Msaada: Nina Millioni 10 itatosha kujenga nyumba?

Msaada: Nina Millioni 10 itatosha kujenga nyumba?

nimemaliza kujenga nyumba wiki iliyopita hata mil.5 haijaisha! sasa hivi nakaribia kuweka solar ninaemjengea ahamie....kuwa makini na mafundi uchwara.
 
nimemaliza kujenga nyumba wiki iliyopita hata mil.5 haijaisha! sasa hivi nakaribia kuweka solar ninaemjengea ahamie....kuwa makini na mafundi uchwara.
Umetumia tofali ngapi, bati ngapi,madirisha mangapi,mbao za kupaua ngapi,vyoo na bafu,kitchen fittings? Labor charge?
 
nimemaliza kujenga nyumba wiki iliyopita hata mil.5 haijaisha! sasa hivi nakaribia kuweka solar ninaemjengea ahamie....kuwa makini na mafundi uchwara.
Wap mkuu maan nipo hapa dsm mm
 
Mimi ninaweza kukusaidia ndugu mawasiliano yangu ni 0755284410 na 0659422357 mfano ukipata nyumba kama hii unaweza fanikiwa. Hii ni moja ya kazi zangu maana mimi ni designer wa majengo
3D_001.png
 
Bafu,vyoo,plumbing,vifaa vya umeme,tiles?
1.Kiwanja 2,500,000 unapata
2.Tofali 6' 2000×1000=2,000,000
3.Fundi 800,000
4.Mbao 1,200,000
5.Bati 60×15,000=900,000
6.Fundi kupaua 300,000
7.Dirisha chuma 80,000×4=320,000
8.Mirango 5×100,000=500,000
9.Cylingboard 20×14,000=280,000
10.Mbao cylingboard 600,000
11.Kufitisha 400,000
12.Cement 30×13,000=390,000
13.Mchanga kazi yote 340,000
Total=11,030,000.
Halo ni kwamba umenakshi kila kitu.
Uzoefu wangu kwa hapo ni dodoma, Arusha ndani ya 15km.
Dar na mwanza sipajui.
Fungi simamia mwenyewe na manunuzi fundi akutume wewe mwenyewe.
Angelis usikwamishwe kama una 10ml kipindi hiki cha jpm unaweza fanya lolote.
Mafanikio mema.
 
Hiyo help inatosha rena inatosha Sana tu tatizo watu asilimia kubwa wanapigwa sana na mafundi na kwenye material...fanya hivi unapo patana na fundi usikubaliane kuwa ajenge nyumba nzima kwa kiasi kadhaa...hapo utapigwa mana atakwambia nyumba nzima kujenga milioni tano au tatu mfano..bado material hadi hapo hela utakuta ishakata..bado hela ya maji ya kujengea. Hela ya kuchimba msingi..bado hela ya kujaza kifusi ndani etc..cha kufanya mwambie fundi ntakulipa kwa tofari mpe ramani ya hiyo nyumba kabla hamja kubaliana bei muulize nyumba kama hii itachukua tofari ngapi..akikupa jibu mwambie sasa mm nataka nikulipe kwa kila tofari moja shilingi 350.. Hiyo ndio bei ya juu kbs..baada ya hapo unakuta fundi huyo huyo ana tafuta mafundi wengine ana wauzia tofari moja shilingi 200 hadi 250.. Kwenye vifaa nenda mwenyewe usitume mtu na wakati wa ujenzi komaa mwenyewe site mwanzo hadi mwisho..watu mna pigwa arf mna kuja kujisifia nime jenga nyumba kwa gharama sana..hapo fundi kalamba tyr milioni 6.. Wakati tunao juwa ujenzi hiyo nyumba ukicheki gharama yake haifiki hata milioni moja na nusu poleni sana..ndugu kwa hela hiyo una jenga tena unajenga sana..achana na hao wanao kukatisha tamaa..mm nipo kwenye hiyo sekta ya ujenzi najua kwa nn hao wana kwambia hivyo..kitu cha kufanya usipatane na fundi kichwa kichwa utalia..kila raheli[emoji120]
 
Bei zake zikoje mkuu, maana kuna fundi nilimpata nikataka anitolee kitu cha vyumba vitatu ananiambia 4m ikabidi nisitishe kwanza
Unaona sasa...mwambie fundi kwa ramani hiyo..itachukua tofari ngapi akikupa idadi ya tofari..mwambie ntakulipa kila tofari kwa shilingi 300 au 350...kwanza ukimwambia hvyo atajua upo vzr kwenye mambo ya ujenzi..kingine usiende kwa hao mafundi wanao jiita mafundi wakuu wakati wakifika site hawafanyi kazi hata kidogo sana sana nao wana wauzia kazi mafundi wadogo..tafuta fundi mdogo mpe kazi achana na hao wanao jiita mafundi wakuu..uone kama gharama itakuja hivyo
 
Somo zuri mkuu live long
 
Asante sana mkuu kwa ushauri umenipa mwanga, hilo la kusema fundi mkuu inawezekana ndio nilikutana naye maana 4m sio mchezo kwa hali ya sasa
 
nimemaliza kujenga nyumba wiki iliyopita hata mil.5 haijaisha! sasa hivi nakaribia kuweka solar ninaemjengea ahamie....kuwa makini na mafundi uchwara.
Nyumba hiyo ambayo hata mil 5 haijaisha ina vyumba vingapi? je umefanya finishing ya plasta nje na ndani? ni ya tofali za block?
 
Inawezekana mkuu tena nyumb nzur isipokuwa n wapi unahengaaa mkuuu
 
Habar zenu wana jf naombeni msaada kimawazo na ushauri mm nina 10 mil nataka kuzielekeza kwenye ujenzi angalau kajumba kadogo na mm niwe na kwangu. Hiyo pesa niliyonayo je inaweza tosha naombeni msaada tafadhari
Kama kiwanja unacho na nyumba ndogo ya kawaida let say room tatu na sebure unajenga boma na kuezeka,finishing utafanya kidogo kidogo
 
Nyumba hiyo ambayo hata mil 5 haijaisha ina vyumba vingapi? je umefanya finishing ya plasta nje na ndani? ni ya tofali za block?
Hawa wanaosema wamejenga kwa 5m hamna hata mmoja alietoa mchanganuo.
 
Afu chini afunge matairi ya trekta,asee ni ubunifu mkuu maana si Tanesco wala Dawasco(kama Dar) wataenda kudai bili zao,lazima wasahau tu wakidhani ni Gari LA mizigo[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Ahaahaa..Nyie watu wa humu jamvini bwana...sasa hapo umemsaidia nini Mdau. NDIO WAZO HILO?
 
Back
Top Bottom