Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

asanteni kwa ushauri wenu,nitaufanyia kazi pia kama mna zahidi la kuongea naomba mueendelee kushauri,kwani natumaini kuna watu wengine apa pia wangependa kujua,mbarikiwe
 
hizi ni plan za baadae, matarajio ni kuanza na mini market (ya mazao ya kilimo na mifugo) subject to expand, tatizo ndugu zangu watz ukianza kuwaambia mawazo ya kuungana na kumiliki supermarket wanakuona kama mwehu wao wanasubiri waone biashara imesimama kwanza ndio waamini.
nimeona kwa wenzetu wakiwa na supermarkets nyingi lakini kila supermarket utakuta ina sifa yake ya kipekee, tatizo tz unakuta kila investor anafungua supermarket ambayo ni copy & paste ya mwenzake huku bei zikiwa juu na mtz wa kawaida hawezi kuzimudu... baada ya miaka 2 zinafilisika.

True mkuu, hilo ndo Tatizo na hii inasababishwa na UMIMI, kila mtu anaona bora amiliki DUKA, Unakuta mtaa unawakazi 400 kuna maduka 30 hapo ndo ujiulize,
Na kuanza na mazao ya kilimo na mifigo na vizuri kabisa, tena inatosha kabisa,
 
Mkuu usifanye biashara hizo. Hazina faida.
Ila kama una connections na hujali dhuluma, basi unaweza pata faida.

Mkuu ni biashara GANI isiyo kuwa na faida, chocote kinacho itwa biashara ni lazima iwe nafaida bila kujalisha ni kiasi gani cha FAIDA

Na hata hivyo ili kutengeneza FAIDA inategemena na huduma yako, make huduma ndo inadetermine FAIDA
 
Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine

Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,

So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO[\color] ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO

Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA,

ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI


Mkuu sahihisho kidogo. Shell ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, PUMA, GAPCO n.k. Ukisema sheli ya Gapco ni sawasawa na kusema BP ya GAPCO.
 
Mkuu sahihisho kidogo. Shell ni kampuni ya mafuta kama ilivyo BP, PUMA, GAPCO n.k. Ukisema sheli ya Gapco ni sawasawa na kusema BP ya GAPCO.

Shell ni kati ya kampuni zilizoanza biashara hizi kwa hapa nchini filling station zote kibongo-bongo tulisummerrize kwa jina hilo shell..
 
Mkuu Pamoja na location ambayo kutoka na UFISADI haifuatwi kwa sasa, ila kuna mambo mengine

Zile kampuni za mafuta kama Total, Lake oil, BP, GAPCO na kazalika ukienda na Proposal ya kueleweka huwa wanakujengea na wewe unakua unauza tu mafuta na ukienda kinyume na Sheria zao wana kunyang'anya sheli mida hiyo hiyo hawana mchezo,

So kuna wanao jenga vya kwao wenyewe na kuna vya Makampuni, na vingi vyenye Majina ya watu binafisi au sehemu uje ni mtu mwenyewe kajenga, Mfano JUMA PETRO STATION, SERENGETI FILLING STATION, hivi huwa ni vya watu binafsi, ila vile vyote vyenye majina ya Makampuni kama vile TOTAL, GAPCO, CAMEL. LAKE OIL, BP, na vinginevyo hizi vimejengwa na wenye makampuni na wanao uza ni menegment tu na mwisho wa siku wanakulipa kamisheni ya kuuza, na hapa kama Sheli ni ya GAPCO ukiuza mafuta ya TOTAL inakula kwako mazima, NA UNALAZIMIKA KUUZA NA GRESE ZAO, OIL ZOTE MBILI NA MAFUTA YA BREAK YA KAMPUNI YAO

Ila kama sheli umejenga wewe mwenyewe una mamlaka ya kuuza mafuta ya kampuni yeyote ile iwe SPACE OIL, LAKE OIL NA KAZALIKA,

ISHU ZA KUWEKA SUPEMARKET NI MANJONJO YA WEWE ULIE PEWA JUKUMU LA KUUZA MAFUTA, ILA KISHERIA BADO NI HATARI INGAWA WAPO WANAO WEKA HADI GEST SHELI

Nimeupenda mtiririko wako jinsi ulivyojibu big up
 
Nakubaliana na hoja za baadhi ya wadau, mimi binafsi ni agent wa viwanja hasa hivyo vya sheli na supermarket na nimeona jinsi wanavyofanya. kuna namna 2 mosi ukiisha pata eneo unaweza waona kampuni mama ile ambayo ungependa uuze bidhaa yao . na wao watakujengea na kuweka pump ila visima unachimba kwa gharama zako. na kituo kikikamilika unatakiwa kudiposit $ 300,000 kwenye fixed account kwa muda fulani, ndipo wao watakuwa wanakupa mafuta na wewe unachukua commission kwa muda fulani hv. njia ya pili ni kujilipua kila kitu unanunua cha kwako na jina la kituo linakuwa la kwako
 
naomba kufahamu kama nshajenga kituo changu cha kuuzia mafuta, je natakiwa kuwa na vitu gani kabla ya kwenda ewura kupata leseni....cjui pa kuanzia jamani...msaada..munitajie vitu ntakavyokwenda navyo ewura....


Msaada jamani naona kama muda unakimbia napoteza muda.....
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna aina mbili za hivyo vituo!aina kwanza jenga cha kwako....kwa standard ya (seek ushauri kwa Oilcom,Gapco,Total etc) ambao watakuuzia hayo mafuta!unakuwa unatumia logo yao .....ukishajenga kituo,unaweka deposit kwao mnaanza biashara!unaletewa mzigo ukiuza unapeleka hela yao ww unabakia faida....wanaleta tena!ila lazima uweke deposit kama 150m hivi!ama la uwe unanunua cash bin cash...hakuna kuchagua kampuni ya kukuuzia!unaenda popote na kununua mzigo unamwaga na kuuza!wajuzi zaidi wakiamka watakumwagia zaidi!subiri
 
kuna aina mbili za hivyo vituo!aina kwanza jenga cha kwako....kwa standard ya (seek ushauri kwa oilcom,gapco,total etc) ambao watakuuzia hayo mafuta!unakuwa unatumia logo yao .....ukishajenga kituo,unaweka deposit kwao mnaanza biashara!unaletewa mzigo ukiuza unapeleka hela yao ww unabakia faida....wanaleta tena!ila lazima uweke deposit kama 150m hivi!ama la uwe unanunua cash bin cash...hakuna kuchagua kampuni ya kukuuzia!unaenda popote na kununua mzigo unamwaga na kuuza!wajuzi zaidi wakiamka watakumwagia zaidi!subiri

sasa ili nianze ya kwangu mwenyewe nijenge na kununua na kuuza kwa business name yangu mwenyewe niwe na nini...natakiwa kuwa na nini b4 naenda kuomba leseni kule ewura? Nafikiri umenielewa mkuu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Heshima yenu wakuu, msaaada mwenye kujua gharama za kufungua sheli ya mafuta, nataka nifanye hii biashara niko mkoani tatizo sijui pakuanzia wapi, mtaji sio tatizo, mwenye mchanganuo plz share,mbarikiwe sana
 
Back
Top Bottom