Msaada wa namna ya kudeal na Mpangaji msumbufu

Ninaweza kukupa ushauri kadhaa juu ya jinsi ya kushughulikia mpangaji msumbufu na namna ya kushikilia mali yake kama hatua za mwisho. Hapa kuna hatua unazoweza kuzingatia:

1. Wasiliana na mpangaji: Anza kwa kuzungumza na mpangaji wako kwa njia ya kirafiki na uwasilishe wasiwasi wako juu ya malipo ya kodi na bili za maji. Jaribu kuelewa sababu ya kutolipa na ongeza umuhimu wa kulipa madeni yake kwa wakati.

2. Weka maandishi: Ikiwa mazungumzo ya awali hayajazaa matunda, andika barua rasmi kwa mpangaji wako. Taja malimbikizo yake ya kodi na bili za maji na wapeleke barua hiyo kwa njia ya kuthibitika ili kuwa na rekodi ya mawasiliano.

3. Panga ratiba ya malipo: Kwa matakwa ya pande zote, unaweza kujaribu kufikia makubaliano ya kulipa madeni yake kidogo kidogo kwa muda fulani. Kwa mfano, unaweza kukubaliana kuwa anaweza kulipa nusu ya kodi na bili za maji katika kipindi cha mwezi mmoja.

4. Toa ilani ya kisheria: Ikiwa mpangaji wako haendelei kulipa au kutoshirikiana, unaweza kufikiria kutoa notisi ya kisheria. Hii inaweza kuwa notisi ya kulipa madeni ndani ya muda fulani au kuwaachisha mkataba wa kupangisha.

5. Lipa hatua za kisheria: Ikiwa mpangaji wako bado anashindwa kulipa na hajali notisi ya kisheria, unaweza kuchukua hatua zaidi za kisheria. Hii inaweza kujumuisha kufungua kesi ya kumwondoa mpangaji au kuchukua hatua zingine za kisheria zinazotolewa katika eneo lako.

6. Shikilia mali: Ikiwa hatua zote za kisheria zimeshindwa, unaweza kujaribu kushikilia mali ya mpangaji wako kama njia ya kurudisha madeni yaliyopotea. Kabla ya kufanya hivyo, hakikisha kushauriana na mwanasheria na kuzingatia sheria za eneo lako kuhusu utekelezaji wa mali.

Ni muhimu kukumbuka kwamba sheria na taratibu za kukabiliana na mpangaji msumbufu zinaweza kutofautiana kulingana na eneo lako na mikataba ya kupangisha. Ni vyema kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa mwanasheria au mamlaka husika ili kuhakikisha kuwa unafuata taratibu sahihi.

Natumai ushauri huu utakusaidia kushughulikia hali hi

yo. Kumbuka kuwa ni muhimu kuwa na rekodi sahihi ya mawasiliano yote na kuzingatia taratibu za kisheria ili kulinda maslahi yako kama mwenye nyumba.
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu

Muandikie notisi , asipo follow throught now from there use power
 
Hili limenifikirisha sana sana kuna mtu namjua mtaani bado kidogo ajitoe uhai jamaa alikuwa hana kazi mkataba umeisha. Ada wife anamdai utafikiri yye ndo mmiliki wa shule , kula nk
Ila wanawake watu wabaya sana aisee yule dada alikuwa anarudi upande wa mwenye nyumba kumgombeza mchizi. Jamaa akawa anapiga tungi mbaya. Sasa amepata kazi kubwa kumzidi yule bwana mwenye nyumba . Tujifunze kuwatendea wqtu mambo mema
Mimi huyo mke ningempa talaka yake chap,mana anakujali kwenye raha tu
 
Kama utakuwa ulipitia maisha ya kupanga kabla hujawa Baba mwenye nyumba hopefully utakuwa na uzoefu na changamoto.

Binafsi nina wapangaji 8, kuna wanaolipa kabla hujawakumbusha na kuna wengine una wakumbusha zaidi ya mara 5 lakini wamekuwa wakitoa ahadi tu pasipo kutimiza.

Kuna mmoja haja ana miezi 4 hajalipa, nasubiria ifike miezi 6 nimtoe kwa nguvu.

Yaani pamoja na kuwajali kwa kuwavutia Maji, Luku yao lakini bado Kodi yenyewe naipata kwa shida.

NB; Nikiambiwa kuchagua biashara ya kufanya hii ya kupangisha sio biashara kabisa, biashara gani hela yako ya mtaji inarudi baada ya miaka 11
Mtuvumilie wapangaji, hali ni ngumu huku mtaani. Lol
 
mrembo usijali.

Naona mpka umefunga PM .

nyie ndo wale mnasema nilifir.wa ila kwa mbinde sanaaaaa.

Mimi huwa nawadunda wenye nyumba kwasababu sheria naijua, Ukija ndani kutoa vitu unapigwa pipe mpka unasahau deni kwa kunogewa na kifir.100000 cha kinyero hiko
 
Unashindwa kulipa kodi ya miezi3 elf60 ety unakimbilia POLISi wametoa bit vyangu na ndani kulikuwa na milion2 inahitaji uwe mpumbavu kukubaliana na hilo endeleeni kudanganyana, vitu vinatolewa na huna utalofanya untavikuta serikali ya mtaa,
HUTAKI USUMBUFU KAA KWA MAMA YAKO AU JENGA NYUMBA YAKO
Kuna mwenzio mwenye nyumba na mjumbe wa mtaa wamelipa 4mil, kisa kutoa vitu nje muhusika Ali safiri.

Akapewa miezi 3 ya kukaa bure ilo atafute sehemu ingine, usiwe mbishiii
 
Mi nadhani pale ukiandika tarehe uliyoingia kama ni baada ya saa sita usik basi akija asbh kukutoa mkatalie. Sheria ya malazi ni masaa 24. yaani siku moja.

Hawa wahuni ndio maana ukienda kuchukua room saa nne au tano huwa wanasema vimejaa coz wanaona hapo wakikupa utakaa Hadi kesho saa nne . Sijui wamelogwa au wateja ndio tumelogwa ?
Wenye guest ni weziiii.
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
Miez miwili ty??nyumba ukiifanya kama biashara utachanganyikiwa na utapiteza ubinadamu wako,fanya kama huduma kusitiri binadamu wenzio unless ukiona mtu ana uwezo hataki kulipa ndo unamuondosha,mm nadai watu miez 6,lkn ukimuona unajiuliza nikimfukuza na watoto ataenda kuishi wapi kula yake tu shida!!
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
Kwani Kwenye mkataba wenu kuna kipengele cha kusumbuana.

Muda wa Kodi umeisha tafuta mpangaji mwingine mpe notice ya week moja Basi,.

Kama Hana hela aondoke hiyo siyo nyumba Yake ni yAKO.
 
Miezi miwili tu?
Kuna mmoja tulipelekeshana mwaka na zaidi..!!
Tulipelekana hadi mahakamani, ila yule mwamba daah!!!
Ilifika mahali nikasema ngoja niende nae hadi mwisho wake tuone utakavyokuwa baada ya kuwa mstaarabu tu kwa kipindi chote hicho!
Mwamba alikuwa na madeni maduka yote ya mtaa, na wengine walijua nyumba yake!
Aliabika siku ya mwisho alikopotelea sijui, vitu vyake vipo vimeoza vingine!!!
Ila nilimuonea huruma kama mwanaume mwenzangu maana awali alikuwa mlipaji mzuri mno, alikuwa analipa kwa mwaka wakati mwingine!
Ila anko Magu aiseeh apumzike kwa amani tu!
Umeandikaa kama Mimi hii issue iliwai kumkuta mpangaji wa mzee wangu....

Sio Siri alitusumbua sana mpk mzee akaogopa jamaa maana alikua kama DUDE wa bongo dar es salaam.....

Anatangaza nyumba kauziwa jamaa alikua kada wa CCM

Kumtolea vyombo nje mpangaji ni process na Ina procedure zake.......

Wasalaam
 
ongea na mkewe kama mara tatu kuhusu hilo jambo.... tena ukiwakuta wawili unaomba samahani na kumuhitaji mkewe kwa mazungumzo.... jamaa atajistukia na kuweka wivu atakufuata na kukulipa hatotaka kero kwa mkewe

kuna muda unatakiwa utengeneze tatizo ili kutatua tatizo
 
Back
Top Bottom