Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Inaonekana mnacomment kwa hisia sana, ila mbona riport imetoa sababu nyingi sana? Fanyeni utafiti ndio muongee na nyinyi......... Ccm songa mbeleeeee!
 
At the end of the day, ccm has to realise it's just a political party. It's bound to be challenged and its performance is measured by the public! So if they cant perform, while the country stumbles from one crisis to another, it is logical to lose support. This is the basics of multi-party democracy.

Nimeipenda hii, very well said, lakini inabidi uimbe taarab ya hayo maneno ili CCM wayaelewe.
 
Miye nimejiunga tu na JF baada ya kuvutiwa na mada na michango mbalimbali ya kuchangia mada basi, nani anamiliki JF mi sijui na wala sina haja ya kujua maana sikuulizwa itikadi yangu ya kisiasa, kidini wala kabila wakati wa kujiunga. Kama ningeulizwa hayo at least ningetia shaka kidogo kwa nini niulizwe hayo, hivyo sina wasiwasi na JF, naamini ni uwanja huru wa kutolea maoni huru bila kujali itikadi za kisiasa, kidini na kikabila, ni mkusanyiko wa watu wa kila aina.
 
Sasa hivi kila mtu anayetumia JF au kuonekana JF maofisini au mitaani ataonekana ni Chadema.. so watch out huko maofisini.. hii ni gia ya kuanza kuwa na censorship police!!!
 
Umemsahau Kigwangalla pia mkuu.

Something is very wrong somewhere. CCM wakija kushtuka wanaweza kuwa wamechelewa. Ushauri mwingine unaweza kudhani umetolewa na Malaria Sugu (as a joke).

Ukiikosoa CCM au CHADEMA unakuwa hasimu wake, jana napata sms nyingi tu toka kwa watu wa CDM ati tumewapa air time kubwa CCM kwenye vikao vyao, sasa nao soon wataambiwa kwenye NEC yao kuwa JF imenunuliwa na CCM?

Kazi ipo kubwa, mpaka watu waelewe maana ya Citizenry Journalism basi tutakuwa tushabatizwa kila aina ya majina, mahasimu, wanafiki, waongo n.k
Max na wanajamii...

Kuna tatizo kubwa kwenye timu ya sasa ya CCM, na tatizo hilo yawezekana linaambukiza kwa kasi ya ajabu

Nasema hivi kwasababu "consultant" wa CCM ameshindwa hata kwenda into details (kama anaweza) kuelezea impact ya JF kwao, impact ya other forums and social netwrorks kwao na hata effect ya UTUMBO WA BAADHI YA VIONGOZI WAO

Hivi nchi ina watu 45M inakuaje waishiwe usingizi na members 36,000+ ambao kwayo a few have multiple IDs, some are CCM members, some only subscribe to limited forums (ambazo sio za siasa) and others are CCM members kama yule ajiitaye Mzanzibara, au Kupenge, Masatu, Kibs nk???

IF CCM WANTS TO ESTABLISH SOMETHING LIKE JF SAWA, LAKINI IF THEY WANT TO START MPINZANI WA JF THEN WATAISHIA KUWA NA MEMBERS LESS THAN 1000 NA WATAKOSA WACHANGIAJI KWANI HAWATAKUA NA CHALLENGES - THEY WILL AGREE ON EVERYTHING AND END UP BORED

SADLY, CONSULTANT KALIPWA KUWADANGANYA WAKUU WA CCM, INCLUDING JAKAYA MRISHO KIKWETE (RAIS WA JMT)!!
 
Viwanja vipi tena hivyo??........isiwe CCM KIRUMBA na vingine vya namna ile..!!!

...Ndo hivyo hivyo! Wanadai viwanja vyote vya mpira ambavyo vilijengwa kwa nguvu za wananchi ni vyao. Tena kama kile cha Nyamagana walikuwa wakiuze mwa Mhindi fulani hivi, sijui mwendawazimu gani aliwashtua kwamba wataleta vita na wananchi waliokijenga, iwapo kitauzwa, wakanywea.
Kweli sisiemu wamefulia.
We run JF
 
Sasa hivi kila mtu anayetumia JF au kuonekana JF maofisini au mitaani ataonekana ni Chadema.. so watch out huko maofisini.. hii ni gia ya kuanza kuwa na censorship police!!!
Very true mkuu

Nakumbuka nilivaa Tisheti ya JF niaambiwa kumbe wewe CHADEMA?? i failed to understand some people
 
Sasa hivi kila mtu anayetumia JF au kuonekana JF maofisini au mitaani ataonekana ni Chadema.. so watch out huko maofisini.. hii ni gia ya kuanza kuwa na censorship police!!!

Acha utani bana,
Ina maana hata wakikuta nipo cafe naperuzi Jukwaa la lugha watahisi ni jukwaa la siasa? Napigana
 
Sasa nimegundua CCM wako karne ya 17 kwani JF ndio walioiba EPA, ndio waliofelisha wanafunzi kidato cha nne, ndio waliolipa management ya PPF, ndio walioleta Richmond/Dowans, ndio wamesaini mikataba mibovu ya migodi,ndio wanapandisha bei za bidhaa.

Mimi nawashauri CCM washughulikie japo hayo matatizo niliyoyataja kwa kuwapeleka wahusika mahakamani na wafungwe sio kufanya changa la macho halafu warudi wasome JF waone maoni ya watu.

Mimi sidhani kama JF ndio wamefanya maisha ya mwananchi wa kawaida kuwa magumu kukosa maji safi, shule bora, huduma za afya bora, na nyingine nyingi tu.
 
mimi siwezi kutoa maoni mpaka niisome ripoti ya CONSULTANT

Media zetu ni za kinafiki sana...one minute wakishapewa pesa hanafumba macho kuhusu tuhuma mbali mbali za ufisadi ...lakini sehemu zingine wanajifanya eti wamefichua ufisadi....they are just practising DR SHAYO JOURNALISM in otherwords waandishi wetu wa habari ni bogus na kila mtu analijua hilo so I cant jump a gun on kuishambulia article ambayo imeandikwa na "MWANDISHI WETU" surely kama mtu hataki credibility yake iwe questioned kwa nini anaandika kwa kutumia kivuli cha MWANDISHI WETU?
 
Hivi CCM inahitaji vyombo gani zaidi za kuzinadi ina maana Gazeti la Uhuru na Mzalendo hazifanyi kazi? Je TBC1 (muda mwingi hutumiwa kuripoti mambo ya CCM) na yenyewe pia haifanyi kazi?

Mbona kipindi kile waliambiwa wajitokeze kwenye Mchakato majimboni walikataa, Je leo hii wataweza?

Kwa taarifa yenu Mwanahalisi lina soko kubwa Monduli kuliko gazeti lolote lile.
 
Kadhalika, chama kinataka kuimarisha mfumo wa uwekaji wa kumbukumbu za mapato na matumizi, kustaafisha waliofikia umri wa kustaafu.
This is a big joke...

Nimepitia mashirika mengi ya umma na nikaona JK amewaongezea muda wa mikataba watendaji wengi wa taasisi hizo......... Mfano shirika la Hifadhi la Ngorongoro kibosile pale tayari alikwisha kufikisha umri wa kustaafu tarehe 9th Machi 2011 lakini kwa vile Mwenyekiti wa Bodi ni swahiba wa JK BW. Pius Msekwa ambaye naye ana kashfa nzito za kuliendesha shirika hilo kwa misingi ya ukabila na nafasi nyingi za juu ikiwemo ya CEO kampa mkerewe mwenzake.....it is no surprise kibosile yule JK kamwongezea mkataba wa miaka miwili wakati vijana wengi wasomi wako mtaani wanasaga lami....

CCM will never change power ebbs out of it......
 
Sasa hivi kila mtu anayetumia JF au kuonekana JF maofisini au mitaani ataonekana ni Chadema.. so watch out huko maofisini.. hii ni gia ya kuanza kuwa na censorship police!!!

Mzee Mwanakijiji........you need to qualify this statement....do you mean CCM even consider Malaria Sugu - whose unrelenting campaign to defend CCM in JF during 2010 general elections remains nonpareil - is part of Chadema war-chest?
 
Nimesoma habari hii chini nikabaki kujiuliza; "Kama huyu ndiye Consultant wa Chama Tawala; hivi washauri wa serikali wanatoa ushauri wa namna hii pia?"

Napata wasiwasi kuwa Consultant huyu kafanya kazi kwa hisia na si kiutaalam kama mlivyotarajia; kama ndiyo njia iliyotumika pia kwa kina Lowassa na wenzake basi kuna uwezekano wengi wameonewa kwa kisingizio cha 'consultant'.

Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.

NB: Nilikuwa nirejee na maelezo marefu, lakini nimefahamishwa na mods kuwa kuna maelezo siku nyingi hapahapa JF; haya hapa

Msimamo wetu na maelezo kidogo




Habari yenyewe ni hii:


Kamati imedhamiria kuwa CCM nayo ifanye bidii kutumia fursa hizo za mawasiliano kama vile kuanzisha vyombo vyake ambavyo vitapambana na hasimu wao kama Jamii Forum.

Mkuu Melo,

Habari husika ilyotoka kwenye gazeti la Nipashe si ngeni mimi binafsi nimekuwa nikishauri wenye mtandao huu kuweza kujaribu kwa makusudi kujipambanua na shutuma kama hizo kuna baadhi ya watu wanadiriki hata kutukana viongozi wa serikali. Kuna kipindi kuna mtu aliwajibishwa kwa kumtukana spika kupitia JF nadhani mlifanya kitu kizuri kumBAN yule member. Lakini mmekuwa mkiwaachia baadhi ya member hapa JF kuwadhihaki viongozi kwa majina ya "vilaza" "mkere" na mengineyo kuna hata waliothubutu kupost picha ya kiongozi mkuu ndani ya serikali akiwa ana umbo la kike na kuandika jina lake kwa kifupi na kumalizia neno "original". Huu si ustaarabu hata kidogo nimelizungumzia mara nyingi na kulitolea mfano kuwa huyu ni kiongozi na ni baba na mjomba wa watu wengine wanampenda mapenzi ya dhati wanaumia wanapoona dhihaki kama hizo! na wanachama wake watiifu na wao wanaumia kwa dhihaki zisizo na msingi zaidi ya kumtusi mtu! nikaenda mbali na kusema vitendo kama hivyo mathalani akifanyiwa yule anaependwa na wanaJF wengi pia wataudhika dini yetu imetuasa tuzipende nafsi za wenzetu kama tunavyozipendelea nafsi zetu.

Nadhani tatizo si JF owners ila ni utashi wa members wengi wa JF nitatolea mfano kuna member siku chache zilizopita kama si jana alianzisha thread ya kumtaka Dr Slaa na yeye awajibike kwenye CDM na akatoa hoja zake ni kuwa chama kujipambanua na shutuma za udini kwakuwa Dr alipata kuwa Padri. Mawazo ya member huyo ukiyaangalia kwa namna moja au nyingine yana ukweli kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa (kwani propaganda ya CDM ni chama cha kikanisa) imeshika kasi kama moto nyikani. Lakini mimi na wewe na yule tumeshuhudia wachangiaji wa thread ile nadhani ifike wakati tuwe wastaarabu.

My take:

CCM na CDM wasihamaki watakapopingwa hadharani kwani hilo litawasaidia kujipanga lakini lugha nzuri na hoja zitumike kwenye kupinga baadhi ya mambo ya vyama hivi.

Ningependa kuona JF inakuwa kisima cha fikra pevu che kuelimisha maswala mbalimbali ya kijamii na kisiasa ni wakati wa sisi members kujivua gamba!
 
PHP:
Kadhalika, chama kinataka kuimarisha mfumo wa uwekaji wa kumbukumbu za  mapato na matumizi, kustaafisha waliofikia umri wa kustaafu.
This is a big joke.............................nimepitia mashirika mengi ya umma na nikaona JK amewaongezea muda wa mikataba watendaji wengi wa taasisi hizo..........................mfano shirika la Hifadhi la Ngorongoro kibosile pale tayari alikwisha kufikisha umri wa kustaafu tarehe 9th Machi 2011 lakini kwa vile Mwenyekiti wa Bodi ni shwahiba wa JK BW. Pius Msekwa ambaye naye ana kashfa nzito za kuliendesha shirika hilo kwa misingi ya ukabila na nafasi nyingi za juu ikiwemo ya CEO kampa mkerewew mwenzake...................it is no surprise kibosile yule JK kamwongezea mkataba wa miaka miwili wakati vijana wengi wasomi wako mtaani wanasaga lami...............................................

CCM will never change until power ebbs out of it.....................................................


Hapo kinaongelewa chama ndugu. Una maaa kuwa kwenye mashirika na bodi zake za wakurugenzi yako chini ya chama cha mapinduzi?
 
Wachangiaji wa JF wengi sio wajinga kwa kiasi flani wanajitambua kuliko makundi mengine ya jamii.

Hoja ya JF kuwa ni CDM haina mashiko ni sawa na ile ya kuilaumu CDM kwa mienendo ya Universities, HAPA BORA CCM waseme kundi kubwa la wasomi, waelewa, wenye utambuzi haliitaki.

Songa mbele JF, hapa tunawakilisha bila chenga
 
PHP:
Hapo kinaongelewa chama ndugu. Una maaa kuwa kwenye mashirika na bodi zake za wakurugenzi yako chini ya chama cha mapinduzi?

Kama serikali CCM inayoisimamia inaendeshwa bila misingi ya kiutu na utawala bora unategemea ahadi hizo ndani ya chama zitawezekana?

Nilipokuwa shule kuna mwalimu mmoja alitufunza ya kuwa pua inakoangalia haiwezi kubadilika na kesho ikaangalia vinginevyo? Usifikiri sijui kuwa yanayozungumziwa ni ndani ya CCM lakini tabia yao nje na ndani ya CCM ni ushahidi kuwa hawawezi kujirekebisha..................wananzungumzia baadhi ya viongozi kujirundikia vyeo lakini huo ni mkakati wa JK kununua uzalendo ndani ya chama na serikalini................................He is buying loyalty at an incredible national pain.............................and that will never change..............................cronyism culture defines and sustains CCM in and outside it.......................
 
hata wafanye nini temechoka kuambiwa wembe wa zamani, makali yale yale. Huu ni uongo tena usiokuwa na fikra. We need change bana.
 
hata wafanye nini temechoka kuambiwa wembe wa zamani, makali yale yale. Huu ni uongo tena usiokuwa na fikra. We need change bana.

Hapo ndio huwa sitaki kushiriki siasa wembe upi mpya? tukiangalia vyama mbadala wengi wa viongozi ni nyembe za zamani tena zilizotoka kwenye hicho chama unachosema ni wembe wa zamani hakuna jipya kikubwa watu waangalie maslahi ya Taifa wasiangalie maslahi yao binafsi. Si tumeshuhudia waliotemwa kwenye kura za maoni CCM wakitimkia CDM na kupewa madaraka? ina maana wao walikuwa wanataka "ulwa" pengine kwa kuukosa wakaamua wautafute kwa gharama yoyote hata ikibidi kusaliti "itikadi" walizoziamini awali? je tuna uhakika gani siku itokee wakaangushwa kwenye mchakato wa uongozi ndani ya CDM na kuambua kurejea walipotoka?


My take.

Hakuna wembe mpya wembe ni ule ule unageuzwa leo upande huu kesho upande mwingine TAFAKARI
 
Bora wakazane kuitumia Clouds FM maana inamashabiki wengi huko wanaweza wakakiimarisha chama.

Hiyo Uhuru FM full mipasho nani atasikiliza hata Makamba mwenyewe hasikilizi.

Mashabiki wake wamepungua sana mkuu. Imebaki kuwa ya mahausgeli wakisikiliza kipindi cha kuchagua hausgeli bora...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom