Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Yaani mawazo yako unayaita Msimamo Rasmi .... MMKJJ acha utani...!!

Unaona ni rahisi tu kwa wao kutoka. Je, safu ya kuwabadilisha wote hao ipo?? Kwenye timu kama mambo hayaendi hubadili team nzima either ni coach au baadhi ya wachezaji au unaongeza/badilisha kamati ya ufindi.

Inawezekana kabisa coach bado yuko poa sasa inabidi baadhi ya wachezaji kama akina Pogba (Mashinji) wapumzishwe ili team icheze!!
 
analipwa , kuna wakati alipendekezwa na Mwakyembe apewe UDC lakini utata ulijitokeza kidogo upande wa elimu na mashambulizi yake kwa ccm na Magufuli siku za nyuma kabla ya kukengeushwa na Dr Slaa akapigwa chini .
kumbe ndio maana anajaribu kusawazisha mambo kwa kuandika upuuzi huku, but kwa umri wa huyo mzee naona bora aache mawazo ya kujipendekeza, muda umeshamtupa mkono.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleza ukabila!!

Tunajua uko mlengo gani kwa faida ya nani.

Wewe ni sawa na zilpendwa,hakuna wa kukuamini tena.

Uliheshimika kwa hoja zako na si kwa jina lako unalotaka kuendelea kulitumia kwa faida ya unaowatumikia.

Mapandikizi yenu yamefeli sasa mnatapata!!

Wewe na Dr.Mihogo wote wanafiki.
Hamuipendi CHADEMA nyinyi
 
Kumuona mwanakijiji kwamba ni munafiki, hakuondoi ukweli kwamba Mbowe ameharibu CHADEMA na upinzani kwa ujumla. Kwa nini ang'ang'anie nafasi ya m/kiti kwa kisingizio eti amekitoa mbali. Mbali wapi na sasa yuko wapi? Huo ndo mwendo pekee wa CHADEMA na kwamba sasa hakuna nguvu nyingine? Akishabikiwa ki-ukabila anajiona anafaa sana, ukweli unabaki kwamba ni sifa za kijinga kusifiwa na kabila lako, nawe unaamini unaweza ongoza chama kushika nchi ya makabila 120.
Nani anamsifu Mbowe kwa kabila lake? huko lumumba ndio mnaendekeza hizo propaganda za kipuuzi, Mbowe haondoki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[Ni QUOTE="Mr. Zero, post: 34434970, member: 3306"]
Yaani mawazo yako unayaita Msimamo Rasmi .... MMKJJ acha utani...!!

Unaona ni rahisi tu kwa wao kutoka. Je, safu ya kuwabadilisha wote hao ipo?? Kwenye timu kama mambo hayaendi hubadili team nzima either ni coach au baadhi ya wachezaji au unaongeza/badilisha kamati ya ufindi.

Inawezekana kabisa coach bado yuko poa sasa inabidi baadhi ya wachezaji kama akina Pogba (Mashinji) wapumzishwe ili team icheze!!
[/QUOTE]
Ni wakati gani utajua tatizo siyo wachezaji bali ni kocha na timu nzima ya ufundi?
 
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.
Wote waliotaka kugombea nae wamerudi nyumbani kwa waliowatuma maana ngoma imedunda. Hizo mbinu mpya unazozitaja ni za kuendeleza chama ama kukiuza kama wengine walivyouza ubunge/udiwani wao?
 
Write your reply...Ni sahihi kabisa Muda wake umefikia Mwisho,Hana kipya kabisa kwenye siasa za kitanzania!! zaidi ya kubuni mikakati mfu
 
Nilichojifunza mimi kwa umri wangu huu mdogo na shule yangu hii ya st kayumba ni kwamba ukiangalia kwa kina utaona kua vyama vya upinzani havijawai kushindwa kua na hoja au sera nzuri hadi vikafa au kua dormant bali kilichovifanya viwe dormant ni siasa chafu ambazo zimekua zikiendeshwa na chama kinachoongoza serikali na kinachooneka sasa kwa Chadema ni muendelezo ule ule ila naona safari hii hicho chama kinachopiga wenzake misumari kimeangukia pua kwa Cdm na hadi sasa dakika 87 ngoma bado bila bila pamoja na kujaribu kuingiza nakubadilisha wachezaji mamluki.Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu anajua tatizo lilipo uko kwingine nikujifanya hamnazo tu uku tukikwepa kunyoosha kidole kwenye tatizo.Kwaiyo mzee kama wewe unaona tatizo liko kwa mbowe na Cdm ni vyema ukawaacha ili chama kife na chama dola kishinde kwa kishindo.
 
Uliposema hawawezi kuwekewa zulia nilikuelewa vizuri sana mkuu. Wao wanakuona hufai ila waelewe ulichowashauri. Wajipange vizuri wabadili gia wakitua sio angani.
 
Hamuipendi CHADEMA nyinyi
MMKJJ, Tanzania kwa sasa haina tarents kama huko nyuma. Siyo CCM siyo Upinzani. Hivi kuna vijana wangapi CDM wanaweza kuireplace hiyo team ya sasa ya Mbowe. Wewe ndiye usiyeitakia mema CDM.

Tumeona jinsi gani JK alivyosota kupanga team yake mwisho skawarudia wale wale akina Mangula, Kinana. Hii ndiyo sababu mpaka sasa Mangula anadunda well beyond his retirement.

Kinachomsaidia Yohana kwa sasa ni ubabe wake ulivyofanikiwa kuzimia opposition otherwise akina Bashiru, Polepole wasingeweza huo mchezo.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT

Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji

Sisi em itafanya party ya Tshs 1 billion
 
Back
Top Bottom