Rais William Ruto kuhutubia kikao cha pamoja cha bunge la Marekani

Ikaria

Member
Jul 17, 2019
74
203
Kamati ya Bunge la Marekani🇺🇲 kuhusu Mambo ya Nje imemuandikia barua Spika wa Bunge kuomba ridhaa yake ili Rais William Ruto ahutubie kikao cha pamoja cha Bunge hilo

Iwapo Mheshimiwa Spika atakubali, Rais William Ruto atakuwa :

• Kiongozi wa kwanza kutoka Kenya kuwahi kuhutubia Bunge la Marekani.
• Kiongozi wa pili kutoka Afrika kuhutubia Bunge hilo katika kipindi cha miaka 18 baada ya Rais mstaafu wa Liberia Ellen Johnson.

Rais William Ruto anatarajiwa kufanya Ziara ya Kiserikali nchini Marekani tarehe 23 Mei 2024.

20240502_102551.jpg
20240502_102556.jpg
 
American interest first, ukiona kiongozi wa Africa anapendwa na mabeberu ujuwe ameshawauza watu wake.
 
Hapa Tanzania labda Polepole tu aweza kualikwa huko. Hatuna watu wengi wenye logic. Haalikwi kwa sababu ya lugha tu, na logic.
 
Hapa Tanzania labda Polepole tu aweza kualikwa huko. Hatuna watu wengi wenye logic. Haalikwi kwa sababu ya lugha tu, na logic.
Labda Logic. Maana lugha hutafsiriwa. Na mpaka wakualike ni Lazima uwe na maslahi nao.

Kwa wazungu Kenya ni 80% ya Afrika Mashariki. Walisema Afrika ya Mashariki mara nyingi humaanisha Kenya kwani ndiko kwenye maslahi yao mengi.
 
#UPDATE📌: Spika wa Bunge la Marekani Mike Johnson, amekataa ombi la kutaka Rais William Ruto ahutubie kikao cha pamoja cha Bunge atakapofanya ziara ya Kiserikali mwishoni mwa mwezi huu Mei, 2024
 

Attachments

  • 20240511_221400.jpg
    20240511_221400.jpg
    217.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom