Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,769
- 10,650
Wakuu nimeamua kuthubutu. Nataka kuanzisha kituo cha kuuzia mafuta (petrol & diesel). Ninapanga kuanza na na pampu mbili tu. Je ni mambo yapi ya msingi ninayopaswa kuzingatia ili kuanzisha kituo?
=============MAJIBU NA MICHANGO============
=============MAJIBU NA MICHANGO============
Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine
Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,
So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO
Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA. ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI