Tembo wanaharibu mazao ya wananchi wa Kijiji Kilosa Mpepo na hakuna msaada

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
341231995_613400627334158_2347888481323351816_n.jpg

Sisi wakazi wa Kijiji Kilosa Mpepo, Tarafa ya Ngilangwa, Wilaya Malinyi Mkoa Morogoro tunachangamoto tunaomba msaada wa Serikali.

Serikali itusaidie kuhusu Tembo wanatumalizia mazao, kwa usiku mmoja wanaweza kula hekari zaidi ya 15, tumehangaika hadi ofisi za Wilayani, TANAPA wamekuja kama watalii tena mchana, wamezungukazunguka wameona uharibifu na hawachukui hatua zozote.

Hivyo, hatuwezi kufanya chochote na hata ukipiga simu hawapokei tena tusaidieni kwa maana mpaka kuja kwenu ni katika kutapatapa, Mwaka jana baada ya mazao kuliwa waliandikisha majina ya Wahanga kwamba watasaidiwa, mpaka leo hamna kitu.

Kingine matukio ya Tembo kuvamia vijiji vilivyo karibu na mbuga ni vitu vya kawaida na wamekuwa wakisababisha madhara kwa watu na mali zao, lakini kwa kuwa mara nyingi hakuna mawasiliano, mambo yanamalizika kimya kimya tu na jamii haijui kinachoendelea, ni hadi itokee kama hivi sisi wenye nafasi tuweze kupaza sauti.

Kwa ufupi Tembo kuua mtu au watu ni jambo la kawaida na wala inaonekana sio ishu kubwa ila binadamu ukimuua huyo mnyama msala unakuangukia wewe.
TEMBO MALINYI.jpg


Updates...

UFAFANUZI WA TANAPA
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TANAPA, Catherine Mbena
amesema: “Eneo ambalo limetajwa hapo kuna maeneo mawili ya hifadhi, kuna Kilombero Game Reserve na Hifadhi ya Nyerere.

"Taarifa iliyopo ni kuwa Hifadhi ya Nyerere walipigiwa simu kuwa kuna Tembo wasumbufu katika Kijiji cha Ihowanja siku nne zilizopita, hicho nilichokitaja ni Kijiji tofauti na kilichotajwa kwenye maoni ya mtoa malalamiko.”

“Maafisa wetu walianza safari kuelekea kwenye eneo husika linaloathiriwa na Tembo siku nne zilizopita.

"Pia inaonekana watu wanachanganya kwa kuwa kuna TANAPA na TAWA ambao wote wanafanya kazi ya kufukuza Tembo.

"Upande wa TANAPA inaelekeza nguvu na muda mwingi katika eneo husika kwa kuwa kuna usumbufu wa Tembo na wanafanya kazi kubwa ya kuwafukuza pindi kunapokuwa na uhitaji huo.

"Bahati mbaya, maafisa waliokuwa safarini walikwama katika daraja kutokana na kivuko kilichopo kati ya Wila ya Ulanga na Malinyi kutopitika, wamekaa hapo kwa siku nne, lakini wamefanikiwa kupita leo asubuhi (Mei 6, 2023) kuendelea na safari kwa ajili ya kwenda kushughulikia changamoto husika."
 
Kwa nini hao tanapa wasishirikiane na wanakijiji kuweka uzio wa pilipili kuzuia tembo kukaribia maeneo ya mashamba......kuna sehemu nyingine wanatumia hii njia kuzuia tembo. Nyinyi huko mmefanya juhudi gani kutumia hii njia ya pilipili?​
 
Kwa nini hao tanapa wasishirikiane na wanakijiji kuweka uzio wa pilipili kuzuia tembo kukaribia maeneo ya mashamba......kuna sehemu nyingine wanatumia hii njia kuzuia tembo. Nyinyi huko mmefanya juhudi gani kutumia hii njia ya pilipili?​
Hameni,hayo ni makazi yao nyie mnatafuta nini huko.Njooni mijini
 
Back
Top Bottom