Mshangao: Imekuwaje Rais Ruto awe Rais wa kwanza kutoka Afrika kufanya ziara rasmi ya kiserikali nchini Marekani?

ezekeo

Member
Aug 27, 2022
63
158
Nimejikuta katika wakati mgumu wa kuiamini taarifa inayosema eti rais Ruto wa Kenya ndie rais wa kwanza kufanya ziara rasmi ya kiserikali nchini marekani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita.

Swali ni je Hawa Marais wengine kutoka afrika ambao kwa mamia walioitembelea marekani kwenye hicho kipindi Cha miaka 15 kabla ya hii ziara ya Ruto ni kwamba ziara zao hazikuwa zikitambulika na serikali ya wamarekani?

Kama jibu ni ndio, vipi kwa nchi zetu za kiafrika kama tuko na huo utaratibu wa kutozitambua ziara za Marais wa nchi nyingine ikiwemo marekani kuwa rais kutoka nchi ya kigeni(nje/ndani ya afrika) aitembelee nchi nyingine ya kiafrika na ziara yake isitambulike kama ziara rasmi yaani ionekane amezurura tu mpaka pale nchi husika ikijisikia ndipo iitangaze ziara husika kuwa ni rasmi?

Kwa idadi ya Marais kutoka afrika waliotembelea marekani tena wengine wakionekana ikulu ya marekani kabisa halafu Leo tuambiwe ziara zao hazikuwa rasmi huko ni kuwakosea heshima viongozi kutoka afrika na ni kuwagombanisha na wapiga kura wao.
 
Nimejikuta katika wakati mgumu wa kuiamini taarifa inayosema eti rais Ruto wa Kenya ndie rais wa kwanza kufanya ziara rasmi ya kiserikali nchini marekani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita.

Swali ni je Hawa Marais wengine kutoka afrika ambao kwa mamia walioitembelea marekani kwenye hicho kipindi Cha miaka 15 kabla ya hii ziara ya Ruto ni kwamba ziara zao hazikuwa zikitambulika na serikali ya wamarekani?

Kama jibu ni ndio, vipi kwa nchi zetu za kiafrika kama tuko na huo utaratibu wa kutozitambua ziara za Marais wa nchi nyingine ikiwemo marekani kuwa rais kutoka nchi ya kigeni(nje/ndani ya afrika) aitembelee nchi nyingine na ziara yake isitambulike kama ziara rasmi yaani ionekane amezurura tu mpaka pale nchi husika ikijisikia ndipo iitangaze ziara husika kuwa ni rasmi?

Kwa idadi ya Marais kutoka afrika waliotembelea marekani tena wengine wakionekana ikulu ya marekani kabisa halafu Leo tuambiwe ziara zao hazikuwa rasmi huko ni kuwakosea heshima viongozi kutoka afrika na ni kuwa honganisha na wapiga kura wao.
Ziara ni nyingi zinazofanywa na maRis kutoka Afrika kumbe wenzetu huwa wanazinaweka kwenye mafungu mafungu, na mimi nimeshangaa sana!

Nikutolee mfano wewe mwenyewe nyumbani kwako utembelewe na omba omba, apige hodi getini umfungulie umkaribishe hadi ndani halafu akuingizie mada zake za vizinga, halafu baadaye aje baba mkwe wako kuwatembelea na kisha baadaye kuondoka.

Hiyo mifano miwili, ukikaa siku mbili aje mtu kukuuliza: ... 'Nasikia juzi ulitembelewa na wageni'...

Cha kwanza kukumbuka akilini mwako nadhani atakuwa ni huyo mkweo na huyo omba omba ingawa naye alikiwa ni mgeni pia lakini hatakuja akilini mwako kwa sababu ugeni wake wewe haukuufurahia.

Wamarekani wanaweka mafungu ya uthamani wa viongozi wa Afrika kwa sababu wengi wao, ziara zao hazina manufaa kwa nchi zao ama kwa Marekani yenyewe, kwa hiyo wanaonekana ni vizurure na omba omba tu.

Tukija kwenye mada yako ni kwamba, Marekani imempa sifa kubwa na maalumu (title)bwana Ruto na pia kumwingiza kwenye rekodi ya 'Mwenzao' asiye mNATO kutokea maeneo ya Afrika na Caribean, ni ziara ya heshima sana.

Na Biden kaitoa orodha ya nchi za wabia wasio wanachama wa NATO na kuiweka hadharani.

Sababu kubwa ya Ruto kuwekwa kwenye orodha ya mwenzao ni kile kitendo chake cha kijasiri cha kupeleka Polisi wa 'F.F.U' kule nchini Haiti katikati ya machafuko kwenda kudhibiti yanayoendelea kisiwani humo.

Sababu nyingine za kumpamba Ruto na ziara yake, zimewekwa bayana na mkuu huyo wa USA.
 
Jifunze tofauti ya State Visit, Official Visit, Working Visit, Private Visit.
 
Nimejikuta katika wakati mgumu wa kuiamini taarifa inayosema eti rais Ruto wa Kenya ndie rais wa kwanza kufanya ziara rasmi ya kiserikali nchini marekani kwa kipindi Cha miaka 15 iliyopita.

Swali ni je Hawa Marais wengine kutoka afrika ambao kwa mamia walioitembelea marekani kwenye hicho kipindi Cha miaka 15 kabla ya hii ziara ya Ruto ni kwamba ziara zao hazikuwa zikitambulika na serikali ya wamarekani?

Kama jibu ni ndio, vipi kwa nchi zetu za kiafrika kama tuko na huo utaratibu wa kutozitambua ziara za Marais wa nchi nyingine ikiwemo marekani kuwa rais kutoka nchi ya kigeni(nje/ndani ya afrika) aitembelee nchi nyingine na ziara yake isitambulike kama ziara rasmi yaani ionekane amezurura tu mpaka pale nchi husika ikijisikia ndipo iitangaze ziara husika kuwa ni rasmi?

Kwa idadi ya Marais kutoka afrika waliotembelea marekani tena wengine wakionekana ikulu ya marekani kabisa halafu Leo tuambiwe ziara zao hazikuwa rasmi huko ni kuwakosea heshima viongozi kutoka afrika na ni kuwa honganisha na wapiga kura wao.
Samia ajifunze kwa Magufuli
 
Jifunze tofauti ya State Visit, Official Visit, Working Visit, Private Visit.
Kwahiyo unamaanisha hata ule utitiri wa Marais wanaotutembelea inawezekana tukaona ziara rasmi zikawa chache hata iwe zaidi ya miaka kumi huko nyuma kwa Marais kutoka bara jingine?

Yaani siku kukitembelewa na rais wa uturuki Recep Tayyip Edogan tuseme ni rais wa kwanza kutoka bara ulaya kufanya ziara rasmi nchini kwetu kwa kipindi Cha miaka kumi iliyopita?
 
Kwa hiyo hata bibi chaudele wa "roho tuwa" alienda kupiga misele tuu kule
 
Kwahiyo unamaanisha hata ule utitiri wa Marais wanaotutembelea inawezekana tukaona ziara rasmi zikawa chache hata iwe zaidi ya miaka kumi huko nyuma kwa Marais kutoka bara jingine?

Yaani siku kukitembelewa na rais wa uturuki Recep Tayyip Edogan tuseme ni rais wa kwanza kutoka bara ulaya kufanya ziara rasmi nchini kwetu kwa kipindi Cha miaka kumi iliyopita?
Fanya homework yako kupata facts, usipende ku speculate.
 
Sawa mkuu lakini taarifa kuwa bara zima la afrika hakukuwahi kuwa na ziara rasmi ya rais kutoka bara la afrika kwenda USA ndani ya kipindi Cha miaka 15 nacho kinafikirisha sana.
 
Swali ni je Hawa Marais wengine kutoka afrika ambao kwa mamia walioitembelea marekani kwenye hicho kipindi Cha miaka 15 kabla ya hii ziara ya Ruto ni kwamba ziara zao hazikuwa zikitambulika na serikali ya wamarekani?
Ni nani alipaswa kuwa wa kwanza na kwanini?
 
Sawa mkuu lakini taarifa kuwa bara zima la afrika hakukuwahi kuwa na ziara rasmi ya rais kutoka bara la afrika kwenda USA ndani ya kipindi Cha miaka 15 nacho kinafikirisha sana.
Wenzetu wamejipanga. Kukutana na rais wao tu wanakutumia kama mtaji. Ndiyo maana unaweza kusikia Samia kaenda US lakini hajakutana na rais.

Katika zama hizi, huwezi kufanya state visit Marekani kama huna geopolitical agenda kubwa, huna lobbying machinery kubwa, huna exports za maana, huna big deals, huna business community kubwa.

Tanzania imeshindwa na Kenya katika hayo mambo yote.

Mara ya kwanza na ya mwisho kwa rais wa Tanganyika kufanya State Visit Marekani ilikuwa around July 15 1963 wakati Nyerere amemtembelea John F Kennedy. Enzi za Tanganyika huko hata kabla ya Muungano. Wakipanga jinsi ya kuukabili Ukomunisti usiingie Africa.
 
Back
Top Bottom