Mshahara wa Mwanajeshi wa Tanzania

Mshahara wa Mwanajeshi wa Tanzania

Mshahara wa mwanajeshi kuwekwa hadharani una madhara hani katika nchi? nadhani ni uoga na hofu isiyokuwa na msingi, hawa wanajeshi tunaishi nao mtaan ni ndugu na marafiki zetu mishahara yako, posho zao na benefits nyingine kwenye financial institutions tunazijua kwa uwaza tu. Mtu angeuliza mafunzo wanayopitia angalau tungeweza kusema siri ila sio mshahara. Na jeshi sio kujitolea kwa miaka hii ni ajira kama ajira nyingine tu na wanamishahara mizur kuliko kada nyingine kama Polisi, Magareza , waalimu na Afya.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Kinachoonekana hapa kuna wengine hatufaham ila kunyamaza inakua tatizo.
Kama mtu anafaham na nimehitaji kutumiwa direct message au private message, tena sema kiasi kadirishi.

Shida ipo wapi hapo?
 
Nisawa na watumishi wengine wa Serikali. Ila ukioa unapata posho ya mke ni kama 75% ya mshahara. Kuna jamaa aliniambia hivyo ila sina uhakika.

Na hiyo posho ya wife, anaweza kuomba awe anachukua wife mwenyewe kama wewe huaminiki.
Sasa mkuu tutasikia hivi mpaka lini?

Si anayefahamu atudokeze japo kwa ufupi?

Tunayasikia mengi, sasa kuliko tuisgie kuimba mambo yakuambiwa tena unakuta anayeniambia naye kasikia tu.

Leo nahoji anayefahamu aseme, hata kwa direct message nashangaa mnatoa ushauri nasaha tu.
Kama unafaham dokeza ROUND FIGURE.
 
Degree ni 1.5m
Comment #40 [emoji2][emoji2][emoji2]
Ndio naanza kuona round figure.
Asante mkuu hatakama hujatoa details sana.
Wakijibu wengine mwisho wa siku nitazitaftia hata wastani.

JF raha sana jamani.
 
Nadhan wengi waliojibu hapo juu ni walipwaji wa mshahara,ndio wasiopenda mishahara yao ijulikane ni kias gani! Mbona mh.mpendwa wetu raisi wa nchi alitangaza hadharani mshahara wake? Hata salary slip alisema angekua tayari kuionyesha,kwa watakaohitaji.Sasa huyo alieuliza amekosea nini,mbona humu mnatoa majibu ya mambo nyeti sasa la mshahara vipi?
 
ingekugharimu nini kusema hujui ama kupita kimya? Idara nyeti kwani hiyo pesa yake inatoka wapi kama si kodi zetu. Unadhani vijana wasomi watahamasika vipi kwenda jeshini bila kujua manufaa yake ikiwemo mshahara?
 
inasemekana eti form 6 wanakula kilo 2 kwa mwezi eti
 
Watu wamekaa kinongwano
hata akiujua utamsaidia nini sasa, mshahara wa Raisi hata ukiujua haukufanyi uvutike kuiomba nafasi hiyo,,,, sasa jeshini ni kada ya kawaida kabisa kama mtu unapenda kujiunga na jeshi wewe nenda kajiunge si basii suala la mshahara utakutana nalo huko huko sio suala letu huna uzalendo wewe maana unatanguliza pesa sana badala ya wito binafsi
ngwa tu hivi kweli huyu alishindwa kupata taarifa za mishahara ya jeshi mpaka aulize kwenye mitandao. Wanajeshi kibao tunawafahamu wanaishi mitaani kwetu anacho kingine anachokitafuta zaidi ya mshahara.
 
Watu wamekaa kinongwano

ngwa tu hivi kweli huyu alishindwa kupata taarifa za mishahara ya jeshi mpaka aulize kwenye mitandao. Wanajeshi kibao tunawafahamu wanaishi mitaani kwetu anacho kingine anachokitafuta zaidi ya mshahara.
Kweli, atakuwa na lake huyu na hao vijana wake!
 
Ukitonga wa maisha unategemea akili ya mtu ilivyo na siyo kazi anayofanya unafikiri kupokea salary kubwa ndiyo njia ya kurahisisha maisha?kama ni hivyo umepotea moja kwa moja.... hela nyingi kwenye akili mbovu ni janga kwa maana hiyo haijalishi unafanya nini na unalipwa kiasi gani mafsnikio yako na ahueni yako ni maamuzi yako juu ya kile unachopata au kinachopitia mkononi mwako mara kwa mara bila kijali ni kikubwa au kidogo
 
Humu wamejaa wanajeshi vilaza ndo wanaojibu majibu ya viroba eti jeshi nikujitolea hakuna mshahara hebu serikali isiwalipe miezi miwili tu tuone huo uzalendo wenu mnaousema na kujitolea kwenu unakuta wanajeshi wanaburuza vitambi eti nawenyewe wanajitolea hahahaha tanzania raha sana kuishi
 
haaa haaaaa daaaah, unachekesha sanaaa; ujue hata jina lako linaonesha wewe kweli ni "MiniActivist " sasa wewe wafikili kila jambo huulizwa katika kandamnasa kama hapa JF? Jifunze nawe mambo ya siri na ya hadhalani, maana kwanza ; mshahara ni siri ya mtu, pili; Jeshi sio kituo cha kugawa hela/mishahara Jeshi ni sehemu ya Uzalendo, Heshima kwa Taifa linalojitambua kama Tanzania, na tatu ; Jeshi sio siasa ; leo huyu anasema kile huyu hiki Jeshi ni nidhamu maelezo yako tu hapa yanaonesha hata nidhamu yako ni ya mashaka sana aiseeee.

Kwa hiyo wahitaji kuelewa nenda mahali husika uliza utajulishwa ILA UWE NA UBAVU, na UWE MTANZANIA. maana nimeishakujulisha kuwa Jeshi sio chumbani kwako ambako unafika kila mahali.

kuhusu, kuelimisha hebu angalia nyuzi zingine ambazo nimechangia uone kama naelimisha au napotosha. mf. katika mwanafunzi wa UDOM aliyetengeneza mtandao wa mawasiliano....unaoelekeana na fb na nyinine pia ujue kuwa unaongea na kichwa na sio kilaza na nina taarifa za kutosha ninapoongea sio tu siasa siasa na maneno chakavu/ au maneno mbovumbovu.

Naamini umeelewa kama kweli wewe ni mwelewa na hii itanipa uwezo wa kuelewa kama kweli wewe na vijana hao wenzako mna uwezo wa KUWA WANAJESHI... Ila tu nikukumbushe kuwa hadi hapo Umeisha poteza sifa zote za kuwa mwanajeshi, kwa kushindwa kutanguliza uzalendo na utaifa ukaleta hela/mishahara kuwa jambo la msingi sana kwako!! pili kutafuta habari za siri/za Jeshi katika mitandao ya kijamii ilihali wajua mahali sahihi pa kupata taarifa kama hizo.

Pia tambua, hapa JF sio Watanzania pekee waliomo humu ni kila taifa labdo hata hili hujui maana kama hujui hilo basi inawezekana ukawa Activist juu yako mwenyewe!

Tena wewe huelewi hata juu ya mtandao wa kijamii hapa hata uwe wapi au nani kutumiwa private message katika in box yako haizuilii wengine kujua ulichotumiwa kwa mfano; wote hapa tunajua kuwa wewe unatumiwa sasa ujumbe kuhusu kadilio la mishahara ni rahisi sana KUFANYA UDUKUZI NA KUJUA KILA KITU , pale ambapo mtu asiyeitakia mema nchi yetu anaweza hitaji kufanya hivyo.
Yaani kwa kifupi hadi hapa wewe HUFAI KUWA MWANAJESHI NA HAO WENZAKO SIJUI WA KIJIWENI AU NYUMBANI KWAKO/KWENU.


Natanguliza Pole Zangu kwako kwa kukosa sifa ya kuwa Mwanajeshi na hao wenzako pia!

Asante.
 
Na bajeti mpya wanaongezewa posho ya kufidia msamaha wa kodi.
 
Watanzania tuwapuuze watu kama hawa ni maadui wa nchi toka lini mshahara wa idara nyeti kama hii ukaulizwa mitandaoni? Kwa nini asiwaulize hao maeafiki zake waliomuambia aje kuuliza humu?
Hawa ndio maadui wa Tanzania kama unataka kujua nenda kambi yeyote iliyo karibu nawe utapata jibu mujarabu.

Tanzania kila kitu n nyeti daah kuna madhara gan mtu akijulikan
 
nenda upanda pale ngome utajibiwa kila swali kwa umakini zaidi bila upungufu
 
Back
Top Bottom