Mgao mkali unaoendelea hapa nchini, unatokana na ilani ya CCM ya kutaka "sifa" ya kusambaza umeme katika Kila Kijiji!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Kwenye biashara kuna kitu kinachoitwa "demand and supply principle"

Unapoona mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wako wa kuhudumia, kinachotokea baada ya hapo ni upungufu mkubwa wa huduma hiyo, ambayo inaweza kusababisha kitu tunachokiita "chaos"

Niseme wazi kuwa kutokana na mgao mkali sana unaoletwa na shirika letu la umeme nchini TANESCO, nchi yetu ipo "under crisis"

Hivi unawezaje kuelezea ukatikaji wa umeme huu tunaoshuhudia, mathalani katika jiji la kibiashara la Dar hivi sasa, ambapo umeme unaweza kukatwa na kuwashwa hata zaidi ya mara kumi Kwa siku?

Wakati mwingine umeme unakosekana kwenye baadhi ya maeneo hapa jijini mchana na usiku mzima!

Hivi hawa TANESCO na serikali ya CCM inajua hasara wanayopata wafanyibiashara, ya mabilioni ya shilingi kila siku?

Nawaonea huruma zaidi Hawa vijana biashara ndogo ndogo, walioamua kujiajiri kwenye salon za kunyoa na zile za ususi wa kinamama, namna ya hasara kubwa sana wanazopata kutokana na kukatika Huku Kwa umeme kusiko na mpangilio hata kidogo.

Lakini leo nataka "niwaibie siri" ya matatizo haya makubwa sana tunayokabiliana nayo ya mgao wa umeme hapa nchini.

Siri hiyo kubwa inatokana na ile "principle" niliyoeleza hapo awali ya "demand and supply"

Nina maana kuwa Kwa mfano tukijua kuwa umeme wote tunaozalisha hapa nchini ni Megawatts 1500 lakini mahitaji pamoja na huo wa REA tunaopeleka kwenye vijiji vyote nchini kuwa ni Megawatts 3000!

Automatically ni lazima tuwe na "scarcity" na kuwa na mgao mkali kabisa wa umeme!

Hivi inakuwaje Kwa serikali hii ya CCM ilete ilani ya kusambaza umeme kwenye vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2025, wakati wakijua fika kuwa umeme walionao hauwezi tosheleza mahitaji ya Hawa Hawa wateja ilionao hivi sasa?

Sasa Hawa CCM kuleta ilani ya kusambaza umeme vijiji vyote nchini, ni kutaka tu kujijengea sifa za kisiasa, lakini wakijua fika kuwa hiyo ni "NEXT TO IMPOSSIBLE MISSION"

Washahili Wana msemo unaosema ukitaka kumwiga nyani anavyopalalamia kwenye matawi unaweza pasuka msamba!

Hawa CCM wasiige hizo nchi zilizoendelea, ambazo wana-supply umeme hadi vijijini, lazima wajue kuwa hilo jambo ni "process" ya kidogo kidogo hadi mwisho unafika.

Lakini sivyo wanavyotaka wao kwenye ilani yao kuwa eti hadi ifikapo mwaka 2025, Kila Kijiji hapa nchini kitawasha "bulbs" za umeme na kutokomeza vibatari!
 
Halafu pamoja na mateso makubwa tunayoletewa na serikali yetu ya CCM, bado kuna baadhi ya watu wanaonufaika na mfumo huu wa utawala, wanatu-discourage, eti tusiandamane hiyo tarehe 24 mwezi huu!
 
Back
Top Bottom