Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta ( petrol station )

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,919
2,000
Wakuu nimeamua kuthubutu. Nataka kuanzisha kituo cha kuuzia mafuta (petrol & diesel). Ninapanga kuanza na na pampu mbili tu. Je ni mambo yapi ya msingi ninayopaswa kuzingatia ili kuanzisha kituo?

=============MAJIBU NA MICHANGO============

1596520826301.png

Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine

Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,

So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO

Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA. ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI
 
newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,368
1,500
Hii biashara haina hasara,ni faida tupu.tatizo ni mtaji na ugumu wa kukubalika ktk kilinge cha wenye shelli hizi.

Unataka kuanzisha mkoa gani,bara bara ipi? - Kwa ajili ya equipments,nenda BIG bon msimbazi,wao wanaofisi ya kuuza vipuri na mitambo ya kuuzia mafuta.
 
  • Thanks
Reactions: SDG

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
Mkuu .... ninakushauri kama una eneo ambalo ni potential kwa wateja wa diesel and gasoline(petrol) lililo karibu na highway nenda kwa oil companies zinazo source (oilcom, camel oil, engen, oryx, total, etc) watakupa requirements zao na kuna uwezekano wa kukupa pumps na mafuta kama franchise na kwa mkataba maalum wa malipo ....

Hii ni nzuri kwani hutaangaika kupata mafuta na itakuwa obligation yao wanakupa reliable supply ya mafuta hata kama kuna uhaba wa mafuta kutokana na mkataba wenu, pia uta enjoy marketing yao automatically ..

Kwani kama engen wakifanya advertisement kwenye TV au billboards basi na kama kituo chako ni engen unakuwa umefanya advertisement automatically.

..... vinginevyo utahangaika sana.
 
ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,663
2,000
Nahisi mkuu hii ni baada ya mafuta ya taa juu na wewe ndo unainvest..
biashara njema mkuu ila mwanzo ni mgumu..
 
Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
1,195
Mkuu, jaribu kwenda pale Kariakoo Big Bon (Boa Bank) kuna ofisi zao wana dili na mambo ya Oil Gas watakupa ushauri mzuri wa kitaalamu
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Parachichi

JF-Expert Member
Jul 22, 2008
511
0
Mkuu b'ness nzuri sana! Ila taabu capital!hv inabd uwe na how much ili uanze hii b'ness?
 
  • Thanks
Reactions: SDG

canaan

Member
Mar 1, 2008
46
95
Unahitaji uwe na certificate ya mazingira kutoka Nemc kabla ya kupatiwa leseni na EWURA, so anzia kwanza EWURA watakupa form na maelezo yote ya taratibu za kuanzisha biashara hiyo
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,076
2,000
Salaam kwa wote wana Jf,naulizia hatua za kupitia pia na ni mtaji gani unafaa kuazisha sheli na supermarket pia,nitashukuru mkinisaidia.
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,908
2,000
Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine

Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,

So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO

Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA,

ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI
 
Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,213
2,000
1. utafiti wa eneo husika i.e kipato cha % kubwa ya wakazi wa hapo (location: si lazima ufungue dar au mkoani katikati ya mji)

2. bidhaa zipi zina mahitaaji makubwa based on kipato cha wakazi

3. gharama za uendeshaji

4. utanunua bidhaa kwa bei gani kutoka kwa supplier na utauza kwe bei gani [lengo la supermarket ni kuuza bidhaa kwa beiya chini compared na
wachuuzi] mara nyingi ilikupunguza bei za bidhaa supermarkets huwa wananunua direct kutoka kiwandani

5. ubora wa bidhaa, usijaze bidhaa za china (watu wanapenda kununua vitu supermarket kutokana na uhakika wa ubora). Ni lazima uwe mkweli kwa mteja.

6. mtaji: % kubwa ya watanzania wanaweza kumudu kununua vitu basic kama chakula, usitake masifa kuuza bidhaa za bei kubwa na usijaribu kuiga shoprite, imalaseko, mlimani city wanafanya nini.

7. uaminifu wa wafanyakazi ni tatizo sugu + michezo michafu ya kubadili bidhaa original na fake + kuingiza na kuuza bidhaaa zao ndani ya biashara yako

8. customer care mbovu

9.

10.

mkuu mafanikio mema hii ni moja ya plan zangu za baadae ninaamini nitafanya vizuri kwakuwa mpk sasa bado sijaona mtu aliye serious kwenye mambo ya supermarkets, mimi ninatarajia kuifanya iwe hub for specific products
 
Mkuu kwenye RED hapo hujaona mtu mmoja mmoja au hata makampuni? make kama ni makampuni makubwa yako yalio seriasi mkuu, na wakenya wakiwa ndo Namba moja, na wameanza kuya fungua kama uyoga, pamoja na kuwepo Dar wapo pia Moshi,

ILA ISHU YA CUSTOMER CARE NDO TATIZO KUBWA KABISA KULIKO YOTE
- Kuna siku nimeingia kwenye supermarket moja hivi huku Arusha ni kakuta wale wauzaji wanasukana na wengine wako bise na magazeti ya UDAKU, hii ni picha mbaya sana kwenye swala la wateja

- Na kuna baadhi ya supermarket wanaangalia kwanza umekuja na USAFIRI GANI kama umekuja na V8 hapo utapata mapokezi ya kufa mtu ila kama umekuja na pikipiki au Baiskeli hakuna atakaye kuchangamkia

SO MKUU UKWELI CUSTOMER CARE NDO TATIZO KUBWA SANA, ACHILIA MBALI MASWALA YA MITAJI NA LOCATION NA LEO HII HATA SHOPRITE ZINAENDA KUFA KWA SABABU YA WATUMISHI WAKE
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,076
2,000
Asante kwa ushauri wako nimeupenda,sasa nataka nijue wastani wa mtaji ambao unaweza fikia hatua ya kuanzisha supermarket
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,908
2,000
Hakuna mtaji maalumu wa kuanzisha supermarket, na hata biashara nyingine yeyote ile, hakunaga specifiuc capital, kikubwa ni strategies zako katika kutekereza huo mradi wako.

Unaweza Kuanza na mtaji wowote ule ulio nao, unaweza kuwa na Bilioni 1 bado ukashindwa kuanzisha huo mradi na unaweza kuwa na milioni 100 bado ukaweza kutekereza hiyo miradi yako.
 
Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
6,831
2,000
Mkuu usifanye biashara hizo. Hazina faida. Ila kama una connections na hujali dhuluma, basi unaweza pata faida.
 
Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,213
2,000
komandoo, /QUOTE]

Hizi ni plan za baadae, matarajio ni kuanza na mini market (ya mazao ya kilimo na mifugo) subject to expand, tatizo ndugu zangu watz ukianza kuwaambia mawazo ya kuungana na kumiliki supermarket wanakuona kama mwehu wao wanasubiri waone biashara imesimama kwanza ndio waamini.

Nimeona kwa wenzetu wakiwa na supermarkets nyingi lakini kila supermarket utakuta ina sifa yake ya kipekee, tatizo tz unakuta kila investor anafungua supermarket ambayo ni copy & paste ya mwenzake huku bei zikiwa juu na mtz wa kawaida hawezi kuzimudu... baada ya miaka 2 zinafilisika.
 
Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,213
2,000
Asante kwa ushauri wako nimeupenda,sasa nataka nijue wastani wa mtaji ambao unaweza fikia hatua ya kuanzisha supermarket
Huwa wanaanza na mini market inayokua kidogo kidogo hiyo level ya supermarket ni hatua ya baadae sana na ni hatari sana kuanza nayo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom