Ni wakati sasa Msemaji Mkuu wa Serikali awe anachapisha taarifa yake na kurusha kwa umma baada ya kuzungumza na vyombo vya habari

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Tathmini inaonyesha msemaji wa serikali baada ya kuzungumza na waandishi wa habari taarifa yake uishia hapo au wakati mwingine kunukuliwa vibaya.

Ili kuweka taarifa na kumbukumbu sawa kwa umma nashauri kuanzia sasa awe anatoa taarifa ya maandishi kwa umma baada ya kuzungumza na wananchi. Nashauri taarifa zake zote alizowahi kutoa ziwe zinapatikana kwenye tovuti zote za serikali ili kila anayetembelea tovuti hizo apate same message sasa na siku za mbeleni.

Nashauri haya kwa sababu yeye ndiye mtoa mwongozo wa wapi tulipo, tunapokwenda na tulipotoka. Maneno yake kwa vyombo vya habari ukiyasumarize yatakuwa msaada mkubwa kwa umma na viongozi wa mikoa na wilaya wasiosikiliza vyombo vya habari.

Nashauri pia taarifa yake ya miezi mitatu iwe inagusa kila sekta na ikiwezekana wasemaji wa taasisi na maafisa habari washiriki kuandaa taarifa za sekta zao.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom