Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,589
- 19,490
ni kwa sababu inaelekea bado huoni tofauti ya chama na serikali. Chan's kinajiendesha kwa matamko ya vikao na ya viongozi wao. Serikali inaendeshwa kwa Sheria na maamuzi bunge. Ni kinyume cha Sherpa kwa mtumishi wa serikali kuchanganya matamkoyakisiasa kwenye utendaji wake. Lazima Ccm wabadilishe ilani yao iwe sheria ya bunge ndipo itambuliwe kisheriaMkuu naona hujui unazungumza nini? Hivi kwenye sheria iliyounda shirika la nyumba inazungumzia kuwa kwamba watapitia upya utaratibu wa kupangisha? Ilani ya Chama kwa wakati husika ndio inayoweza kusema nini kifanyike kwenye sekta husika na nini kisifanyike. Unataka kusema Ununuzi wa Meli mpya ziwa Victoria upo kwenye sheria iliyounda mamlaka ya bandari? UUzaji wa nyumba za serikali umo kwenye seria iliyoanzisha NHC au ilikuwa ilani ya Chama? Ubinafsishaji, ujenzi washule za kata, ujenzi wa barabara n.k ni vitu gani kama sio ilani? Kinachofanyika Bunge linapitisha tu bajeti ambayo inatekelezwa na watumishi wa serikali.