Malipo ya Pensheni hadi kufa kwa watumishi wa umma ni mfumo ovyo sana

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,681
46,367
Huu mfumo wa kuwalipa pensheni viongozi na watumishi wastaafu kwa muda wote mpaka wanapofariki sio endelevu, unaliumiza taifa kiuchumi na kuwadumuza watumishi wa serikali ambao wanasubiria pesa kiduchu kila mwezi zisizoweza kubadili chochote maishani mwao. Huu ni mfumo wa kitwana na kimasikini sana hasa kwa watumishi wastaafu wa ngazi za chini.

Serikali inapaswa kulipa kwa mkupuo pesa zote za pension kwa wastaafu muda mfupi tu pale watumishi wanapostaafu kisha kuwaacha waendelee na maisha ya binafsi. Kama hili ni gumu sana basi angalau iwekwe ukomo kwamba wastaafu walipwe pensheni zao zote ndani ya kipindi kisichozidi miaka mitatu tu tangu wastaafu.

#Pension ni actuarial science.
 
Ilitakiwa baada ya kustaafu, kila mstaafu anachukua mzigo wake, na kwenda kupambana kivyake mtaani. Akiamua kuzitapanya au kutapeliwa hayo yake, atajua mwenyewe.
 
Walipwe hivyo hivyo kila mwezi. Wakilipwa kwa mkupuo wanamaliza halafu wanaanza kulilia waingizwe TASAF.
 
Back
Top Bottom