Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

mkuu 'sheli' ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, TOTAL, OILCOM, CAMEOIL nk. maneno sahihi ni 'kituo cha mafuta' au kwa kinyasa 'petrol station'

Jamani neno sheli limetoholewa na kuingizwa kwenye misamiati ya kiswahili mara baada ya kuonekana linatumika sana hivyo kiswahili fasaha cha neno 'Fuel station ni 'Sheli'
 
sio petrol station ni 'fuel station' sababu pale hawauzi petrol peke yake. Kuna petrol,diesel,kerosene,gas na hata mkaa na kuni wanaruhusiwa.

Wewe nawe umeyumbisha inaitwa "Petrol filling station" kwasababu mafuta yote yanayopatikana hapo yana asili ya petroli. Hata makaa ya mawe ni fuel, kuni ni fuel, gas ni fuel etc.... Though tumetoka nje ya mada kulingana na uhitaji wa alie anzisha hii thread.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
mkuu hii inaitwa kasoro juu ya kasoro. kwa taarifa yako neno 'petrol linasimama kwa niaba ya mafuta ya aina zote (mafuta ya nishati). ukiona lori la mafuta limeandikwa 'petroleum usije ukadhani limebeba mafuta ya petroli tu, hua yanabeba aina tofauti kama vile mafuta ya taa na dizeli. na sector yenyewe inaitwa petroleum and gas. bila shaka nimekuongezea ujuzi dogo

sio petrol station ni 'fuel station' sababu pale hawauzi petrol peke yake. Kuna petrol,diesel,kerosene,gas na hata mkaa na kuni wanaruhusiwa.
 
mkuu hii inaitwa kasoro juu ya kasoro. kwa taarifa yako neno 'petrol linasimama kwa niaba ya mafuta ya aina zote (mafuta ya nishati). ukiona lori la mafuta limeandikwa 'petroleum usije ukadhani limebeba mafuta ya petroli tu, hua yanabeba aina tofauti kama vile mafuta ya taa na dizeli. na sector yenyewe inaitwa petroleum and gas. bila shaka nimekuongezea ujuzi dogo

kwahiyo haya magari yetu yalio mengi yanatumia Gas ila wengi tunayaita magari ya petrol sindio??
 
  • Thanks
Reactions: SDG
wakuu, hamtendi haki hata kidogo, jamaa kaja na wazo lake , badala ya kufocus na alichokiomba kusaidiwa, tumehamisha maada halisi na kuanza kunyumbulisha vitu. please guys mwenye uelewa wa namna ya kujenga hiyo hiyo SHELI, aje hapa atoe mwongozo, watu wengi tutafaidika na hili.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Heshima yenu wakuu, msaaada mwenye kujua gharama za kufungua sheli ya mafuta, nataka nifanye hii biashara niko mkoani tatizo sijui pakuanzia wapi, mtaji sio tatizo, mwenye mchanganuo plz share,mbarikiwe sana

samahani mtaji ulonao ni Kiasi gani?
 
Inategemea na ukubwa kituo unachotaka kufungua. Lakini vituo standard ya kati ni 250-300million
 
  • Thanks
Reactions: SDG
mkuu hii inaitwa kasoro juu ya kasoro. kwa taarifa yako neno 'petrol linasimama kwa niaba ya mafuta ya aina zote (mafuta ya nishati). ukiona lori la mafuta limeandikwa 'petroleum usije ukadhani limebeba mafuta ya petroli tu, hua yanabeba aina tofauti kama vile mafuta ya taa na dizeli. na sector yenyewe inaitwa petroleum and gas. bila shaka nimekuongezea ujuzi dogo
TANZANIA PETROLIUM DEVELOPMENT CORPORATION-TPDC shirika la maendeleo ya petroli tanzania,ni hao hao wanacontrol utafiti 1wa gesi na mafuta,be it diesel or kerosene or petrol, i think the difference comes at the time of processing,in my opinion petrol embraces other products
 
Naomba data za uhakika kwa mwekezaji anapenda kuanzisha kituo cha mafuta cha kisasa kwa ajili ya uuzaji wa petrol, diesel, kerosene na lubricants apa apa nchini TANZANIA. Swali langu linahusisha wazo la designing kituo icho, usalama wa mahali pa uuzaji (safety measures) na haswa upatikanaji wa bidhaa hiii kwa hapa kwetu TANZANIA

Nakaribisha michango yenu wadau
 
Naomba data za uhakika kwa mwekezaji anapenda kuanzisha kituo cha mafuta cha kisasa kwa ajili ya uuzaji wa petrol, diesel, kerosene na lubricants apa apa nchini TANZANIA.Pia mwenye ujuzi wa kudesign kituo icho cha mafuta, anaweza kunipa wazo la designing na usalama wa mahali pa uuzaji (safety measures)Nakaribisha michango yenu wadau

Mkuu inataka kwenda peponi lakini hutaki kufa.
 
TAFAKURU, Hongera kwa wazo lako na azima ya kutaka kuanzisha hiyo biashara. Richa ya kuomba ushauri na lujifunza hapa JF bado kuna umuhimu wa kuwaona wataalamu wa Planning and designing ya miradi, ili mchekeche wazo lako kwa pamoja na pia wakufanyie kitaalamu wewe ibaki kutekeleza tu kwa kadri utakavyo shauriwa. Bahati mbaya wajasaliamali wengine hawathamini mchango wa washauri wa masuala haya. Kushauriwa haimanishi tu mshauriwa hajui bali kuongeza utaalamu katika suala husika ili malengo yafikiwe, ndo maana hata taasisi huwa na wataalamu wao lakini hutafuta washuari wengine nje ya ofisi.

Mradi wako ni mzuri na mkubwa kiasi chake, unahitaji Planning na designing yenye commitment ya hali ya juu. Hapa JF unapata disorganized information zenye mashiko lakini bado utahitaji kukaa na kuzichambua vema kiuhalisia wa mradi wako. Usiogope gharama za Planning stage ya biashara yako, ni hatua mhimu sana.

Tembelea blog hii kwa ushauri zaidi: KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
 
Habari za passover wakuu,
Kutokana na kuongezeka kwa vyombo vya usafiri hasa bodaboda nimeona oppoturnity ya kufungua petrol station kule kwetu kwa mpaka sasa ni wachuuzi wachache ambao wanapanga mafuta barabarani kwenye vidumu ndio wanaotoa huduma hiyo tena kwa bei ya juu tsh 2500/litre ya petrol sasa wakuu naomba mnijuze ni mtaji kiasi gani unatakiwa ili niweze kumiliki petrol station na taratibu zikoje na masuala ya kodi manake huko ndiko kunasumbua, bei ya zile pump na upatikanaji wake, matank n.k.

Nitashukuru kwa michango yenu.
 
Hongera kwa wazo zuri la kibiashara ila kuanzisha kituo kipya itakuchukua kama mwaka mzima hivi kuweza kukamilisha kila kitu hadi kufungua kituo.

hatua ya kwanza ni kupata eneo la kuweka kituo lililotengwa kwa ajili ya biashara hiyo, ya pili unatakiwa kwenda halmashauri kuomba kibali cha ujenzi, tatu utaenda Fire kupata certificate ya kujenga kituo, nne itakubidi ufanye Environmental impact assessment, ukishapata certificate unaenda Ewura kwa ajili ya vibali. baada hapo ndio unaweza kuanza kujenga kituo.

kuna watu huwa hawafuati hizo taratibu ila huwa kuna shida zake na hasa kwa kipindi hiki.

kujenga kituo standard ambacho hutopata shida ya ewura kwa kijijini ni kama 150m.
 
nashukuru sana mkuu nadhani 150 ni kituo kilichokamilika
 
Back
Top Bottom