TikTok2020
JF-Expert Member
- Oct 20, 2022
- 1,817
- 3,140
Wanajamvi
Taharuki ya kuadimika kwa mafuta ya Petrol na Diesel imeanza tena kama ilivyo ada kila ukifika mwisho wa mwezi
Leo tarehe 27.09.2023 Urambo Tabora Hali si shwari misururu ya madumu kweli sheli yameanza
Inasiktikisha sana kuona wananchi wakiteseka namna hii na serikali tushindwa kutatua tatizo hilo
Kila mwisho wa mwezi inatokea upungufu mkubwa sana wa mafuta na hili linafanyika ili kusubiri beimpya zinazotangazwa kila mwanzo wa mwezi
---
Wananchi wa Urambo mkoani Tabora wakiwa wamepanga foleni kusubiri huduma ya kuuziwa mafuta asubuhi ya leo Jumatano, Septemba 27, 2023 katika moja ya kituo cha mafuta katikati ya mji huo.
Kwa mujibu wa wakazi, foleni ya mafuta Urambo ni tatizo sugu lililodumu kwa takribani miezi mitatu sasa huku ufumbuzi wake ukiwa bado haujajulikana.
Urambo yenye vituo vitatu pekee vya mafuta, petroli inauzwa kwa gharama ya Sh 3,331 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh 3,377.
"Changamoto ya mafuta ni kubwa hapa Urambo, inatuchukua dakika mpaka 45 wakati mwingine kufikia foleni yako ya kujaza mafuta, tunawahi asubuhi angalau foleni ni ndogo. Tuna miezi mitatu sasa hatujui ni lini changamoto hii itakoma," amesema Omary Juma mwendesha gari dogo ya mizigo maarufu 'Kirikuu'.
(Imeandikwa na Herieth Makwetta)
Tuna safari ndefu sana.