Mohamedex121
JF-Expert Member
- Jan 27, 2022
- 1,688
- 3,142
Habarini wakuu. Naimani humu nyote ni wazima wa afya. Nilikuwa naomba msaada ya kisheria.
Kuna hili suala la migogoro ya wanafamilia hasa kwenye mirathi ambayo huathiri jamii kwa namna moja ama nyingine na sijui suluhisho ni lipi?
Familia nyingi hasa hizi kwenye jamii zetu unakuta ni familia kubwa zenye ndugu wengi. Ni jambo la kawaida kukuta familia moja kuwa na watoto kumi au zaidi.
Mbali na hayo familia nyingi huwa ni masikini na ni ngumu sana kukuta watoto wengi wa familia moja kuwa na maisha mazuri, unaweza kuta ni mtoto mmoja ama wawili ndio wenye maisha mazuri
Na hili suala la kuwajengea nyumba wazazi kipindi ambacho Mungu amekubariki huwa haliepukiki kwa mtoto mwenye kuwapenda wazazi wake, hii inakuwa kama shukurani kuwapa wazazi na pia kuwapa hifadhi .
Swali langu linakuja apa, hivi ikitokea mtoto akamjengea nyumba mzazi wake na kwenye hati kuandika jina la mzazi wake, je pindi mzazi anapokufa mali zinarudi kwa mtoto aliyemjengea au zinakuwa za familia na kugawana mirathi??
Natanguliza shukurani wakuu.