JITU BANDIA
JF-Expert Member
- Feb 5, 2023
- 2,680
- 6,023
Anaandika Nyemo.H Nyemo toka Facebook
Habari za usiku huu,
Naombeni msaada wa kisheria. Leo nimeingia kwa pilato!
Iko hivi wakuu, mzazi wangu wa kiume (baba) alipofariki miaka kadhaa iliyopita nikiwa na miaka mitatu(3). Kulitokea kashkash za ndugu upande wa baba kutaka kumdhulumu nyumba.
Baada ya purukushani za hapa na pale. Mwaka 19 akakabidhiwa nyumba kama msimamizi wa mirathi. Huku ikiandikwa jina langu kama mtoto mkubwa wa kiume.
Ikapita tathmini Fulani ya kupisha ujenzi wa miundombinu Fulani kule lindi. Jina likiwa ni lile lile la kwangu nikiwa Bado na umri wa miaka 13.... Ile tathmini imedumu kwa takribani miaka 24 pasipo malipo.
Ndipo ikarudiwa tena mwaka 2021 nikiwa mtu mzima!, niko kikazi mkoani Kagera. Ikumbukwe kwa miaka yote mzazi wangu wa kike alikuwa akiishi(na Bado wanaishi pamoja na mwanaume mmoja)
Sasa nimekuja kugundua hivi karibuni kuwa alibadili jina! Na kuweka jina lake(nahisi kwa ushauri wa huyo bwana wake)
Kwakuwa ni mama, sikutaka kufatilia saana, hadi hivi sasa ambapo naona huyu mzee, anajipa uhalali kabisa kuwa hiyo fedha yeye ndie ataigawa!
Nimepandwa na hasira mnoo. Na kuona hii ni dharau isiyomithirika wanayotaka kuifanya. Na Mimi siwezi kuvumilia huu upumbavu! Watoto tuko watatu jumla na tuko pamoja kwa hili.
Nilikuwa nna mpango nifungue Shauri la kuomba tafsiri ya mahakama na muongozo wa mgawanyo wa Mali iliyopatikana kutokana na mirathi.
Najua hili linawezekana, na humu kuna manguli wa Sheria humu. Naombeni ushauri na msaada wenu kwenye hili. Je, naanzia wapi!?
Maana nimesoma Sheria yetu ya mirathi ya kimila na kiserikali tunayoitumia(tuliiadapt toka India kama sikosei) ya mwaka 1967.
Inasema wazi, mzazi wa kike atapata theruthi moja ya Mali, na watoto theluthi 2.
Msaada jamani pa kuanzia. Maelezo yamekuwa marefu kumradhi.