Msechu (NHC): Natekeleza ilani ya CCM

Msechu (NHC): Natekeleza ilani ya CCM

Nchi yoyote inayofuata utawala wa sheria huongozwa kwa kufuata misingi na taratibu za kisheria ambazo zimetungwa na kuhalalishwa ndani ya bunge halali (legislature). Nchi haiongozwi wala kutawaliwa kutumia sera wala ilani za uchaguzi za vyama vya siasa. Ilani hizo na sera za vyama vya siasa inatakiwa zitumiwe kutoa mwelekeo wa utungaji wa sheria! Kwa mfano ni sheria zipi zitungwe, sheria hizo zikazie nini, vipaumbele katika utendaji viwekwe wapi, n.k.

Ni jambo la hatari sana na ni upotovu mkubwa kuingiza siasa katika utendaji wa serikali (ndo hayo yanayoendelea) na jambo hili limeshehenezwa sana na muundo wa CCM ambao hautoi mgawanyo wa kiutendaji kati ya serikali na chama. Tunajua wote jinsi jambo hilo lilivyougharimu uchumi wa Tanzania enzi za chama kushika hatamu. Wanasiasa (wawakilishi wa vyama) kwenye mashirika ya umma ni mojawapo ya vyanzo vya migogoro na matitizo ya kimenejimenti yaliyoua mashirika mengi ya umma.

Ni kweli kuwa baada ya kubadili mfumo, bado nchi inaendeshwa kimazoea. Watendaji wa serikali na hata Mawaziri (ambao ni wanasiasa) inatakiwa watekeleze sheria za nchi. Na sheria za nchi ni zile zilizotungwa na bunge!! Ni kweli kuwa sera na ilani za vyama vinaathiri utungwaji huo wa sheria, lakini sheria zikishasimama haziwi za vyama tena. Zinakuwa sheria za nchi na zinawahusu watu wote.

Haya ya kukaa na kusema hapa tunatekeleza ilani ya uchaguzi wa chama tawala ni upotovu na unaipeleka nchi pabaya mahali ambapo kila kitu kina-siasishwa na kufanya sehemu ya siasa. Manake utasema hata mahakama zinaamua kwa kufuata ilani ya vyama vilivyoko madarakani kwa sababu vyama hivyo ndo vimetoa sera inayoongoza sheria!! Tumepotoka mno na kupoteza mwelekeo! Hakika huu ugonjwa hautapona haraka mpaka kiingie chama kingine madarakani; hata hapo kuna hatari chama kingine kikiingia madarakani, kuendeleza mfumo huo.

Watendaji wote pamoja na rais mwenyewe wanaongoza nchi kwa kufuata sheria za nchi na si ilani wala sera za vyama vyao. Sera na ilani za vyama vya siasa zinatumika kuweka mwongozo tu wa sheria zitungweje! Ndo maana sheria zinajadiliwa na kupitishwa bungeni.

Hii inasababishwa mambo mengi kupenyezwa; mambo ambayo hayakupita bungeni yanapenyezwa kwa visingizio vya ilani na sera za vyama. Hatari hapa ni kubwa sana!!
 
Namimi pia nipo curious kujua ni kipengele gani cha ilani anachoreffer na kwa kutetea hatua gani anazochukua sasa...

Hao ndio watalaam wetu, nusu wanasiasa nusu wataala; baada ya hapo utasikia anagombe Ubunge! We ushangaai iweje Kamishana wa Madini kugombea ubunge? umewaikusikia nchni gani kama si katika nchni ya hii iliyojaa vijana walio hasiwa akili? Hii ina maana wanapofanya kazi wanatekeleza matakwa ya wanasiasa zaidi aka Balali na EPA nk ndio ilani zenyewe za CCM.
 
Ndo ameishajifukuzisha kazi rasmi.
Kilichomfanya ashindwe kutoa justifications zake kwa lugha ya kibiashara na kukimbilia
kwenye lugha za siasa hatakisahau maishani mwake. nimeanza kumuhesabia siku.
 
Nehemia,wala haukutakiwa kujitetea hivyo. Kwamba unatekeleza sera za Chama? Unajumuisha yote uliyoyafanya unatekeleza sera za CCM?
Tatizo watu hawajazoea speed yako. Make sure kila unachokifanya una baraka ya Board yako. Dunia haikawii kukugeuka. Kaza buti
 
Msechu my hero,

Aliwatumia vijana wa chadema pale UDSM walikusanywa na Dr mkumbo wawape pressure wahindi...

Angalizo vijana wa chadema are very cheap..to organize

Mungu anisamehe tu,manake neno ambalo ningekwambia hapa lingenisababishia permanent ban.
 
Jamani, hebu tupeni cv ya mchechu kwani inaelekea hujyu jama ni kiboko.
 
Technoctratic yeyote mwenye akili timamu hawezi kujitetea kwa refer sera za chama lazima atetee kanuni, sheria na taratibu za nchi, kwa utetezi huu inadhihirisha wazi jinsi siasa zilivyoharibu bongo za watanzania na ndio maana unakuta proffesors wanaacha kazi nzuri za research,kufundisha na kuandika vitabu wanakimbilia siasa na kupelekeshwa na makatibu wa vyama wasio na shule kama akina makamba
 
ni kwa sababu inaelekea bado huoni tofauti ya chama na serikali. Chan's kinajiendesha kwa matamko ya vikao na ya viongozi wao. Serikali inaendeshwa kwa Sheria na maamuzi bunge. Ni kinyume cha Sherpa kwa mtumishi wa serikali kuchanganya matamkoyakisiasa kwenye utendaji wake. Lazima Ccm wabadilishe ilani yao iwe sheria ya bunge ndipo itambuliwe kisheria
Mkuu wewe ni mtumishi wa serikali? Unaonekana unapenda ushabiki kwa vitu ambavyo viko wazi tu. Sijui lakini labda watu wengine watakusaidia kukuelimisha kuhusu hili na zaidi ya hapo kasome Code of conduct for Public Service. Unasema mambo yote yanaenda kwa sheria na zilizotungwa na bunge hivi standing orders na circulars mbalimbali zinapitishwa na bunge lipi? Hata Mishahara ambayo bunge linapitisha bajeti yake uliza kama wabunge wetu huwa wanashiriki kupitisha zaidi ya kuambiwa ni siri. Na kwa kuongeza kama Chadema wangeshinda na kuweka kima cha chini cha 315000/= au kupunguza bei ya vifaa vya ujenzi ungejua kama ni ilani ya chama tawala ndio inayotekelezwa. Hope utakuwa umenielewa unless uwe na kichwa kigumu sana
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hao ndio watalaam wetu, nusu wanasiasa nusu wataala; baada ya hapo utasikia anagombe Ubunge! We ushangaai iweje Kamishana wa Madini kugombea ubunge? umewaikusikia nchni gani kama si katika nchni ya hii iliyojaa vijana walio hasiwa akili? Hii ina maana wanapofanya kazi wanatekeleza matakwa ya wanasiasa zaidi aka Balali na EPA nk ndio ilani zenyewe za CCM.
Na wewe hushangai Mwalimu tena Mkaguzi kugombea Ubunge?
 
..Kutekeleza Ilani ya Chama kulichoko Madarakani ni sawa Jamani lakini hii ni kinadharia zaidi..Maaana yake ni kwamba Ilani inaweza kutafsrika katika Sera, Miongozo na Maelekezo ya Mara kwa mara ya Serikali...Sema kiukweli huwezi kutamka moja kwa moja kwamba natekeleza Ilani ya Chama ilihali wewe ni mtumishi wa Umma!!!..Sasa kama Mchechu anatekeleza Ilani ya Chama, Werema naye anaweza kuibuka na kudai natekeleza ilani ya Chama na CAG naye aseme hivyohivyo...ofcoz iatakuwa ndivyo sivyo..
Kinadharia inaweza kuonekana hivyo lakini kwa wale watumishi wa UMMA ni bora wakawa wanasema wanatekeleza maelekezo ya Serikali kuliko kusimama kwenye 'back up' ya Chama!!
Nimefurahishwa na mchango wako!!!!!!!!! Ni kweli kabisa hakutakiwa kusema directly namna japo huo ndio ukweli. Alitakiwa aache kazi hiyo kwa Wanasiasa i.e Mawaziri kama Mama Tibaijuka
 
Mkuu wewe ni mtumishi wa serikali? Unaonekana unapenda ushabiki kwa vitu ambavyo viko wazi tu. Sijui lakini labda watu wengine watakusaidia kukuelimisha kuhusu hili na zaidi ya hapo kasome Code of conduct for Public Service. Unasema mambo yote yanaenda kwa sheria na zilizotungwa na bunge hivi standing orders na circulars mbalimbali zinapitishwa na bunge lipi? Hata Mishahara ambayo bunge linapitisha bajeti yake uliza kama wabunge wetu huwa wanashiriki kupitisha zaidi ya kuambiwa ni siri. Na kwa kuongeza kama Chadema wangeshinda na kuweka kima cha chini cha 315000/= au kupunguza bei ya vifaa vya ujenzi ungejua kama ni ilani ya chama tawala ndio inayotekelezwa. Hope utakuwa umenielewa unless uwe na kichwa kigumu sana

Nina kichwa kizuri sana ndugu yangu. Kama kuna governement circular imetoka na imetangazwa kwenye Government Gazette, basi hiyo ni kama sheria na itatekelezwa, lakini mtekelezaji hawezi kuwa anatekeleza serka za chama fulani bali anatekeleza ile order ya serikali. Kama serikali yetu inaandika mambo ya kisiasa kwenye madokument ya sheria basi wanakosea wote. Msechu kama professional hatakkiwi naye afanye makosa ya wanasiasa. Ni kama ambavyo polisi wanavyojiingiza katika kutetea CCM eti kwa vile ni chama tawala ilihgali kuna tofauti kubwa sana baina ya serikali na Chama. Mtu kama Nnauye ambaye ni kiongozi wa CCM lakini hana wadhifa wowote serikalinali hatakiwi kutoa amari yoyote kwa wafanyakzi wa serikali. Miaka kadhaa ilipofika, niliwahi kumsikia Malegezi wa Umoja wa Wazazi akisema atamachukulia hatua eti Mkuu wa Wilaya ya handeni kwa kushindwa kwenda kumpokea!!!. Upuuzi huu wa kutokujua mipaka baina ya siasa na majukumu ya serikali ndio unatufanya tunaishi kisiasa siasa hadi leo baada ya miaka hamsini.
 
nakubaliana na tetere.CCM halisi ni chama cha wakulima na wafayakazi na mabdiliko yanaendelea NHC hayawezi kuakisi mtizamo huo.Si muda mrefu watanza kumkimbia na Kumkana mchechu.Ila ni lazima Mchechu aseme hivyo, lakini sidhani CCM ilikuwa na hiyo dira ambayo ameichukua Mchechu.Sidhani dira huwa inabadilika kulingana na ni nani anaongoza shirika.Yetu macho
 
Kazi ya ku-invoke kuwa yanayotekelezwa ni matokeo ya policy za vyama hivi na vile ni ya wanasiasa. Hata hivyo kwa hali ilivyo Tanzania leo hii ni vugumu kujua tofauti kati ya mwanasiasa na mtendaji. Imekuwa ni kawaida kwa watendaji ku-invoke kauli za kisiasa ili wapate "shavu" la wanasiasa. Tatizo letu kubwa ni mfumo ambao umewapa nguvu kubwa wanasiasa. Huu ni mfumo hatari sana kwa maendeleo. Wanasiasa wana nguvu na uwezo wa kuingilia eneo lolote la kiutendaji bila kufuata utaratibu wowote unaoeleweka. Kwa hali hiyo watendaji wengi ambao hawajikombi kwa wanasiasa wako "exposed to malice" za wanasiasa!

Ndo maana utawasikia watendaji kila siku wakijikosha kuwa wanatekeleza sera za chama. Ni lazima to review mfumo wetu, ili interference ya wanasiasa kwenye maeneo ya utendaji idhibitiwe sana na sheria na taratibu. Kwa jinsi hii wanasiasa hawataweza kuwa na nguvu kubwa waliyonayo leo. Na hiyo ndo itamaliza " huku kujikomba" tunakokusikia kila kukicha kutoka kwa watendaji kwenda kwa wanasiasa!!
 
Back
Top Bottom