Msaada: Nina Millioni 10 itatosha kujenga nyumba?

Msaada: Nina Millioni 10 itatosha kujenga nyumba?

Nina jua ninajua chongumza nina uzoefu na hizi kazi,nyumba ndogo ya kawaida vyumba vitatu haiwezi maliza tofari 3,000 ambazo ni sawa na 3,000,000.nyumba ya vyumba vitatu haiwezi maliza mabati 100 tuseme kila bati 15,000 inakula 1,500,000.tofauri 3,000 kujengea haziwezi maliza mifuko 50 @13,000 inakuja 650,000 hapo bado fundi wa ujenzi let say 900,000 unabakiza hela mbao za kuezekea na mchanga na fundi wa kuezeka,piga jumla kama hapo 10M imekwisha au bado
Madirisha,grills,vyoo/bafu,mashimo ya maji taka,plumbing na fundi wake,umeme na vifaa vyake na fundi wake,gypsum na ufundi wake,tiles,makabati ya jikoni. Hebu nipe gharama ya hivi vitu maanake wengi mnaweka gharama ya boma ambayo kwenye ujenzi ndio kitu rahisi. Nyumba nyingi zinakwama kwenye finishing. Kama mnazungumzia boma 10m inatosha.
 
Hizo pesa zitatosha hata nyumba ya vyumba vitatu self contained yaani choo, bafu, jiko, sebule na kavaranda. Cha kuzingatia ni lazima design yake iwe very compact, built up area isizidi 54 square meters. Tumia matofali ya kuchoma. Tumia changarawe kwenye base ya floor. Msingi tumia matofali ya cement au mawe kutegemea yapi ni nafuu huko kwenu. Tumia mabati ya kawaida ya gauge 30, dari la kawaida, wiring ya kawaida, plumbing ya rahisi, plastering ya cement, rangi ya maji kwenye ukuta na ceiling board za kawaida, madirisha na milango ya kawaida achana na aluminium windows. Tumia fundi mmoja wa kawaida na vibarua wasiozidi 2. Cesspit za rahisi.

Note; Design ndiyo most important, unaweza kupata ushauri kwa mafundi. Hususani chumba cha kulala 2.5m by 3m kinatosha, sitting room 3m by 3.5m, master bedroom 3m by 3m, jiko 2m by 2.5m, bafu cum choo 1.5m by 2m, stoo 2m by 2m.
Afadhali wewe umesema atumie vitu vya kawaida. No gypsum,no aluminium windows,no tiles etc.
 
Afadhali wewe umesema atumie vitu vya kawaida. No gypsum,no aluminium windows,no tiles etc.
Hivyo vitu atakuja kuweka miaka ya baadaye kama mambo yatakuja kumnyookea. Hata hiyo nyumba ataweza kuja kuipanua na kuwa kubwa zaidi au kui demolish na kujenga ghorofa. Cha mhimu kwa sasa awe na nyumba yake inayolingana na uwezo wake wa sasa. Ya kesho hakuna anayeyajua, anaweza akafulia kabisa. Hiyo 10m aliyoipata asiitumie kwa anasa za pombe na michepuko, itakwisha sasa hivi.
 
Madirisha,grills,vyoo/bafu,mashimo ya maji taka,plumbing na fundi wake,umeme na vifaa vyake na fundi wake,gypsum na ufundi wake,tiles,makabati ya jikoni. Hebu nipe gharama ya hivi vitu maanake wengi mnaweka gharama ya boma ambayo kwenye ujenzi ndio kitu rahisi. Nyumba nyingi zinakwama kwenye finishing. Kama mnazungumzia boma 10m inatosha.
Nilisema kwenye post yangu ya awali hiyo hela itatosha kuinua boma na kuezeka,nikamwambia finishing atafanya pole pole wakati tayari nyumba imeshasimama
 
Nilisema kwenye post yangu ya awali hiyo hela itatosha kuinua boma na kuezeka,nikamwambia finishing atafanya pole pole wakati tayari nyumba imeshasimama
Anaweza kumwona Msanifu majengo akamlipa kidogo akamchorea nyumbba ambayo atajenga kwa phase wakati akiishi ndani ila kiuhalisia mil 10 si ndogo ila itamkwamisha
 
Mdogo wangu,
Hongera kwa kudunduliza hiyo 10 M.
Kabla sijakushauri labda niulize kwanza
1. Una kiwanja?
2. Kipo eneo ambalo linafikika kirahisi?
3. Nyumba ina tafsiri pana, unataka nyumba ya aina gani ?Ukubwa na unatumia materials gani kujenga(specs na schedule of materials). Kwa baadhi ya nyumba milioni 10 ni bei ya Mlango tu na kwa baadhi unajenga na chenji inabaki.

Note: Milioni kumi ni nyingi sana lakini pia milioni kumi ni kidogo sana kutegemeana na aina ya nyumba unayotaka.
 
By experience inatosha chumba na seble tu tena usiwe na madoido.
 
Watu ambao hamjawahi kujenga ndio mpo mbele kumkatisha mwenzenu tamaa. Milion 10 inatosha kuanza ujenzi. Unaweza kuanza ujenzi wa nyumba ndogo ya kawaida ya vyumba vitatu, sebure ,jiko na dinning ILA hauwezi kumalizia kwa pesa hiyo hiyo, jenga itakapoishia jipange tena taaratibu utajikuta umekuwa mwenye nyumba. Kumbuka maisha ni nyumba bila kuwa na sehemu nzuri ya kuishi ni ngumu kupata maendeleo.

Ni ukweli mtupu kiongozi
 
Ujenziii unahitaji moyo,anza taratibu ila kwa mkoa wangu ingejenga bila mawazo.maana tofali ya kuchoma inahusika
 
Habar zenu wana jf naombeni msaada kimawazo na ushauri mm nina 10 mil nataka kuzielekeza kwenye ujenzi angalau kajumba kadogo na mm niwe na kwangu. Hiyo pesa niliyonayo je inaweza tosha naombeni msaada tafadhari
Inatosha mkuu mimi nimejenga kwa 8m tu ila kadogo dogo
 
Mdogo wangu,
Hongera kwa kudunduliza hiyo 10 M.
Kabla sijakushauri labda niulize kwanza
1. Una kiwanja?
2. Kipo eneo ambalo linafikika kirahisi?
3. Nyumba ina tafsiri pana, unataka nyumba ya aina gani ?Ukubwa na unatumia materials gani kujenga(specs na schedule of materials). Kwa baadhi ya nyumba milioni 10 ni bei ya Mlango tu na kwa baadhi unajenga na chenji inabaki.

Note: Milioni kumi ni nyingi sana lakini pia milioni kumi ni kidogo sana kutegemeana na aina ya nyumba unayotaka.
Kiwanja ninacho mkuu na panafikika kirahisi sana , pia nyumba ni ndogo kama chumba jiko sebule
 
Back
Top Bottom