Msaada wa namna ya kudeal na Mpangaji msumbufu

Morgan Fisherman

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
1,799
2,074
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
 
Tumia ustaarabu pesa inasumbua Sana ndugu ukiona mtu anakucheleweshea kodi usifikiri ni makusudi Hali ni mbaya Sana huku mahangaikoni.

najua kuwa lazima atakuwa anakufikiria sana kwa kuwa kipao mbele chake au Cha mtu yeyote kwenye maisha haya ni sehemu ya kulaza mbavu.

Jaribu kumsikiliza na kumuelewa miezi 2 sio mingi kabisa kwa sisi watafutaji mpe muda hata Kama atakutoroka muache aende punguza roho mbaya nae hana Kama wewe ambavyo huna unamkomalia.
 
20230521_000537.jpg
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu

Miezi miwili tu?
Kuna mmoja tulipelekeshana mwaka na zaidi..!!
Tulipelekana hadi mahakamani, ila yule mwamba daah!!!
Ilifika mahali nikasema ngoja niende nae hadi mwisho wake tuone utakavyokuwa baada ya kuwa mstaarabu tu kwa kipindi chote hicho!
Mwamba alikuwa na madeni maduka yote ya mtaa, na wengine walijua nyumba yake!
Aliabika siku ya mwisho alikopotelea sijui, vitu vyake vipo vimeoza vingine!!!
Ila nilimuonea huruma kama mwanaume mwenzangu maana awali alikuwa mlipaji mzuri mno, alikuwa analipa kwa mwaka wakati mwingine!
Ila anko Magu aiseeh apumzike kwa amani tu!
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
Usitegemee kodi ya mpangaji kuishi wala usiipangie bajeti kodi anayotarajia kukulipa.

Ukitaka kupata kodi ambazo hazina usufumbufu jenga apartment hakuna mpangaji msumbufu, ila hawa tunaokaa nao nyumba moja wanasukuma siku tu wamejichokea kuliko wewe, uwe mwelewa tafuta kazi ya kufanya usiishi kwa kutegemea kodi.
 
Kama utakuwa ulipitia maisha ya kupanga kabla hujawa Baba mwenye nyumba hopefully utakuwa na uzoefu na changamoto.

Binafsi nina wapangaji 8, kuna wanaolipa kabla hujawakumbusha na kuna wengine una wakumbusha zaidi ya mara 5 lakini wamekuwa wakitoa ahadi tu pasipo kutimiza.

Kuna mmoja haja ana miezi 4 hajalipa, nasubiria ifike miezi 6 nimtoe kwa nguvu.

Yaani pamoja na kuwajali kwa kuwavutia Maji, Luku yao lakini bado Kodi yenyewe naipata kwa shida.

NB; Nikiambiwa kuchagua biashara ya kufanya hii ya kupangisha sio biashara kabisa, biashara gani hela yako ya mtaji inarudi baada ya miaka 11 🙆
 
Fanya kama wazungu wanavyo fanya
Kabla ya kumpangisha aoneshe bank statement inayoonesha kipato chake ..uridhike kwanza ana kipato kweli au anabangaiza...

Kingine aweke dhamana ya hela ...mfano kuna mikataba unaweka Kodi ya miezi miwili kama dhamana ya kuharibu kitu....ikitokea mnasumbuana unampa notice haraka...
Pesa unamrushia ya dhamana kama hajaharibu kitu au humdai....
 
Kama utakuwa ulipitia maisha ya kupanga kabla hujawa Baba mwenye nyumba hopefully utakuwa na uzoefu na changamoto.

Binafsi nina wapangaji 8, kuna wanaolipa kabla hujawakumbusha na kuna wengine una wakumbusha zaidi ya mara 5 lakini wamekuwa wakitia ahadi tu pasipo kutimiza.

Kuna mmoja haja ana miezi 4 hajalipa, nasubiria ifike miezi 6 nimtoe kwa nguvu.

Yaani pamoja na kuwajali kwa kuwavutia Maji, Luku yao lakini bado Kodi yenyewe naipata kwa shida.

NB; Nikiambiwa kuchagua biashara ya kufanya hii ya kupangisha sio biashara kabisa, biashara gani hela yako ya mtaji inarudi baada ya miaka 11 🙆
Bora uweke lodge ...wanakupa chako mapema na ikifika asubuhi Saa nne unawagongea waondoke hata kama waliingia Saa nane usiku
 
Back
Top Bottom