Njia pekee kukwepa mgawanyo wa mali za ndoa ni kuandika majina ya watoto

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
NJIA PEKEE KUKWEPA MGAWANYO WA MALI ZA NDOA NI KUANDIKA MAJINA YA WATOTO.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu katika Rufaa Na.102/2018 kati ya Gabriel Nimrod Kurwijila Vs Theresia Hassan Malongo inasema kuwa mali iliyoandikwa jina la mtoto haiwezi kugawanywa na wanandoa pale ndoa inapovunjika.

Kwa wale wanandoa ambao wasingependa kugawana mali basi mnaweza kuandika majina ya watoto katika kila mali mnayonunua.

Hii ni bora sana na itakuwekeni na amani katika mali mnazochuma pamoja kuliko mnavyofanya kuviziana, kufichana, usiri usiri ,na wakati mwingine kuandika majina ya wazazi na ndugu.

Niliwahi kukuandikieni kuwa kuandika jina la mzazi sio salama sana sababu mzazi naye anaweza kuoa ama kuolewa mali zako zikaenda kwa mama au baba wa kambo, pia mzazi anaweza kufuja mali hizo, na pia mzazi akifa ni vigumu kuwashawishi ndugu zako na warithi wake halali kuwa mali zilikuwa zako. Watapenda mgawane mirathi.

Aidha, usisubiri ndoa ivunjike ndio uje kusema mali ni za watoto, laa hasha. Ama kusema tu 'hizi mali ni za watoto' bila kuwaandika majina ni kupoteza muda na kudanganyana.

Tunachosema hapa ni kuwa andika majina ya watoto, msiishie kusema. Ikiwa hazijaandikwa majina ya watoto zinahesabika ni za wazazi na ndoa ikivunjika ni lazima zigawamywe kwa wazazi. Muda huu huruhusiwi kusema mali ni za watoto.

Kitu pekee kinachokubaliwa kuwa mali fulani ni ya watoto ni ile mali kuwa imeandikwa majina ama jina la mtoto basi.

Mahakama inasema kitendo cha wazazi kuandika jina la mtoto maana yake ni kuwa ilikuwa dhamira ya wazazi kumpa mtoto ile mali na hivyo ni yake.

Na haijalishi umri wake, na pia ni.sawa mali moja kuandikwa mtoto zaidi ya mmoja, hata watano wanaweza kuandikwa katika mali moja, sheria imeruhusu.

Hii ikusaidieni kuacha kuviziana, usiri usiri wa mali mwishowe udhulumiwe nk.
 
Yaan mali zangu niweke mtoto

Mtoto yake ni Elimu tu mengine akapambane

Halafu sasa hivi hebu tuzungumzie bandari mali za ndoa acha watajuana wenyewe
 
Back
Top Bottom