kwa woga.

Chama kinachokufa wnakiogopa nini? Tangu lini watu wakakimbia maiti si wakae mkao wa kuizika? Chadema inawaendesha puta mpaka hawajielewi. Chadema ina vijana ni nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa Maendeleo yao na ya Taifa. Hakuna ubishi ya kuwa watanzania wengi wamekata tamaa na hatima ya kiutawala katika nchi yao.

Wengine wanajiuliza kama hii kweli ni nchi yao au ni wakimbizi. Wengine wameamua kususa na wengine wameamua bora liende. Mfumo wa kiutawala umewaathiri watu wengi wa nchi hii hasa wakiwepo masikini ambao hatima yao ya jioni (achilia mbali ya kesho) hawaijui. Chadema ni ni mwanzo wa nuru mpya katika zama mpya.
 
Mwananchi,
Aliyewahi kuvuma akifa hasahauliki

Mitume, mandela,.nyerere, washington n.k

The fact that they talk about you is just because they once adored you dearly
 
Back
Top Bottom