Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maxence Melo, Apr 12, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Nimesoma habari hii chini nikabaki kujiuliza; "Kama huyu ndiye Consultant wa Chama Tawala; hivi washauri wa serikali wanatoa ushauri wa namna hii pia?"

  Napata wasiwasi kuwa Consultant huyu kafanya kazi kwa hisia na si kiutaalam kama mlivyotarajia; kama ndiyo njia iliyotumika pia kwa kina Lowassa na wenzake basi kuna uwezekano wengi wameonewa kwa kisingizio cha 'consultant'.

  Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.

  [​IMG]

  NB: Nilikuwa nirejee na maelezo marefu, lakini nimefahamishwa na mods kuwa kuna maelezo siku nyingi hapahapa JF; haya hapa

  Msimamo wetu na maelezo kidogo


  Habari yenyewe ni hii:

  Siri ya Kamati Kuu kufyeka mafisadi hii

  Na Mwandishi wetu (Nipashe)
  12th April 2011

  Maumivu makali yanatarajiwa kuwakabili baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye tuhuma za rushwa kama mapendekezo ya Kamati Kuu yaliyopitishwa na sasa yanasubiri baraka za Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) yatakubalika.

  Vyanzo vya ndani ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokaa Jumamosi iliyopita na kuona sekretarieti ikivunjwa, vinasema kwamba ripoti ya Kikosi Kazi kilichoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kutoa hotuba juu ya haja ya chama hicho kujivua gamba ambayo aliitioa mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya CCM Februari mwaka huu, inabainisha wazi kuwa tuhuma dhidi ya chama hicho kukumbatia wala rushwa zimewagharimu.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Kikosi Kazi hicho ambacho ni watu wanaoelezwa kuifahamu vizuri CCM na wakiwa wametakiwa kutafiti sababu ambazo zinakifanya chama hicho kikongwe kuwa katika hali mbaya kama kilivyo sasa, wanataja bila kutafuna maneno kwamba maamuzi juu ya kuwang’oa wenye tuhuma za ukiukaji wa maadili ndani ya chama ni lazima yafanyike sasa.

  “Utafiti umebaini kwamba suala la rushwa limekwisha kuwa ni mzigo mkubwa kwa chama chetu. Pamoja na juhudi kubwa ambazo serikali ya CCM imezifanya katika kupambana na rushwa nchini ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mpya dhidi ya rushwa; kuunda upya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa; na kutunga sheria ya udhibiti matumizi ya fedha katika uchagzui; bado wananchi wengi wanainyooshea vidole CCM kwa kuishutumu kwamba inakumbatia wala rushwa,” imesema sehemu ya ripoti hiyo na CC kukomelea msumari kwa kusema kwamba:

  “Tunataka kufanya mageuzi yatakayotuondoa katika muonekano huo, ili tuonekane kuwa ni chama kinachopambana na rushwa kwa vitendo.”

  Jopo la watafiti pia limeweka wazi kuhusu taswira ya CCM kuwa imeathiriwa sana na migogoro ya viongozi, hususan makundi yanayozozana ndani ya chama hicho.

  Wataalam hao pia wamesema CCM imeathiriwa na tuhuma za ufisadi, kwa kuwa ni chama kinachokumbatia mafisadi; udhaifu wa vikao vya maamuzi kutofanyika; kujipenyeza kwa kasi kwa wafanyabiashara wasio waaminifu na adilifu katika vikao vya chama; baadhi ya viongozi kujilimbilizia vyeo; CCM kushindwa kusimamia serikali kiasi cha kuiacha kuingia katika mikataba mibovu isiyokuwa na maslahi kwa taifa; kufifia kwa utamaduni wa kuwajibishana; kupotea kwa sifa ya chama kuwa cha wanyonge.

  Ili kutibu maradhi hayo, Kamati Kuu imeadhamiria kuwa: “Kwa hiyo, tunawajibika kufanya mageuzi ambayo yataonyesha kwa vitendo kuwa CCM bado ni chama kinachojali maslahi ya wanyonge; na kwamba CCM si chama kinachokumbatia mafisadi wala walarushwa.”

  Suala la ukoloni mamboleo ambao uimetajwa kama utandawazi pia umeelezwa kuwa umeathiri sana CCM kwa kuwa kwa nguvu ya mawasiliano ya kompyuta kama simu za mkononi, intaneti, blogs, twitters, facebook na you tube, vimechafua sana CCM ndani na nje ya nchi.

  Katika ripoti hiyo, kwa mfano mtandao wa Jamii Forum unatajwa kuwa unamilikiwa na Chadema na kwamba umetumiwa sana kuichafua CCM ndani na nje ya nchi.

  Kadhalika, CC imeelezwa kwamba fedha nyingi kutoka nje ya nchi zimekuwa zikiingizwa nchini kusaidia harakati ya kuiondoa madarakani CCM kama ilivyo kwa vyama vingine vikongwe barani Afrika, na kwamba fedha hizo zinatolewa kwa vyama vya siasa na hata kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, hakuna chama wala chombo cha habari mahususi vimetajwa.

  Kamati imedhamiria kuwa CCM nayo ifanye bidii kutumia fursa hizo za mawasiliano kama vile kuanzisha vyombo vyake ambavyo vitapambana na hasimu wao kama Jamii Forum.

  Wataalam pia wamezungumzia hatari ya CCM kuchukiwa na kundi la vijana, ikisema kwamba ndani ya vyuo vya elimu ya juu vijana wengi wamejiunga na vyama vya upinzani na kuwapa wakati mgumu wale wanaoshabikia CCM; kwa hiyo juhudi sasa zinatakiwa kuelekezwa kuwavuta vijana zaidi katika chama hicho.

  Hali ngumu ya maisha imetajwa kama moja ya sababu za kuchukiwa kwa CCM, na chama kimetaka juhudi zaidi zielekezwe kutatua ugumu wa maisha ili kauli mbiu ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania’ inafanikiwe.

  Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 yametajwa kama kuwika kwa jogoo anayeamsha watu, kwa sababu ushindi wa CCM kwa maana ya idadi ya kura za urais na hata viti vya ubunge vimepungua sana ikilinganishwa na mwaka 2005, huku vyama vya upinzani vikizidi kujiimarisha na kujongezea ushindi.

  Ili kukabiliana na mwelekeo huo, CCM sasa imedhamiria kubuni mikakati ya kuwa karibu na makundi mbalimbali ya kijamii, kama wafanyakazi, washirika, wanafunzi, ambao kwa sasa wako nje ya jumuiya tatu za Chama, yaani UVCCM, UWT na Wazazi.

  CCM imedhamiria kuwa hata muundo wake ni tatizo na kwa maana hiyo mageuzi ya muundo wa chama ni muhimu kwa sasa; miongoni mwake ni kuachana na ngazi ya chama kata na mkoa; kuanzisha kuchagua Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wilaya na kuachana na nafasi ya mkoa, kupunguza wajumbe wa kwenye kapu ambao ni 85; kuachana na utaratibu wa viongozi wastaafu kuwa wajumbe wa vikao vya kudumu vya chama kwa kuwa ni kuwasumbua na badala yake kuanzishwa kamati ya viongozi wastaafu watakaotoa ushauri wa mambo nyeti ya kitaifa yatakapohitajika.

  Mengine ni kuchaguliwa kwa makatibu wa mikoa na wilaya katika ngazi ya NEC ya maeneo yao; kuajiria kwa ujuzi na weledi, kuanzisha kamati ya ajira kuepusha upendeleo; kuanza utaratibu wa kupata maoni ya wanachama kwa kila ngazi walau kwa siku moja kwa mwezi.

  Chama hicho pia kimejielekeza katika kujikomboa kiuchumi kwa kupendekeza harakati za kutafuta fedha na si kusubiri wakati wa uchaguzi, harambee za kuchangia chama ziwe endelevu na zikipatikana fedha ziwekezwe.

  Kimepania kuzungumza na wapangaji wake kwa nia ya kuongeza pango; kuwekeza katika viwanja vyake; kutafuta wabia, kutafuta hati pale ambako hakuna na kuuza baadhi ya viwanja vya michezo ili kupata fedha za kiwekeza kwenye faida zaidi.

  Kadhalika, chama kinataka kuimarisha mfumo wa uwekaji wa kumbukumbu za mapato na matumizi, kustaafisha waliofikia umri wa kustaafu.

  Wataalam pia wamegusia mambo ya uchaguzi na sasa Kamati Kuu inapendekeza kwa NEC chaguzi zote za chama sasa zifanyike mwaka mmoja kuliko kuwa na mlolongo wa chaguzi kwa miaka minne, kwani kila uchaguzi huzaa majeruhi wanaohasimiana.

  Kuhusu jumuiya za chama, UVCCM imepewa changamoto ya kuvutia vijana zaidi, UWT kuendelea kuwaunganisha wanawake, lakini imeonekana kuwa Wazazi inazidi kukosa mshiko na kwa maana hiyo inapendekezwa ifutwe.

  Sababu kubwa ni kwamba wanachama wake pia wako UVCCM, UWT na CCM kwenyewe, lakini pia kazi yake ya kuendeleza shule nayo imepitwa na wakati kwa sababu ifikapo mwaka 2015 elimu ya lazima kwa kila Mtanzania itakuwa ni ya sekondari na baada ya mfumuko wa shule za kata shule zake hazitakuwa na nguvu tena.

  MBIO ZA URAIS

  MBIO za urais wa mwaka 2015 zimetajwa kuwa mwiba mkali dhidi ya mshikamano wa CCM na sasa Kamati Kuu ya CCM inakusudia kuwasilisha kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) pendekezo la kutafutwa kwa utaratibu wa kumpata mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.

  Uamuzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa matokeo ya utafiti wa Kikosi Kazi kilichopewa majukumu ya kuchunguza sababu za CCM kupoteza umaarufu katika siku za hivi karibuni na hatua zinazostahili kuchukuliwa kudhibiti hali hiyo.

  Kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya CCM, utaratibu huo unapekezwa katika ripoti ya Kamati Kuu kwenye ajenda ya Hoja na Haja ya Kufanya Mageuzi Ndani ya Chama Cha Mapinduzi, kipengele kilichopea jina la “kanuni za uchaguzi za chama na mbio za urais katika uchagzuzi wa 2015.”

  Kamati Kuu imethibitisha kwamba mbio za urais wa mwaka 2015 ni miongoni mwa mambo ambayo yanakiumiza sana chama ndani kwa ndani, hali inayohitaji ufumbuzi wa haraka.

  Kamati Kuu imebaini kwamba makundi ya vinara wanaowania urais yamewagawa wanachama na kuathiri mshikamano ndani ya chama kwa kiwango kikubwa.

  “Imeonekana kuwa kiini cha tatizo hili ni utaratibu wa kupata wagombea wa CCM ambao unatumika hivi sasa, kulingana na Kanuni za Uchaguzi wa kuingia katika vyombo vya Dola zilizopo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ambao NIPASHE imeiona.

  Kamati Kuu imesema kwamba katika kipindi cha uongozi kilichopita, NEC iliunda kamati ya kutafuta utaratibu bora wa kupata viongozi wa dola wanaoingia kwa tiketi ya CCM.

  Ililezwa kwamba kamati hiyo iliongozwa na Dk. Mohamed Gharib Bilal, sasa Makamu wa Rais, na kwa maana hiyo NEC inashauriwa iunde kamati nyingine kama hiyo.

  Kamati hiyo kwa mujibu wa Kamati Kuu itafanya utafiti na kuwasilisha mapendekezo yake juu ya utaratibu bora zaidi wa kumpata mgombea urais kupitia CCM.

  Utaratibu unakusudiwa utumike mwaka 2015 na ulenge kuzuia matumizi makubwa ya fedha kwa nia ya kununua kura za wajumbe wa vikao vya uchujaji na vya uteuzi wa mwisho katika mchakato ndani ya CCM.
   

  Attached Files:

 2. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao nao wameishiwa sera. Hiyo JF nani anaifahamu huko mitaani kwetu, na bado wanaichukia CCM!!!!!!!!!!
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  inferiority complex....unaogopa kivili chako mwenyewe
  waanzishe mafisadi forum
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du! bongo bana, na I am very sure wanaosema hivi watakuwa wameijua JF mwaka jana, Kwa kifupi kama taifa "WE HAVE A PROBLEM, BIG PROBLEM" sasa kama maconsultant wenyewe ndiyo hawa unategemea nini tunapoingia mikataba mikubwa mikubwa ya serikali.......
   
 5. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  duuu hii kali sasa ngoma inogile
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  "Kamati imedhamiria kuwa CCM nayo ifanye bidii kutumia fursa hizo za mawasiliano kama vile kuanzisha vyombo vyake ambavyo vitapambana na hasimu wao kama Jamii Forum."

  Niliwahi kuwahoji humu kipindi kile cha uchaguzi watu waliokuwa wanalalama lalama humu kwamba JF ni ya CDM watuonyeshe forum ya CCM. All in all CCM imezeeka na I betcha, hawawezi hata siku moja kuendesha a thing similar to just 1% of JF. With them hii itakuwa dili na multi-million shillings will be involved. Isipofanikiwa watabaki kunyosheana vidole. Level yao nik blogging period.

  Na toka lini JF akawa hasimu wa CCM? Ina maana akina Kibunango, WJM, Kasheshe, Kada, Nape, January, Mbunge pia ni mahasimu wa CCM? Unless nimetipiwa kidogo juu ya nini maana ya neno hasimu.
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  hivi uhuru na mzalendo bado zinachapishwa?
   
 8. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Nilicheka tu baada ya kuiona hii habari lakini nikaja kuwaza sana; hivi CCM wanadanganywa kiasi hiki? Hawa 'consultants' wanatumia vigezo gani kuwasilisha maoni yao kwa viongozi wetu wa kitaifa?

  CHADEMA wanapewa credit nyingi ambazo hata mtu huwezi kuamini kama wanapewa; ni wazi CCM wanaiogopa CHADEMA sasa kwa kuamini ina hela nyingi sana mpaka inaweza kufadhili vitu vingi tu.

  Twitter, FaceBook etc nazo naona zinawatisha CCM kwa ushauri huu wa 'consultant'; huu ni upotoshaji wa wazi. Nilikuwa napuuzia lakini nahisi kuna tatizo ambalo linatakiwa kuwa addressed kwa viongozi wa kiserikali na hata vyama, hivi wao ni vilaza kuambiwa uwongo wa mchana na kuuamini?

  Nina wasiwasi 'consultants' hawa wanafanya kazi kwa hisia tu
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yeah bado yapo sokoni.

  Siamini bibi yangu kule Matombo kama anajua kuna blog na JF lakini bado anaichukia CCM.
   
 10. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  bado na uhuru fm wanayo...tatizo ni utilisation ya hivyo vyombo
   
 11. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Umemsahau Kigwangalla pia mkuu.

  Something is very wrong somewhere. CCM wakija kushtuka wanaweza kuwa wamechelewa. Ushauri mwingine unaweza kudhani umetolewa na Malaria Sugu (as a joke).

  Ukiikosoa CCM au CHADEMA unakuwa hasimu wake, jana napata sms nyingi tu toka kwa watu wa CDM ati tumewapa air time kubwa CCM kwenye vikao vyao, sasa nao soon wataambiwa kwenye NEC yao kuwa JF imenunuliwa na CCM?

  Kazi ipo kubwa, mpaka watu waelewe maana ya Citizenry Journalism basi tutakuwa tushabatizwa kila aina ya majina, mahasimu, wanafiki, waongo n.k
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  At the end of the day, ccm has to realise it's just a political party. It's bound to be challenged and its performance is measured by the public! So if they cant perform, while the country stumbles from one crisis to another, it is logical to lose support. This is the basics of multi-party democracy.
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huu ni UJINGA wa hali ya juu. Yaani mie kuwa JF tayari nimekuwa MALI ya Chadema?

  Mtu mwenyewe hata Kadi ya chama chochote sina na leo unaambiwa "umemilikiwa na Chadema."

  JF ni watu na wala siyo Maxence Melo au sijui nani. Wale ni wadhamini wetu tu.

  Ukitaka kuamini hilo, jiulize kitu kimoja: Kuna forum nyingi sana za Watanzania na Blog kibao ila kwa nini JF ndiyo inatesa namna hiyo? Ni kwa makala za wadhamini wa JF au MEMBERS wa JF?

  Michuzi Blog ingeliweza kuwa kwenye nafasi ya JF leo hii ila kutokana na Michuzi kubania thread za watu na comments za watu, Michuzi blog imebakia kuwa kama kitawi cha CCM na Bwawa la Maini. Blog nyingine ya wauza nywele nayo iko juu na sababu ni kuwa wanafanya vizuri sana katika Issue ambazo wameamua wazifanye. Hata Ze-Utamu na yeye alifanikiwa saaana kwa sababu HAKUBANIA habari za watu.

  JF imekuwa wazi kwa watu na kuachia habari ziandikwe na kuachwa hata kama ni SIRI NZITO ya Serikali. Zimeondoloewa tu zile ambazo au zinatukana au zina majungu. Kuachia habari huku zisomwe na watu wote wanaoingia JF ndiyo kumeifanya JF iwe hapo ilipo na kuwapa SIFA za UJASIRI wadhamini wa JF.

  Ila leo mtu akija na kusema JF ni mali ya Chadema ni sawa na kusifia Jiko fulani linapika vizuri na LIMEDHAMINIWA na fulani na unasahau kuwa WAPISHI wake wakihama, jiko litabako historia. Wanataka kusema mtu kama FMes ni Chadema? Kibunango ni Chadema? Malaria Sugu, Mwiba, Junius, Kishonga, Ndalu, Tumaini, Ngongo, X-Pasters na wengine wengi wanaoshinda hapa wakimtukana Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla na wao wamekuwa ni Chadema?

  Hebu mwangalia Waberoya na makala zake, unataka kusema huyo ni Chadema?

  Kweli MFA MAJI, HAACHI KUTAPATAPA.......... Atashika hata kitoto cha Ndege/bata ili asizame.
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hapo kweli huyo consultant kawadanganya, kuna sehemu hata mitandao ya simu ni shida kupatikana lakini watu wanaichukia ccm. Humu mbona wapo members wengi tu wa ccm?
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bora wakazane kuitumia Clouds FM maana inamashabiki wengi huko wanaweza wakakiimarisha chama.

  Hiyo Uhuru FM full mipasho nani atasikiliza hata Makamba mwenyewe hasikilizi.
   
 16. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  You can say that again Mkuu! These days hata maongezi ya kawaida kabisa kuna watu hawataki uwe neutral either with us or against us. Independent thinking haiwavutii wengi.
   
 17. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  Eti watauza viwanja vya michezo! Viwanja vyote ni vya umma wanavihodhi kwa nguvu tu. Wanaogopa kwamba vitarudishwa kwa umma mara serikali isiyo ya CCM itakapoingia madarakani 2015.

  Na hii ni mbinu ya kufisadi mabilioni ya serikali toka kwenye halmashauri zetu.

   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  tbc1...
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Viwanja vipi tena hivyo??........isiwe CCM KIRUMBA na vingine vya namna ile..!!!
   
 20. L

  LAT JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  duh ... kashaga na kupen'ge wameshafanya kazi yao
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...