Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Doto12

JF-Expert Member
Nov 2, 2023
268
568
Sehemu ya 1.

sina budi kuendeleza hii stori.

Iko hivi wife na mimi tulifahamiana Kijijini. Nilikuwa F6 yeye akiwa F4 leaver. Nilimsaidia akapata Chuo cha Takwimu akaenda akafanya akapata cheti. Wakati akiwa chuo tulioana, mimi nilikuwa nafanya kazi. Miaka mitatu baadae tulijaaliwa watoto wazuri.

Maisha yaliendelea nikiwa kazini na yeye akiwa ofisi moja masuala ya takwimu nchini. Mambo ya ndoa yalikuwa safi sana nili enjoy ndoa labda kwa sababu ilikuwa ya kusafiria. Maana yeye mkoa mimi mkoani. Nilifanikiwa kumuhamishia mkoani kwangu yeye na watoto. Tuliishi vizuri kwa wastani wa miaka 5.

Baadae Mama yake akapitia wakati mgumu, tukashauriana tumjengee kibanda. Kwa kuwa wapo watoto wakubwa wakaona washirikiane wote. Kwa kuwa wife ndiye mwenye kipato kizuri akakopa Benki Milioni 27 lakini nyumba haikuisha.

Kero ikaanza sasa. Kila wakati anataka pesa ya Ujenzi kwa Mama Mkwe. Majuzi alipata bingo Ofisini kwao (Milioni 20) ni pesa ya offer ya Serikali yenye riba kidogo. Lahaulaaa!! Si akaipeleka yote kwenye ule ujenzi.

Wana JF wenzangu, kumbuka si kwamba sisi na Watoto wetu hatuna mahitaji, hapa ada, nyumba haijaisha asilimia Mia. Why apeleke Milioni 20 kwao? Hivi? Hajui ile nyumba hawataishi watoto wake? Ndani ni kuchuniana.

Najuta sana kuoa mwanamke huyu.



Sehemu ya 2
 
Pole mkuu, nakushauri tu muache mkeo ajenge kwao! Na wewe Jenga kwako! Mwanaume hudumia familia yako kwa kuhakikisha wanaishi pahala pazuri na panapofaa!

Acha na hela ya mkeo maana SIYO YAKO

Mimi nilikopa fedha nikajazia ujenzi wa nyumba anayojenga mume wangu maana ni familia moja, matokeo yake amekuja kunitemgenezea maneno ya kashfa machafu yasiyo faa!

Mkopo ukiisha, nachukua mwingine na NITAJENGA KWETU ili siku tukiachana niende kwetu kwa raha! Wanaume mna matatizo sana ACHA MKEO AJENGE KWAO, wewe Jenga KWAKO.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Ndoa nyingine ni utapeli ,nakushauri mkae chini muwajengee watoto wenu ,kujenga nyumba ya ndugu sijui mzazi kma mnataka ya kifahari utaumia na usitegemee pesa ya mke.

Maisha gani kama majambazi mnaviziana..

Fanyeni muwajengee watoto wenu mapema msije kuwapa mitihani baadae waje kuwajengea nyie ,mwanamke akishajenga kwao hapo atakuletea nyodo maana kashapata pa kukaa.
 
Back
Top Bottom