Msemaji wa Serikali Hakuwa mkweli kuhusu Mafao ya PSSSF kwa watumishi wa serikali walio staafu

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Msemaji wa serikali alitangaza akiwa Singida kuwa tar 22 mwezi huu september wastaafu tayari wamelipwa stahiki zao za Mafao. Leo hii tupo wastaafu 15 kutoka secta mbali mbali tulio staafu mapema mwaka jana mwezi wa 12, 2020, leo tarehe 30 septemba tumeenda Benki saa 2.27 usiku na kubaini hamna mafao yaliyowekwa na ofisi ya PSSSF kwenye akaunti zetu hadi sasa, Tofauti na namna Msemaji wa Serikali alivyo watangazia waandishi wa Habari na watanzania.

Niwaombe tu Wastaafu wote, msitilie maanani kauli ya rais alivyo tangaza kuwa wastaafu watakuwa wanalipwa mafao yao kila mwezi kauli hii itawapoteza na mtashindwa kufanya shuguli nyingine. Mjipange vilivyo maana mtakuwa na safari ndefu sana, msemaji wa serikali aje asahihishe kauli yake j2 ijayo maana ni taarifa zisizo na ukweli wowote, ajiridhishe kwanza na taarifa kabla hajazitoa kwa waandishi wa Habari.
 
Back
Top Bottom