Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

Acha utani wewe kituo cha mafuta hakijengwi kwa pesa ya kununulia nyanya.
Punguza ujuaji nkamu haya sasa weka kiwango chako
Shida mmezoea sifur zinapoongezwa
Million 700 inatosha kuanza kituo cha mafuta ten hapo parefu mno pump nne andaa milio 30-40
Kisima chini miundo mbinu yake 10 million mpaka 20

Paa na wiring itategemea Ila kama la kisasa sana weka m50

Afu gari za kubeba mzigo tanks mbili au moja inatosha Ila mbili inakupa unafuu weka 300m
Hapo unanza kazi vibali hongo weka 50
 
Mkuu tofauti ya filling station na service station ikoje?
Kujenga/building filling station ukiwa na 150m unaweza...

Kujenga service station, uwe na 350m and na kuendelea kulingana na services utakazotoa, ukubwa wa majengo, wingi na ukubwa wa matenki etc..

Kwenye kuendesha, hapo sijui, ila utahitaji not less than 200m kununa stock ya mwanza ya mafuta, mishahara, EWura permits na OSHA


Watu wanadanganyana sana hasa kwenye ujenzi, which is not as they say
 
Hongo
Punguza ujuaji nkamu haya sasa weka kiwango chako
Shida mmezoea sifur zinapoongezwa
Million 700 inatosha kuanza kituo cha mafuta ten hapo parefu mno pump nne andaa milio 30-40
Kisima chini miundo mbinu yake 10 million mpaka 20

Paa na wiring itategemea Ila kama la kisasa sana weka m50

Afu gari za kubeba mzigo tanks mbili au moja inatosha Ila mbili inakupa unafuu weka 300m
Hapo unanza kazi vibali hongo weka 50
 
Japo faida naona ni ndogo sana
Acha uongo.

Faida ni kubwa mno. Labda serikalini wakuwekee kizingiti cha mambo ya kodi.

Ukiwa sehemu nzuri unauza almost lita 2000 tena high way.

Hapa mjini unauza hadi lita 5000 kwa siku.
 
Faida kwenye mafuta ni 200 au chini ya hapo.
Acha uongo.

Faida ni kubwa mno. Labda serikalini wakuwekee kizingiti cha mambo ya kodi.

Ukiwa sehemu nzuri unauza almost lita 2000 tena high way.

Hapa mjini unauza hadi lita 5000 kwa siku.
 
MIMI NILIWAHI KUULIZIA HII BIASHARA KITAMBO SANA NA NILIJIBIWA HIVI;

Mwaka 2014 niliwahi kufanyakazi GAPCO (terminal-kurasini) kipindi hiko Meneja Mkuu alikuwa mzee MOSHA kabla hajastaafu, kuna siku alikuja kukagua matenki kwenye eneo yalipojengwa matenki (farm tank).
Basi tukakutana na kwakuwa yeye alikuwa ndio boss pale akaniuliza maswali kuhusu services za matenki maana yalikuwa yanatakiwa kupigwa rangi upya, katikati ya maongezi nilimuuliza;
‘’ hivi mzee nikiwa na milioni mia sita naweza nikafungua kituo cha kuuza mafuta yaani (petrol station)? Maana haiitwi sheli.... sheli ni jina la kampuni ya kuuza mafuta zamani zileee kama leo ilivyo Total, Puma, Engen, Kobil n.k

Alinijibu hivi;
‘’kijana wangu kama umeuza nyumba ya urithi umepata hiyo pesa ni bora ufanye biashara nyingine tu, hiyo pesa ni kidunchu mno usione watu wanamiliki vituo ukadhani ni biashara ya mzaha! Hiyo pesa kama kweli unataka kufanya biashara ya mafuta labda ukodi kituo cha kampuni yoyote mfano hapa Gapco tukukodishe yaani kila kitu ni mali yetu isipokuwa wafanyakazi na mafuta utakayoweka tu ndio mali yako... tena tunakuuzia kwa masharti halafu kukipata tu hiko kituo lazima ukutane na changamoto’’

Baada ya kuniambia hivyo nikataka kujua kidogo hayo masharti na hizo changamoto zake zipoje?

Akaendelea kusema;
‘’ 1.kwanza mafuta lazima unnue kwenye terminal ambayo inamiliki kituo mfano kama kituo chako ni Gapco huruhusiwi kunnua terminal nyingine hata kama bei imepanda au kukiwa na upungufu wa mafuta inakubidi usubiri sio kunnua kwingne.
2.Mafuta unapangiwa ujazo (lita) za kununua kwa kila mwezi na hiyo ipo kwenye mkataba, mfano unaweza kuambiwa kwa kila mwezi unatakiwa kunnua lita 80,000 ni lazima unnue haijalishi kama hauuzi hiyo ni juu yako lazima unnue kila mwezi.
3.Pamoja na kuwa unanunua mafuta yao lakini kituo unakilipia kodi kama kawaida.
4.Na ili upate wateja wengi lazima uwe na msingi mkubwa yaani biashara ya mafuta mwenye msingi mkubwa ndio mwenye wateja wengi.....kivipi?
Ipo hivi unapouza mafuta kuna watu watanunua kwa cash (hawa huwa hawanunui mafuta mengi) na kuna kampuni ambazo (hazitanunua kwa cash yaani wao wanapohitaji unawajazia unaandika mwisho wa mwezi mnapiga hesabu unalipwa) kampuni hizi utakuta zinamiliki magari madogo, malori au mabasi yanayokwenda mikoani mfano unapata kampuni moja tu ya NEW FORCE hebu fikiria lile basi moja kutoka dar mpaka sumbawanga linatumia lita ngapi? (takribani mia tatu). Halafu jiulize hizo basi zipo ngapi? Zote zije kunyonya mafuta kwako kilasiku halafu malipo ni mwisho wa mwezi utaweza kumudu? (Kumbuka kila mwezi unatakiwa ufikie kiwango cha manunuzi uliyowekewa) ina maana lazima uwe na pesa ya ziada ndio maana nikakwambia kwa hiyo hela yako haitoshi.
5.kupata kituo katika kampuni yoyote ile ni kama kupata nyumba ya NHC utakuta mtu mkataba wake unaisha baada ya miaka mitano ijayo lakini kuna watu wengine si chini ya wanne au watano na wao pia washatoa order ya kukitaka endapo atashindwa biashara au mkataba wake ukiisha...kwa ufupi ili uweze kupata uwe mpambanaji haswaa!
KUMBUKA HII ILIKUWA MWAKA 2014
NA SASAHV GAPCO IMEUZWA INAITWA TOTAL
Amekuwa realistic.
 
Your Ideal Budget

Land plot size 4400 sq m or 1 acre (depending on location)
= 30 Million

Storage tanks
:

One diesel tank of 25,000 liters capacity = 10 million
One petrol tank capacity 10,000 liters. = 7 million
17 Million

Dispensing pumps:


- One product, one nozzle. = 12 million
- Two products, two nozzles. = 17 million
29 million

Legal Costs including NEMC, EWURA, etc

= 8 million

Initial working capital for diesel and petrol.

= 72 million

9 kg dry powder fire extinguisher.
= 0.13 million

Standby generator (5 KVA).
= 2 million
74.13 Million

Initial salary for employees:


Manager = 0.8 million

Supervisor = 0.4 million

Pump attendant = 0.2 million

Watchman = 0.1 million

Sweeper = 0.1 million
= 1.5 Million


Furniture including sofa, carpet, desktop computer, chairs, tables, etc.
= 2.5 Million

1 canopy

= 30 million

Miscellaneous

= 3 Million

One electronic fiscal device (EFD).

= 0.86 Million
> Total Cost TZS 195 Million


NOTE: In this budget, I didn’t include construction costs of office buildings, toilets, and floors as it depends on how you want your station to be. I recommend you to hire a petrol station contractor who will help in designing and estimating your construction costs.
This is perfect.
 
Nimejitahidi kuusoma uzi huu kwa umakini...kwani hata mm nafikiria kufanya biashara hii kama ntabarikiwa.... kwa maelezo na takwimu za wadau....nimegundua ukiwa na 500m unaweza kujenga na kuazisha kituo kikubwa cha kuanzia pump nne....bado sijapata maelezo ya kutosha kuhusu faida katika biashara hii....faida ikoje wadau?
 
Nimejitahidi kuusoma uzi huu kwa umakini...kwani hata mm nafikiria kufanya biashara hii kama ntabarikiwa.... kwa maelezo na takwimu za wadau....nimegundua ukiwa na 500m unaweza kujenga na kuazisha kituo kikubwa cha kuanzia pump nne....bado sijapata maelezo ya kutosha kuhusu faida katika biashara hii....faida ikoje wadau?
500m nyingi sana mkuu kwa kuanzia
 
Back
Top Bottom