Leo nimekuwa msomaji zaidi, nimegundua watu wengi mnaifahamu JF. Zaidi ya nilivyodhania mwanzo.
Inasikitisha members wengine hapa pamoja na kuwa wao ndio wanaandika hoja zao wanataka iaminike kuwa waendeshaji ndio wanaopanga nini kijadiliwe; ni uzushi usio na ukweli.
Hivi hawa hawa wana JF wangekuwa ni mali ya CDM, jana na juzi wangehangaika kufuatilia kinachojiri Dodoma kwenye shughuli ya CCM? Si wangehakikisha hakisikiki kabisa? Naamini kuwa wengi ni wazalendo, walikuwa wanataka kujua hatma ya CCM, hatma ya taifa (kwa kuwa ndicho chama tawala).
Mshauri huyu wa CCM alifanya kazi yake, kwa kutafuta ujira wake. Wasiwasi wangu ni kuwa kama mambo yote kafanya kwa mtindo huu basi viongozi wa juu wa CCM wamenyweshwa 'sumu' na kuna watu watakuwa wameonewa sana, msishangae baadae kukaibuka mvurugano mzito ndani ya CCM ambao kuzimika unaweza kuwa kazi kubwa na kupelekea kumegeka kwa chama.
Yangu mie macho
Point noted,JK ama Makamba wameshazuiliwa kujiunga JF kama Slaa na wengineo?Always the blame lies with somebody else.
CCM wanatakiwa kuweka mikakati thabiti ya kuweza kushinda 2015. Kitu kimoja ambacho waelewe ni kuwa, siku zinavyozidi kwenda, wao ndio wanazidi kupoteza wapiga kura. Sababu moja ni kwamba, vijana walio na miaka 13 mpaka 17, ambao walikuwa hawajafikia umri wa kupiga kura kwenye uchaguzi uliopita, watakuwa wamefikia huo umri. Na hawa vijana wengi wako kwenye households ambazo zimeichoka CCM. Kila kukicha wanawasikia wazazi wao wakilalamika kuhusu maisha magumu, ufisadi, mabomu, umeme..nk, vyote vilivyosababishwa na CCM.
Kwa hiyo ni dhahiri, wakati wao wa kupiga kura ukifika, hawataipigia CCM, na hawa vijana kwenye hii age bracket ni wengi. Wao wanataka kubaki kuilaumu JF. Lakini hata kwa mfano ni ya Chadema, so what? Ni sawa na kulalamika kuwa Barcelona wana Messi! Sasa asicheze, au wamevunja sheria?
Natamani waanza hata kesho, yani tutawafuata na kuwanyuka hukohuko!inferiority complex....unaogopa kivili chako mwenyewe
waanzishe mafisadi forum
Kuuza VIWANJA vya Michezo?
Lini hiyo wanataka kufanya? Hiyo nayo itabidi sisi wa Tabora tugome maana tulijenga wote.
Hapa itabidi Wanaharakati na Chadema wapeleke kesi mahakamani na kuwaambia watu wowote wanaotaka kununua viwanja kuwa kuna siku watanyang'anywa maana ni MALI ya Wananchi na CCM imefanya kutumia mabavu kama Gbagbo na kujichukulia Nchi na viwanja vyake.
Hili inabidi kulifungulia thread yake PEKE yake kama kweli CCM wanataka kufanya upuuzi huo.....
Hata hao consultants wanao tumiwa na ccm mimi nawatilia shaka..
Na ndi hao mara nyingi wanategemewa kusukuma hili gurudumu letu la maendeleo
Magazeti mengi yana longo longo na habari za kuwafeva baadhi ya watu kutokana na matakwa yao, ndio maana jamii yote sasa hivi inahamia kwenye free media na journalism huku hakuna longo longo ,na kwanza vigazeti vyao vingi wanachukua taarifa kutoka hapa JF.
JF is everything
Huu ni UJINGA wa hali ya juu. Yaani mie kuwa JF tayari nimekuwa MALI ya Chadema?
Mtu mwenyewe hata Kadi ya chama chochote sina na leo unaambiwa "umemilikiwa na Chadema."
JF ni watu na wala siyo Maxence Melo au sijui nani. Wale ni wadhamini wetu tu.
Ukitaka kuamini hilo, jiulize kitu kimoja: Kuna forum nyingi sana za Watanzania na Blog kibao ila kwa nini JF ndiyo inatesa namna hiyo? Ni kwa makala za wadhamini wa JF au MEMBERS wa JF?
Michuzi Blog ingeliweza kuwa kwenye nafasi ya JF leo hii ila kutokana na Michuzi kubania thread za watu na comments za watu, Michuzi blog imebakia kuwa kama kitawi cha CCM na Bwawa la Maini. Blog nyingine ya wauza nywele nayo iko juu na sababu ni kuwa wanafanya vizuri sana katika Issue ambazo wameamua wazifanye. Hata Ze-Utamu na yeye alifanikiwa saaana kwa sababu HAKUBANIA habari za watu.
JF imekuwa wazi kwa watu na kuachia habari ziandikwe na kuachwa hata kama ni SIRI NZITO ya Serikali. Zimeondoloewa tu zile ambazo au zinatukana au zina majungu. Kuachia habari huku zisomwe na watu wote wanaoingia JF ndiyo kumeifanya JF iwe hapo ilipo na kuwapa SIFA za UJASIRI wadhamini wa JF.
Ila leo mtu akija na kusema JF ni mali ya Chadema ni sawa na kusifia Jiko fulani linapika vizuri na LIMEDHAMINIWA na fulani na unasahau kuwa WAPISHI wake wakihama, jiko litabako historia. Wanataka kusema mtu kama FMes ni Chadema? Kibunango ni Chadema? Malaria Sugu, Mwiba, Junius, Kishonga, Ndalu, Tumaini, Ngongo, X-Pasters na wengine wengi wanaoshinda hapa wakimtukana Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla na wao wamekuwa ni Chadema?
Hebu mwangalia Waberoya na makala zake, unataka kusema huyo ni Chadema?
Kweli MFA MAJI, HAACHI KUTAPATAPA.......... Atashika hata kitoto cha Ndege/bata ili asizame.
Mkuu,
Nilicheka tu baada ya kuiona hii habari lakini nikaja kuwaza sana; hivi CCM wanadanganywa kiasi hiki? Hawa 'consultants' wanatumia vigezo gani kuwasilisha maoni yao kwa viongozi wetu wa kitaifa?
CHADEMA wanapewa credit nyingi ambazo hata mtu huwezi kuamini kama wanapewa; ni wazi CCM wanaiogopa CHADEMA sasa kwa kuamini ina hela nyingi sana mpaka inaweza kufadhili vitu vingi tu.
Twitter, FaceBook etc nazo naona zinawatisha CCM kwa ushauri huu wa 'consultant'; huu ni upotoshaji wa wazi. Nilikuwa napuuzia lakini nahisi kuna tatizo ambalo linatakiwa kuwa addressed kwa viongozi wa kiserikali na hata vyama, hivi wao ni vilaza kuambiwa uwongo wa mchana na kuuamini?
Nina wasiwasi 'consultants' hawa wanafanya kazi kwa hisia tu
mkuu ni sawa kabisas!
Labda point nyingine ni kutokana na viongozi waandamizi wa CDM mara kwa mara kujitokeza hapa Jamvini kama Zitto, Regia Mtea,Dr. Slaa na wengineo.
Walichofanya CDM ni kutumia opportunity iliyojitokeza kuweza kupata mawazo ya wasomi ambao wengi wao hukutanishwa mahali hapa.
Ingekuwa ni vyema kama vyama vingine basi vikatumia nafasi hii, ikiwezekana kwa viongozi wao waandamizi kujibu au kutolea ufafanuzi wa baadhi ya hoja kama wanavyofanya CDM.
nafikiri CCM inabidi wakae chini na wajiulize, watafute busara ya kutafuta namna ya kujipenyeza kwenye jamii bila kudharau. Hebu pata picha kama Makamba au Chiligati angekuwa anajibu hoja humu ndani, sidhani wangefika hapo walipofika.
Sisemi ni lazima wafanye hivyo, isipokuwa waache kufanya mambo mengi kisiri siri, hii ni demokrasia, na chama ni vizuri kikawajibika kwa wananchi kwa kutumia njia zozote zinazowezekana.
Inawezekana chuki wanayoipata hapa huenda siku moja ikahamia CDM, CUF au NCCR. Watu kamwe hawataacha kuikosa serikali na vyombo vyake.
CCM imeipa CHADEMA heshima isiyostahili. Sidhani ni kweli CDM wamepata nguvu kiasi cha kushika maeneo yote yanayoonekana yana upinzani.
Angalizo pia kwa CDM, kwamba wasibweteke na kila kinachoendelea hapa JF, wengi ni washabiki tu ambao kesho wanaweza kushabikia upande mwingine.
Pia heshima kwa JF kutoka kwa CCM naona pia imezidi mno. Sidhani kundi la watu hawa humu jamvini likawa na athari kwa nchi nzima kwa maana ya kuiporomosha heshima ya CCM. Wapiga kura wengi wako vijijini ambao hawajui hata maana ya Internet. Na pia ni sehemu ndogo sana ya Watanzania wenye uwezo wa kupata huduma ya internet achilia mbali kupenda siasa. Hivyo basi ni kuitwisha mzigo JF na wamiliki wake ambao hauna mantiki yoyote.