Don Vito
JF-Expert Member
- Jul 15, 2018
- 1,340
- 2,092
Hahaaa, watu hawapo serious kabisaKuna mdau hapo juu kampigia hesabu za haraka haraka Kuwa ni milioni 15
Hahaaa, watu hawapo serious kabisaKuna mdau hapo juu kampigia hesabu za haraka haraka Kuwa ni milioni 15
Wala so kiasi hicho! Kituo kidogo chenye pump mbili na underground tanks zisizo zidi Lita 20,000 kiasi cha 60 milioni kinatosha kabisa kukupatia heshima wilayani na hata mikoani Kama mmiliki wa kituo cha mafuta.Yani jinsi unavyozungumzia hiyo biashara utafikir Ni biashara ya machungwa it's cost a billions of money
Siyo lelemama! Sasa sh ngapi? Hasa ndiyo anachotaka kufahamu mtoa mada.Sina taarifa kamili......
Labda ufanye kazi za super dealer... Kwa mfano unapewa kituo ambacho kipo tayari,unakua unauza products zao tu.. Kama Puma,Total au Engen... na unakua unakula hela kwa commission kutokana na mauzo yako.... La sivyo ku operate kituo cha mafuta sio lelemama mkuu
Hii Ni tabia ya sisi watanzania, mtu anakurupuka na kusema tu billion mbili. Wala hajui Kama Kuna categories za vituo, ukubwa wa Tank, mode of operation etc.
Tunapenda kijifanya tunajua kila kitu na kukatishana tamaa.
Kimsingi Kuna two category filling station au kituo kidogo eneo lake lazima liwe so chini ya 600sqm. Walau liwe na pump mbili, ukubwa wa Tank itategemea na uwezo wa mmiliki lakini so chini ya 30,000 liters.
Kuna kituo kikubwa Petrol Service station ambacho eneo lake sio chini ya 2000sqm, pump zaidi ya nne, Kuna car service, restaurant/kiosk.
Kituo kikubwa kinagharimu Kati ya 300 - 400ml kukijenga kidogo Ni Kati ya 90m - 150m kulingana na upatikanaji wa eneo na material.
Matenk Ni Kama 15m lenye ujazo wa 20,000 pump 10 - 15m.
Mafuta unaweza kuingia ubia na wasambazaji ama ukanunua na kuuza.
Kila Lita ina margin Kati ya 65 - 130.
Hivyo unaweza kufanya hesabu zako hapo
Tusikashinane tamaa.
Kama hujui kaa kimya like unachokijua hata Kama Ni kidogo sema lakini kukatishana tamaa
Kiwanja
Kwani kutoka 600ml inabaki ml ngapi kufika bl moja mkuu?Uwanja mil.600! Halafu hapohapo paap bil1.2!
Jamani mbona fedha kiasi cha billion mnakifedhehesha sana kama fedha za kutupatupa chini ovyo kutuza ma harusi wa kwenye maigizo ya kiNaigeria?
Hapo tayari kiwanja umepata, sasa matenki, pampu na mtaji wa mafuta ya kuanzia ndiyo ifike millioni elfu moja(1,000,000,000,000/=) !
Acheni kudharau pesa nyie!
MIMI NILIWAHI KUULIZIA HII BIASHARA KITAMBO SANA NA NILIJIBIWA HIVI;
Mwaka 2014 niliwahi kufanyakazi GAPCO (terminal-kurasini) kipindi hiko Meneja Mkuu alikuwa mzee MOSHA kabla hajastaafu, kuna siku alikuja kukagua matenki kwenye eneo yalipojengwa matenki (farm tank).
Basi tukakutana na kwakuwa yeye alikuwa ndio boss pale akaniuliza maswali kuhusu services za matenki maana yalikuwa yanatakiwa kupigwa rangi upya, katikati ya maongezi nilimuuliza;
‘’ hivi mzee nikiwa na milioni mia sita naweza nikafungua kituo cha kuuza mafuta yaani (petrol station)? Maana haiitwi sheli.... sheli ni jina la kampuni ya kuuza mafuta zamani zileee kama leo ilivyo Total, Puma, Engen, Kobil n.k
Alinijibu hivi;
‘’kijana wangu kama umeuza nyumba ya urithi umepata hiyo pesa ni bora ufanye biashara nyingine tu, hiyo pesa ni kidunchu mno usione watu wanamiliki vituo ukadhani ni biashara ya mzaha! Hiyo pesa kama kweli unataka kufanya biashara ya mafuta labda ukodi kituo cha kampuni yoyote mfano hapa Gapco tukukodishe yaani kila kitu ni mali yetu isipokuwa wafanyakazi na mafuta utakayoweka tu ndio mali yako... tena tunakuuzia kwa masharti halafu kukipata tu hiko kituo lazima ukutane na changamoto’’
Baada ya kuniambia hivyo nikataka kujua kidogo hayo masharti na hizo changamoto zake zipoje?
Akaendelea kusema;
‘’ 1.kwanza mafuta lazima unnue kwenye terminal ambayo inamiliki kituo mfano kama kituo chako ni Gapco huruhusiwi kunnua terminal nyingine hata kama bei imepanda au kukiwa na upungufu wa mafuta inakubidi usubiri sio kunnua kwingne.
2.Mafuta unapangiwa ujazo (lita) za kununua kwa kila mwezi na hiyo ipo kwenye mkataba, mfano unaweza kuambiwa kwa kila mwezi unatakiwa kunnua lita 80,000 ni lazima unnue haijalishi kama hauuzi hiyo ni juu yako lazima unnue kila mwezi.
3.Pamoja na kuwa unanunua mafuta yao lakini kituo unakilipia kodi kama kawaida.
4.Na ili upate wateja wengi lazima uwe na msingi mkubwa yaani biashara ya mafuta mwenye msingi mkubwa ndio mwenye wateja wengi.....kivipi?
Ipo hivi unapouza mafuta kuna watu watanunua kwa cash (hawa huwa hawanunui mafuta mengi) na kuna kampuni ambazo (hazitanunua kwa cash yaani wao wanapohitaji unawajazia unaandika mwisho wa mwezi mnapiga hesabu unalipwa) kampuni hizi utakuta zinamiliki magari madogo, malori au mabasi yanayokwenda mikoani mfano unapata kampuni moja tu ya NEW FORCE hebu fikiria lile basi moja kutoka dar mpaka sumbawanga linatumia lita ngapi? (takribani mia tatu). Halafu jiulize hizo basi zipo ngapi? Zote zije kunyonya mafuta kwako kilasiku halafu malipo ni mwisho wa mwezi utaweza kumudu? (Kumbuka kila mwezi unatakiwa ufikie kiwango cha manunuzi uliyowekewa) ina maana lazima uwe na pesa ya ziada ndio maana nikakwambia kwa hiyo hela yako haitoshi.
5.kupata kituo katika kampuni yoyote ile ni kama kupata nyumba ya NHC utakuta mtu mkataba wake unaisha baada ya miaka mitano ijayo lakini kuna watu wengine si chini ya wanne au watano na wao pia washatoa order ya kukitaka endapo atashindwa biashara au mkataba wake ukiisha...kwa ufupi ili uweze kupata uwe mpambanaji haswaa!
KUMBUKA HII ILIKUWA MWAKA 2014
NA SASAHV GAPCO IMEUZWA INAITWA TOTAL
Hiyo mbona inatosha kabisaAcha utani wewe kituo Cha mafuta hakijengwi kwa pesa ya kununulia nyanya.
Inabaki millioni mia4. Lakini kwa muktadha wa 'komenti' yako inabakia millioni mia6!Kwani kutoka 600ml inabaki ml ngapi kufika bl moja mkuu?
Yaani hadi mda huu nashindwa kuelewa kama pesa yangu inatosha ama hamna maana kila mtu na lake.Siyo lelemama! Sasa sh ngapi? Hasa ndiyo anachotaka kufahamu mtoa mada.
Embu soma vizuri post#101 inaweza ikakusaidia pa kuanzia.Yaani hadi mda huu nashindwa kuelewa kama pesa yangu inatosha ama hamna maana kila mtu na lake.
100 million inatosha kabisa,kama uneshapata eneo, designing, mantaki ya mafuta, pump etc, usitishe watu kwamba 700 million or 2 billionMil. 700 au bil. Mbili!?
Post #48 au #101!?Embu soma vizuri post#101 inaweza ikakusaidia pa kuanzia.
Uwakala wa hizi kampuni unapataje ?Sina taarifa kamili......
Labda ufanye kazi za super dealer... Kwa mfano unapewa kituo ambacho kipo tayari,unakua unauza products zao tu.. Kama Puma,Total au Engen... na unakua unakula hela kwa commission kutokana na mauzo yako.... La sivyo ku operate kituo cha mafuta sio lelemama mkuu
Sory sir! I mean post#48.Post #48 au #101!?
Asante mkuu.Sory sir! I mean post#48.
Andika Kiswahili.it's cost a billions of money
Fafanua vizuri mkuu.Mwaka 2013 Gharama za kuanzisha kituo kidogo ilikua ni roughly 500M hiyo iwe ni maeneo ya porini au vijijini, kwasasa ukiadjst na inflation ongeza M kadhaa hapo, then ingia porini.