Msaada wa namna ya kudeal na Mpangaji msumbufu

Msaada wa namna ya kudeal na Mpangaji msumbufu

There is no permanent situation in our life.

Ishi na watu vizuri, shida zina tabia ya kukutanisha na watu ambao hukuwatendea vyema.

Kuna Ninja mmoja ameishi kwangu sasa hivi ana mawe na connection za kufa mtu, ana mjengo wake wa ghorofa na ana Kampuni yake, Jana tu katoka kunitembelea na kanitowa na pocket money juu.

Makonda aliwahi kumdhalilisha Chongoro hadharani, sasa hivi Makonda ni jobless kabaki na mitako yake tu na Chongolo ndio Katibu mkuu wa CCM.
Kaka umeongea vyema ila hapo kusema makonda saivi ni jobless ndio uongo uyo mtu ni mtoto wa ccm amekulia umo tangu mdogo enzi za kina sitta,

Magu akumtoa makonda bali alimkuta umo tayari anajina lake zuri tu.
 
We jamaa vp vunja mlango weka vitu vyake nje anavikuta akirudi,au vifungie stoo badilisha kitasa na mpk avikomboe alipe kodi miezi miwili.
Sema kulogwa sasa.
Unataka mwenzio badala ya kulipwa yeye, amlipe yeye mpangaji, mdanganye tyuuh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
Fukuza huyo. Lakini muache tabia ya kuomba kodi kabla ya muda. Tarehe ya malipo ni 30 ila ww unakomaa upewe tarehe za mwanzo wakati namimi najiweka sawa nkulipe. Muwe na vyanzo vingine pia, mnasumbuaga sana mbaka tunawablock kabisa
 
Sasa hizo nyumba zenu za urithi huko uswahilini temeke unadhani Kodi Bei gani kwa mwezi haiwezi kuzidi 30-40 kwa miezi miwili 80 na Umeme 90 Sasa ndo unataka kutoa vitu nje


Jenga nyumba yako mambo ya urithi yamewafanya mmekuwa wajinga na Sio wewe tu .mpo wengi wajinga wajinga Kama wewe
Mkuu mimi nataka nikuweke sawa kidogo, hiko ivi unakuta wazazi waliwai kuja mjini chapu wakajenga sasa kuna ubaya gani mtu kuishi kwao aangaike na kujenga nawakati pa kukaa bure tena kwao papo?

Nyie mnao kuja mjini wengi wenu ata nyinyi mnatamani kabisa wazazi wazazi wenu wangewai wakajenga mapema ili leo hii mkawa na kwenu mjini,

Mimi nimejenga huko pwani nachukua kodi tu lakini hapa mjni dsm nakaa kwenye nyumba ya baba yangu na sina mpango wa kutoka mpaka kufa
Wenye wivu wajinyonge.
 
Fanya kama wazungu wanavyo fanya
Kabla ya kumpangisha aoneshe bank statement inayoonesha kipato chake ..uridhike kwanza ana kipato kweli au anabangaiza...

Kingine aweke dhamana ya hela ...mfano kuna mikataba unaweka Kodi ya miezi miwili kama dhamana ya kuharibu kitu....ikitokea mnasumbuana unampa notice haraka...
Pesa unamrushia ya dhamana kama hajaharibu kitu au humdai....
Kwa hio ambao hatuna bank account tusipange
 
Unaelewa maana ya mkataba? Unalipa kodi TRA?

Kwanza ukijifanya unajuwa sana mkataba ukikutana na mjuwaji inabidi akulipe pungufu pesa nyingine awapelekee TRA wakate nao kodi yao.
Akiwapelekea tra nao wakate kodi yao namfukuza watu wanao hitaji nyumba za kupanga ni wengi sana.
 
Jenga nyumba mkuu hizi nyumba za urithi zinawafumbaza haiwezekani unalalamika kisa Kodi ya miezi miwili 90k unaishi Maisha ya hovyo Sana. Jitafakari nyumba za urithi Tena huko uswahilini temeke nyumba chafu unategemea ulipwe bila usumbufu!
Nyumba za utithi mjini gharama sana ndio maana hata wazazi wako awakuweza kujenga mjini badala yake wamewaachia uko kijijini kwenu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie wala sijawahi kusumbuana na mzee wa mjengo, tena uzuri wake mzee wa mjengo yuko mkoa mwingne, huwa tunamrushia kwa muamala.

Mie huwa nalipa tena hata kabla ya muda kufika, maana madeni mie naogopa km ukomaa.

Kuna rafiki angu yeye wazazi wake wanajua yuko hostel, kumbe kapanga nje. Alijiahidi kulipa lipa ikafka hatua akakwamaa uwiiiiiiih
Sio kwa yule baba afu nae alikua maeneo Yale Yale alisumbuka mnooo.

Ila wenye nyumba muwe wavumilivu bhana.
Hongera kuwa muungwana.

Kuna baadhi ya Wenye nyumba pia hawana huruma inapofikia suala la Kodi.

Muhimu kuvumiliana
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
Samehe kodi hiyo. Kibongobongo kodi ya mwezi sio ishu. Unapoendelea kumvizia akulipe ndio unampa muda zaidi wa kuendelea kuishi kwako.

Kwa upande wa pili angalia sababu za usumbufu wake. Muhimu sana
 
Kodi tunakwama maana landlord anataka miezi 6 wengine mpaka mwaka! Ingekua ya mwezi mbona poa tu
 
Back
Top Bottom