Mahakama yawatengua wasimamizi mirathi ya bilionea Mrema akiwemo Michelle Mrema

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha imetengua wasimamizi wa mirathi ya bilioni 18.3 ya mali za Marehemu, Melau Mrema aliyefariki mwaka 2017 na kumteua mtoto wa marehemu Randle Mrema kuwa Msimamizi wa mali .

Akisoma hukumu hiyo katika shauri dogo namba 170 la mwaka 2022 lililofunguliwa na Randle Mrema pamoja na Lulu Mrema dhidi ya waliokuwa wasimamizi wa mirathi Janeth Kimaro na Viv Mrema na Michelle ambaye alishawai kugombea ubunge kupitia Ccm umoja wa vijana ambao pia ni watoto wa marehemu Mrema.

Jaji Devota Kamzora alisema kuwa mahakama imezingatia sababu zilizotolewa na waleta maombi ikiwa ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wa mali kushindwa kukusanya mali na kulipa madeni pamoja na udanganyifu .

Sababu zingine zilizotolewa na waleta maombi ni kujimilikisha mali kwa manufaa binafsi pamoja na kutoelewa majukumu yao na kushindwa kugawa mali kwa wanufaika hukunwakifanya udanganyifu kwenye nyaraka kuwa wamegawanya wakati wanaufaika hawana habari.

Marehemu Mrema alifariki Julai 30,2017 na kuacha mali mbalimbaki yakiwemo nyumba za kupangisha, Mashamba,hoteli,magari , viwanja ,hisa kwenye mabenki,fedha Tasilimu pamoja na miradi ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni nk.

Katika maamuzi ya jaji Kamzora alisema mahakama imegundua kuwa waliokuwa wasimamizi wa mirathi walishindwa kueleza zilipo fedha za kodi za majengo zinazolipwa na wapangaji pamoja na hisa za marehemu katika benki ya CRDB katika kipindi cha miaka minne.

Pia mahakama imebaini kuwa kiasi cha sh,bilioni 1.8 kilichokuwa benki hazijulikani zilipo.

Pia waliokuwa wasimamizi wa mirathi walishindwa kuithibitishia mahakama namna walivyogawa mali za marehemu kwa wanufaika na kulipa madeni licha ya wao kuwasilisha nyaraka zinazoomesha kuwa waligawanya mali za marehemu kwa usawa.

Mahakama ilibaini kuwa licha ya wasimamizi kufunga mirathi lakini bado waliendelea kujinufaisha na mali hizo kwa manufaa yao binafsi.

Katika mwenendo wa shauri hilo Mahakama ilibaini udanganyifu wa mgawanyo wa mali halisi za marehemu baada ya kughundua mali zingine zenye thamani ya sh bilioni 15.5 zilikuwa hazijaorodheshwa .

Katika utetezi wa wajibu maombi kupitia wakili wao George Njooka waliieleza mahakama kuwa walishagawa mali za marehemu kama takwa la sheria linavyosema.

Wakili Njooka alisema kuwa kumekuwepo na ugumu katika familia hiyo kutokana na mgogoro wa kifamilia uliopo na hivyo kusababisha wasimamizi wa mirathi kushindwa kutekeleza majukumu yao vizuri.

Alisema sababu nyingine iliyosababisha wao kutokamilisha kukusanya na kugawa mirathi ya marehemu kwa wakati ni pamoja na ukubwa wa madeni na kesi zilizokuwa zikiendelea mahakamani kuhusiana na mali za marehemu.

Kabla ya maamuzi hayo wakili Njooka aliieleza mahakama athari zinazoweza kujitokeza iwapo mahakama itabatilishwa uamuzi wa wasimamizi wa mirathi ni pamoja na kutasababisha gharama kubwa pasipo na msingi

Katika maamuzi ya jaji Kamzora alitengua walimamizi waliokuwepo na kumteua Randle Mrema akishirikiana na Lulu Mrema kuwa wa simamizi wa mali za marehemu na kutoa miezi sita kuhakikisha wamwkamilisha kukusanya ,kulipa madeni na kugawa mali za marehemu kwa wanufaika .Hata hivyo mahakama ilisema iwapo kama kuna mali iliuzwa kiuzembe inaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani.

Akiongea nje ya mahakama msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na Mahakama, Randle Mrema ambaye ni mtoto wa marehemu, alisema amepokea uamuzi huo kwa furaha lakini anaona ana deni kubwa la kurekebisha yale yote yaliyotarajiwa kufanywa na wasimamizi waliopita .

Alisema amejipanga kukamilisha kulipa madeni, kufufua biashara zilizokuwa zimekufa ikiwa ni pamoja na hoteli lakini kushirikiana bega kwa bega na wakurugenzi wengine kwenye makampuni ambayo marehemu alikuwa mmiliki.

............
kesi-pic%20(1).jpg
 
Mabilionare wa Arusha hao! Ninyi kila mwenye hela bilionea!:D:D:D:D:D:D
Sasa huoni yanaongelewa mabilioni mkuu?

Kwa wakazi wa Arusha na Kilimanjaro Mrema alikuwa mtu mkubwa sana.

Kumbuka utawala wa Kikwete semina na warsha mbali mbali za serikali zolifanyikia hoteli ya Mrema iitwayo Ngurdoto.

East Africa na ule mkutano wa Sulvan ulifanyikia pale.

Kwa kifupi huyu marehemu alikuwa na vitega uchumi vingi sana.
1. Ngurdoto
2. Impala hotel
3. Naira spring hotel.
4. Mashamba makubwa sana ya kahawa tena sehemu muhimu sana.
 
"kwenye msiba wa fukara mambo huwa shwari, lakini kwa mwenye mali ni matatizo, ufikia hata ndugu kutoelewaana"

Suleiman mbwembwe huyo, katika ngoma ya nitakaza moyo.
Ottu kwenye ubora wao.
Huu mgogoro ndani yake kuna watoto waliokayaa shile na lazi walikuwa wakilewa tu, baada ya Mrema kutangulia sasa wameshtuka wachukue chao mapema.

Bushmamy anaweza kutujuza zaidi
 
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha imetengua wasimamizi wa mirathi ya bilioni 18.3 ya mali za Marehemu, Melau Mrema aliyefariki mwaka 2017 na kumteua mtoto wa marehemu Randle Mrema kuwa Msimamizi wa mali...
Mali bila daftari...
 
Marehemu Mrema ninamfahamu vizuri sana

Tangu hajawa tajiri yaani alipokuwa Dobi wa yule Mhindi aliyemtajirisha pale jirani na Clock tower miaka ya 1990 -1993 na akawa muuza vijago tena anaweka chini

Then akawa dereva tax wakati anaishi kwenye ile nyumba pale marangu bar kona ya Florida kuelekea Seliani Hospital na kununua tax 4 zilizoandikwa Meridians kama jina la Guest House yake hapohapo Florida wakati ule

Tatizo kubwa la Mrema ni " Kuwa na Watoto wengi sana"

Watoto wake wameshakuwa, baadhi wamesoma na baadhi hawakusoma lakini wote wanaona kuwa wana haki ya kudai urithi wa baba yao....huku wamezidiwa akili na dada yao Mkubwa ambaye alishapiga pesa za Ngurdoto na anataka kufungua hotel yake

Amini, Usiamini kuna kipindi miaka ya 2000 mwanzoni Mrema alikuwa na Mini School Bus inajaza watoto wake tu kuwapeleka Arusha School na Green Acres

Mrema ana watoto sio chini ya 30 kwa wanawake tofauti

Ila kwa kazi jamaa hakuwa mvivu, he was so active kwenye kazi, kwa mfano alikuwa anaamka saa 10 usiku pale Impala wakati tunapeleka kuku na sausage anapiga mahesabu yake mpaka saa 3 halafu mchana anaenda kulala

Mrema alikuwa hafanyi kazi mchana, anakuwa amelala nyumbani then usiku anafanya kazi mpaka kufuta meza na madirisha ya Impala Hotel

Kuzaa zaa sana nje bila kuweka misingi inayoeleweka ni tatizo sana kwetu Wanaume

Mdogo wake nipo naye hivi sasa

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Mali ya baba inatuoa roho bora nikaeee peembeni ,niinusuru roho ................huo ndio msondo ngoma siwezi lala bila kibao chao
 
Marehemu Mrema ninamfahamu vizuri sana

Tangu hajawa tajiri yaani alipokuwa Dobi wa yule Mhindi aliyemtajirisha pale jirani na Clock tower miaka ya 1990 -1993 na akawa muuza vijago tena anaweka chini

Then akawa dereva tax wakati anaishi kwenye ile nyumba pale marangu bar kona ya Florida kuelekea Seliani Hospital na kununua tax 4 zilizoandikwa Meridians kama jina la Guest House yake hapohapo Florida wakati ule

Tatizo kubwa la Mrema ni " Kuwa na Watoto wengi sana"

Watoto wake wameshakuwa, baadhi wamesoma na baadhi hawakusoma lakini wote wanaona kuwa wana haki ya kudai urithi wa baba yao....huku wamezidiwa akili na dada yao Mkubwa ambaye alishapiga pesa za Ngurdoto na anataka kufungua hotel yake

Amini, Usiamini kuna kipindi miaka ya 2000 mwanzoni Mrema alikuwa na Mini School Bus inajaza watoto wake tu kuwapeleka Arusha School na Green Acres

Mrema ana watoto sio chini ya 30 kwa wanawake tofauti

Ila kwa kazi jamaa hakuwa mvivu, he was so active kwenye kazi, kwa mfano alikuwa anaamka saa 10 usiku pale kampala wakati tunapeleka kuku na sausage anapiga mahesabu yake mpaka saa 3 halafu mchana anaenda kulala

Mrema alikuwa hafanyi kazi mchana, anakuwa amelala nyumbani then usiku anafanya kazi mpaka kufuta meza na madirisha ya Impala Hotel

Kuzaa zaa sana nje bila kuweka misingi inayoeleweka ni tatizo sana kwetu Wanaume

Mdogo wake nipo naye hivi sasa

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
Kuzaa sana ni changamoto ila wengi huona ni ufahari
 
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha imetengua wasimamizi wa mirathi ya bilioni 18.3 ya mali za Marehemu, Melau Mrema aliyefariki mwaka 2017 na kumteua mtoto wa marehemu Randle Mrema kuwa Msimamizi wa mali .

Akisoma hukumu hiyo katika shauri dogo namba 170 la mwaka 2022 lililofunguliwa na Randle Mrema pamoja na Lulu Mrema dhidi ya waliokuwa wasimamizi wa mirathi Janeth Kimaro na Viv Mrema na Michelle ambaye alishawai kugombea ubunge kupitia Ccm umoja wa vijana ambao pia ni watoto wa marehemu Mrema.

Jaji Devota Kamzora alisema kuwa mahakama imezingatia sababu zilizotolewa na waleta maombi ikiwa ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wa mali kushindwa kukusanya mali na kulipa madeni pamoja na udanganyifu .

Sababu zingine zilizotolewa na waleta maombi ni kujimilikisha mali kwa manufaa binafsi pamoja na kutoelewa majukumu yao na kushindwa kugawa mali kwa wanufaika hukunwakifanya udanganyifu kwenye nyaraka kuwa wamegawanya wakati wanaufaika hawana habari.

Marehemu Mrema alifariki Julai 30,2017 na kuacha mali mbalimbaki yakiwemo nyumba za kupangisha, Mashamba,hoteli,magari , viwanja ,hisa kwenye mabenki,fedha Tasilimu pamoja na miradi ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni nk.

Katika maamuzi ya jaji Kamzora alisema mahakama imegundua kuwa waliokuwa wasimamizi wa mirathi walishindwa kueleza zilipo fedha za kodi za majengo zinazolipwa na wapangaji pamoja na hisa za marehemu katika benki ya CRDB katika kipindi cha miaka minne.

Pia mahakama imebaini kuwa kiasi cha sh,bilioni 1.8 kilichokuwa benki hazijulikani zilipo.

Pia waliokuwa wasimamizi wa mirathi walishindwa kuithibitishia mahakama namna walivyogawa mali za marehemu kwa wanufaika na kulipa madeni licha ya wao kuwasilisha nyaraka zinazoomesha kuwa waligawanya mali za marehemu kwa usawa.

Mahakama ilibaini kuwa licha ya wasimamizi kufunga mirathi lakini bado waliendelea kujinufaisha na mali hizo kwa manufaa yao binafsi.

Katika mwenendo wa shauri hilo Mahakama ilibaini udanganyifu wa mgawanyo wa mali halisi za marehemu baada ya kughundua mali zingine zenye thamani ya sh bilioni 15.5 zilikuwa hazijaorodheshwa .

Katika utetezi wa wajibu maombi kupitia wakili wao George Njooka waliieleza mahakama kuwa walishagawa mali za marehemu kama takwa la sheria linavyosema.

Wakili Njooka alisema kuwa kumekuwepo na ugumu katika familia hiyo kutokana na mgogoro wa kifamilia uliopo na hivyo kusababisha wasimamizi wa mirathi kushindwa kutekeleza majukumu yao vizuri.

Alisema sababu nyingine iliyosababisha wao kutokamilisha kukusanya na kugawa mirathi ya marehemu kwa wakati ni pamoja na ukubwa wa madeni na kesi zilizokuwa zikiendelea mahakamani kuhusiana na mali za marehemu.

Kabla ya maamuzi hayo wakili Njooka aliieleza mahakama athari zinazoweza kujitokeza iwapo mahakama itabatilishwa uamuzi wa wasimamizi wa mirathi ni pamoja na kutasababisha gharama kubwa pasipo na msingi

Katika maamuzi ya jaji Kamzora alitengua walimamizi waliokuwepo na kumteua Randle Mrema akishirikiana na Lulu Mrema kuwa wa simamizi wa mali za marehemu na kutoa miezi sita kuhakikisha wamwkamilisha kukusanya ,kulipa madeni na kugawa mali za marehemu kwa wanufaika .Hata hivyo mahakama ilisema iwapo kama kuna mali iliuzwa kiuzembe inaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani.

Akiongea nje ya mahakama msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na Mahakama, Randle Mrema ambaye ni mtoto wa marehemu, alisema amepokea uamuzi huo kwa furaha lakini anaona ana deni kubwa la kurekebisha yale yote yaliyotarajiwa kufanywa na wasimamizi waliopita .

Alisema amejipanga kukamilisha kulipa madeni, kufufua biashara zilizokuwa zimekufa ikiwa ni pamoja na hoteli lakini kushirikiana bega kwa bega na wakurugenzi wengine kwenye makampuni ambayo marehemu alikuwa mmiliki.

............View attachment 2770595

Halafu unakuta marehemu alikuwa anajibana sana kutumia hela asije akafirisika.
 
Back
Top Bottom