Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Huyo mwandishi wa Nipashe naye ana matatizo kwenye kupambanua mambo! angeweza kuelezea wazi experience yake ya hapa JF maana naye ana access.

Duh huyo Consultant amekula hela za bure! wangenipa hiyo tenda.
 
kwanza huyo consultant wao ni haramia...........wameshindwa kuchambua mambo na namna ya kuwasaidia wananchi then wanaanza kupayuka ovyo........hawakazwi kujiunga waje na tupambana kwa hoja za maana na sio kulilia uvunguni
 
Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.

nasubiria urejee mkuu, ni dhahiri ccm bado mtete pamoja kuwa inakaribia nusu karne. Yote haya yanasababishwa na kutowapa nafasi watu wenye fikra mbadala kwa wakati husika. Na kuendelea kuendeshwa na taarifa za 'kiintelijensia' kutoka kwa ma-consultant wao!
 
Nimesoma habari hii chini nikabaki kujiuliza; "Kama huyu ndiye Consultant wa Chama Tawala; hivi washauri wa serikali wanatoa ushauri wa namna hii pia?"

Napata wasiwasi kuwa Consultant huyu kafanya kazi kwa hisia na si kiutaalam kama mlivyotarajia; kama ndiyo njia iliyotumika pia kwa kina Lowassa na wenzake basi kuna uwezekano wengi wameonewa kwa kisingizio cha 'consultant' (Kinana!)

Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.

Hapo ndipo patamu,Karibu Mkuu,sema usikike,Tunasubiri tamko lako
 
tatizo kubwa la CCM ni kwamba watu wanaowaona wana "upeo" mkubwa wakukiongoza na kukisaidia chama kurudisha hadhi yake hawana mvuto kwa wananchi wakawaida kwasababu wengi wao hawawajui wananchi na matatizo yao, wanatumia nadharia zaidi ya hali halisi kujaribu kutatua matatizo ya wananchi..
 
mbona ccm wana radio uhuru, radio tz,tbc fm, magazeti ya uhuru, mzalendo television tbc1 pia ni ya kwao. Mimi nadhani hao ma-consultants wanatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Tatizo sio media, tatizo ni kwamba ccm imeshindwa kutatua matatizo na umasikini wa waTZ kwa miaka 50 tangu uhuru. CCM wasitafute mchawi, unatoa makamba mkubwa unaweka makamba mdogo.
 
mbona ccm wana radio uhuru, radio tz,tbc fm, magazeti ya uhuru, mzalendo television tbc1 pia ni ya kwao. Mimi nadhani hao ma-consultants wanatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Tatizo sio media, tatizo ni kwamba ccm imeshindwa kutatua matatizo na umasikini wa waTZ kwa miaka 50 tangu uhuru. CCM wasitafute mchawi, unatoa makamba mkubwa unaweka makamba mdogo.

umesahau redio imani.
 
ama kweli mswahili ni mswahili tu! juzi juzi alikuwa rombo akasema mramba ni mkali kama panga la zamani, akaenda monduli akasema hajaona mwanaume kama EL. Leo anasema lazima tujivue gamba lile lile alilolisifia.
 
Mimi binafsi nilivutiwa na JF bila kuwa na kadi ya chama chochote cha kisiasa hapa duniani!

JF is a platform wherereby people air their divergent perspectives across issues/agenda in order to share views. Ni mtandao huru, ni vichwa vinavyofikiri. Hukosoa na kujadili pale penye tatizo. Hao wanaofikiri kuwa JF ni ya Chadema ni kwa sababu hawakufanya utafiti wa kutosha au walitaka ku-justify malipo yao ya consultation! Wangewashauri CCM watatue kero za wananchi na kutimiza ahadi zao za maisha bora kwa kila Mtz waone kama JF haijawapongeza! Wameona mtaji wa Uhuru/Mzalendo/Habari Leo/Rai/Tambwe Hiza etc haulipi???

Consultants aina ya akina Kinana ndio wanaompotosha Mkiti wao na kwa kuwa ndio Rais wetu wote tunadidimizwa kwa ajili ya akili za watu wachache wenye ubongo uliomea fungus. Washauri hao wawahi Loliondo kupata "single dose" kwa babu!
 
Yaani hiyo ripoti yao imeongea mambo mengi lakini tatizo lenyewe wameliweka mbaaaali wakitangulia na kumtafuta mchawi eti vijana eti JF. Hatimaye baadaye ndio wanataja tatizo, lakini kwa kupita tu. Hili hapa;

Hali ngumu ya maisha imetajwa kama moja ya sababu za kuchukiwa kwa CCM, na chama kimetaka juhudi zaidi zielekezwe kutatua ugumu wa maisha ili kauli mbiu ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania' inafanikiwe.

Halafu sasa wakapendekeza ufumbuzi;

Ili kukabiliana na mwelekeo huo, CCM sasa imedhamiria kubuni mikakati ya kuwa karibu na makundi mbalimbali ya kijamii, kama wafanyakazi, washirika, wanafunzi, ambao kwa sasa wako nje ya jumuiya tatu za Chama, yaani UVCCM, UWT na Wazazi.

Je ni sahihi kwamba ukifanya hivyo utakuwa umetatua tatizo?
 
Ni uongo wenye kutu kusema JF inafadhiliwa na CDM na wanaCDM ndo wanakusanyika kwa wingi humu,, natangaza maslahi, mm nimwanaccm hai na siwezi kuhofia hili kwani hapa zinatundikwa mada za msingi na zenye kujenga Tanzania hata kama zinaibomoa au kuijenga CCM ama CDM. Tatizo letu kubwa wana CCM, baada ya kushindanisha hoja tunabaki kulalamika kuwa CDM wametawala huku.

Hata hivyo ninafurahi kuwa kwa jinsi JF ilivyopatiwa shavu la kutosha na hawa ma-'consultant' wetu labda JF itazidi kumea na kuwafikia hata wa vijijini (kama makampuni ya simu yanavyosambaa) na kuwawezesha kutoa mawazo yao bila uoga wa aina yoyote
 
People's Power! These two words isolated are very familiar to us. But used together it's something different all together! It's people themselves, if you know what I'm talking about. People!They always have their way when they want it. There are seldom no "rules" against them. Not any government, not any court of law, not any prison can hold them back. Remember the tower of Babylon? It took GOD ALMIGHTY Himself to confuse their tongues in order to stop them (If you know the story). He knew them, they are simply unstoppable when they stand together as one. Whoever is complaining about CDM, about Dr Slaa, about JF, about anything...I'm not surprised. It's just not very simple to come to term with it. It's still a new idea to them or at least a new thing here in our dear Tanzania. No body saw it coming in America,Tunisia,Egypt,Yemen,Kenya etc.It's like this:

  • It has got no colour
  • It has got no tribe
  • It has got no religion
  • It has got no age
You may try to paint it and name it what you want,but it is not! It is simply PEOPLE who go out there for their own. It's EITHER THEIR WAY OR YOUR HIGHWAY! Huwezi kuzuia maji kwa mikono. Wapi ingefanyika rally ya kuwakusanya hao cyber army waingie JF? On the contrary, ni wazi kuwa watu walioishiwa kisiasa wanaweza kufanya hivyo wakitaka,hasa kwa kutumia vijisentui walivyo navyo. Kama wanaweza kuwapeleka watoto wa shule PHYSICALLY kwenda kujadili muswada wa katiba,watashindwa vipi VIRTUALY .
Mkuu Max, maoni kama haya si ya kubeza kwani ndio tafsiri halisi ya watazamaji wanaoingalia JF kwa nje.

Kwa mfano; katika kipindi cha miezi 6 hivi kuanzia kampeni hadi kuelekea uchaguzi wa 2010, 'cyber army' wa CDM walifurika sana hapa hadi ikaonekana kama vile CDM wanapewa 'air-time' kubwa sana hapa JF; sina uhakika kama ni by accident or design.
Nakumbuka vilevile kipindi cha 2006 - 08, wakati JK akiwa kwenye kilele chake, watu wengi walifikia kusema eti JF inamilikiwa na uliokuwa 'MTANDAO' wa ccm.

Tumieni maoni kama haya ama Changamoto na ma-MODs wajaribu kutoonyesha ushabiki katika mijadala. Pengine si vibaya; kutegemea na agenda husika, JF wakatangaza msimamo wao kuunga mkono upande mmojawapa kama tunavyoona katika Media House nyingine.
 
Hapo kweli huyo consultant kawadanganya, kuna sehemu hata mitandao ya simu ni shida kupatikana lakini watu wanaichukia ccm. Humu mbona wapo members wengi tu wa ccm?

hao ndo maconsultants wenyewe!
siunaona wanavyokuja na threads zao"Ni wakati na CDM wamondoe DR. Slaa" nk
 
ahaaaaaaaaaaaa nani mkakwambia ccm wamo?wananja waliopo eti wanaogopa kuja kuenguliwa pindi watakapotaka uongozi,usidanganyike mtanzania wewe popote kiongozi bora anapatikana vijana 2amke kuwaondoa hawa wachache wanaolisishana madalaka na kuwafanya watanzania makapu ya mapaki
 
Jamani, ccm kweli imefikia itimisho, jk katoa nyoka kaweka nyoka (makamba na mtoto) bila kukumbuka mtoto wa nyoka ni nyoka, ndugu zangu hasiye ijua ccm atasema eti makamba amejihuzuru. Sasa uzembe kama huu utasingizia CHADEMA
 
Hahahahaha jamani mbavu zangu! Hivi kama kuanzisha waacheni waanzishe. Ila wangekuwa na busara wangejiuliza kwanini vyombo vyao vya chama havisikilizwi ama kushabikiwa.

Mtu akinunua magazeti yale yanayotoka Jumatano kama RaiMwema au MwanaHalisi anaonekana mjanja na si atayeshika au kusoma (achilia mbali kununua) magazeti yao Uhuru na Mzalendo.

Au kufungulia Uhuru Radio mweee....waacheni waendeleee kufungua tu wawape ajira wasaka tonge
 
Mtoto aliyezoea kubebwa bebwa hulilia kila mgongo upitao mbele yake, "nibebe, nibebe". Na watu waliozoea kumdekeza mtoto huyo huchuchumaa kwa haraka na kumweka kwenye mbeleko. Mtoto hunyamaza na kujisikia kafika peponi wakati mwingine akiwazodoa wengine na akiachwa muda mrefu mgongoni husinzia kwa raha mustarehe. Ikitokea siku akaja mtu ambaye mtoto anataka abebwe naye naye mtu yule akakataa mtoto hujiliza kwa sauti kama kaona mizimu ya watu wa kale, atajiangusha chini na machozi yanayosindikizwa na makamasi yakimdondoka kama maporomoko ya mto Rufiji na kuwapigia kelele nyumba nzima hadi majirani wanashtuka - lakini majirani wanajua "ni zake hizo".

Basi aweza tokea mtu na kusema "si uchuchumae umbebe jamani atulie?". Yule mtu akikataa basi mtu mwingine huweza kujitolea na kumwita mtoto "haya baba njoo, njamaza, njoo ni kubebe mtoto mzuri". Mtoto hukimbilia mgongo huo uliojitolea kama aliyeoneshwa peremendena kwa furaha huudandia kama utingo wa gari linalokwenda "Mbagala, huku nyumba mbele jalala" na huzungusha mikono shingoni na miguu pembeni akiitikisa tikisa hadi viatu kumtoka na kichwa hukilaza kwa utulivu huku dole gumba lake amelitundika mdomoni. Kabebwa.

CCM ni mtoto aliyezoea kubebwa; migongo ya kuibeba ni mingi:

TBC
Jeshi
TISS
Polisi
Watendaji serikalini
Wafanyabiashara wakubwa
n.k n.k

So..tunamsikia akilia "JF hainibebi, JF hainibebi..." Hivyo hoja inatolewa, tuwatengenezee jukwaa lao wenyewe na tuanza kwa pamoja kushangilia mambo yanayofanywa na CCM, tuimbe nyimbo za kutukuza uongozi wake, na tuwasifie kwa mabadiliko "makubwa". Tusipofanya hivyo.. atalia hadi tukome!! Na kama nimesoma vizuri hata kucha tutaparuriwa!!! HADI TUKUBALI KUMBEBA KWENYE MBELEKO YA JUKWAA HURU ZAIDI LA MAONI TANZANIA.

VIVA JAMII FORUMS!!
 
CCM wamo humu wengi sana tu.

Tatizo ni kwamba wamepigwa butwaa na ndio maana hawawezi kujenga hoja. Hawajawahi kuwa wapinzani,hawajawahi kuhojiwa kwa uwazi kama inavyofanyika hapa JF. Hawajui nini maana ya uwajibikaji kwa wananchi.. Sasa mnadhani watu wa aina hiyo watataka tujadili issue nyeti humu? Wakati wanajuwa wazi kuwa wanafanya utumbo ambao umelifikisha Taifa hapa tulipo? Sidhani kama watakubali kujipiga kitanzi.

Kwa mfano kashfa zote za ufisadi, hao consultants walitegemea wana CCM waje hapa na kupata sapoti ya wananchi ambao ni wasomaji na members humu? Ukweli ni kwamba hao wana CCM wakija humu na kujibu hoja za ufisadi, basi watajikuta wakitoa siri zaidi.Hilo ndiyo tatizo. Hakuna hoja itakayoweza kuzima ukweli.

Tunategemea mufanye mabadiliko ili muweze kupata hoja za kusimamia hapa JF, msipowachukulia hatua mafisadi,hakuna kitakachobadilika.

Msitegemee kabisa kuwa eti JF itasapoti ufisadi.... Uwe unafanywa na CCM ama CDM, no difference here.
 
Status
Not open for further replies.
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom