Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine
Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,
So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO
Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA. ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI
1. utafiti wa eneo husika i.e kipato cha % kubwa ya wakazi wa hapo (location: si lazima ufungue dar au mkoani katikati ya mji)
2. bidhaa zipi zina mahitaaji makubwa based on kipato cha wakazi
3. gharama za uendeshaji
4. utanunua bidhaa kwa bei gani kutoka kwa supplier na utauza kwe bei gani [lengo la supermarket ni kuuza bidhaa kwa beiya chini compared na
wachuuzi] mara nyingi ilikupunguza bei za bidhaa supermarkets huwa wananunua direct kutoka kiwandani
5. ubora wa bidhaa, usijaze bidhaa za china (watu wanapenda kununua vitu supermarket kutokana na uhakika wa ubora). Ni lazima uwe mkweli kwa mteja.
6. mtaji: % kubwa ya watanzania wanaweza kumudu kununua vitu basic kama chakula, usitake masifa kuuza bidhaa za bei kubwa na usijaribu kuiga shoprite, imalaseko, mlimani city wanafanya nini.
7. uaminifu wa wafanyakazi ni tatizo sugu + michezo michafu ya kubadili bidhaa original na fake + kuingiza na kuuza bidhaaa zao ndani ya biashara yako
8. customer care mbovu
9.
10.
mkuu mafanikio mema hii ni moja ya plan zangu za baadae ninaamini nitafanya vizuri kwakuwa mpk sasa bado sijaona mtu aliye serious kwenye mambo ya supermarkets, mimi ninatarajia kuifanya iwe hub for specific products
Asante kwa ushauri wako nimeupenda,sasa nataka nijue wastani wa mtaji ambao unaweza fikia hatua ya kuanzisha supermarket